Vetting system ya viongozi ilishindwaje kumchuja Ole Sabaya?

Nimekuelewa fika mkuu, lakini huna hoja.
Ati kwa sababu mtu wa awamu ya kwanza alitenda maovu basi iwe ruksa kutenda maovu sasa.
Tunafahamu baba yake Lengai Ole Sabaya ni mmoja wa waliotenda mabaya miaka hiyo, and he got away with it.
Nasisitiza, hujanielewa. Ila wewe ng'ang'ania tu kuwa umenielewa.
 
Mkuu umesahau ,mwendazake alikua ashauriki mkuu ,alisema ukimshauri ndo waalibu kila kitu
 
Kujuana, kuwekana... kazi maalum!!!
 
Hizo sababu za kukata jina la Sabaya ndiyo sababu zilizofanya Marehemu Pombe akampenda na kumteusa ili amtumie kwenye mission zake chafu.
 
Jamaa alikuwa na tatizo, litajulikana tu, muda ukifika.
We acha tu mkuu, hata wasaidizi wake ni vile wapo Kimia ila wenda wameyapitia mengi , unaamuka hasubui ujui mwenda zake ana nini kichwani mwake juu yako, Maisha ya digdig ,kabla ya kufanya Jambo unajiuliza ivi sijui bwana yule litampendeza hata Kama lipo kisheria, lo MWENDAZAKE bwana
 
Hapi mpaka alikuwa anamtisha JK eti atamshughulikia, pumbafu kabisa
Hatari sana mtoto huyu alijisahau....akaanza kutukana mamba mto hajavuka eti atamtwanga JK daaaa dharau kubwa sana....
 
Mkuu Jidu, wakati mwingine inakuwa rahisi tu kukujibu hapa bila ya kujisumbua na yaliyo ndani ya mada yenyewe, pamoja na kwamba mada itakuwa na maelezo mhimu zaidi, kufuatia kichwa kinachoyabeba.

Hivi kweli mkuu bado unaamini kwamba kuna hiyo "vetting" unayoisemea hapa?

Sasa hivi, wengi wetu tumekwishatambua ni kiasi gani nchi yetu ilivyo wazi (vulnerable). Tunaweza kuongozwa na mtu yeyote toka chini hadi juu kabisa ya uongozi wa nchi kwa viongozi mapandikizi tu!

Nchi yetu hii haina uwezo tena wa mchujo wenye vigezo makini.

Watu wanaingia tu madarakani, hata misimamo yao haijulikani, kwa sababu hawajawahi kutoa msimamo popote pale katika uongozi wao. Watu hawa wanachoweza vizuri sana ni kujificha nyuma ya watangulizi wao, bila ya kuonyesha dalili zozote za kuwa na mawazo tofauti wanayoyaamini wao.
Kazi yao kubwa ni maslahi yanayotokana na nafasi zao.

Inapotokea sasa pakawa wazi..., hapo ndio sasa hujionyesha wanakosimamia. Wananchi hawana nafasi ya kuhoji, kwa sababu utaratibu huo haupo.

Kama hatujapata pandikizi hadi wakati huu, basi kuna hatuko mbali.

Nchi yetu imevurugika sana. Mifumo iliyosifika kwamba tunayo, haijulikani imepotelea wapi!

Tatizo tulilonalo, hata tukipata viongozi mapandikizi Tanzania, hawakosi manazi wa kuwapigia zumari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…