Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Imeatangazwa kuwa tawi la Alqaeda la Afrika Magharibi linajulikano kama AQIM limemchagua muAlgeria Abu Obaida Yusuf al-Annabi aliyekuwa mjumbe baraza la watukufu wa tawi hilo kuchukua nafasi ya Abdelmalek Droukdel aliyekuwa kiogozi wake aliyeuliwa na majeshi ya Ufaransa mwezi Juni nchini Mali kutokana na mashambulizi ya majeshi ya Ufaransa nchini humo.
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa taasisi ya kimarekani iitwayo SITE monitoring group ambayo ni maalum katika kufuatilia harakati za wanamgambo wa kiislamu maeneo mbali mbali duniani.
Tawi hilo la AQIM lilionesha video ya maiti ya kiongozi wao aliyefariki na mashambulizi hayo muda mfupi kabla ya kumtambulisha kiongozi wao mpya.
Bwana Annabi kabla ya hapo amekuwa akioneshwa kwenye video mara kwa mara akihamasisha mashambulizi kwa askari wa kifaransa.
Uchaguzi huu mpya wa tawi la Alqaeda umekuja sambamba na mahojiano aliyofanyiwa hivi karibu mjomba wa kiongozi aliyepinduliwa na kuuliwa wa Libya kanali Gadafi.Akiwa nchini Misri mjomba huyo Ahmed Kadhaf al-Dam ambaye alikuwa mshauri wa Gadafi katika mambo ya kiutawala na balozi wa Libya amesema yako makundi ya kiislamu yaliyotajwa kuwapo nchini humo lakini hakumbuki kuwepo mujahidina wala wenye imani kali mpaka pale habari hizo zilipotajwa na viongozi wa Ufaransa na Marekani wa wakati huo.
Viashiria vya uongo wa taarifa za ISIS,ALSHABAAB,BOKOHARAM na Alqaeda ni hivi :
1.Kwanza kama kweli vikundi hivyo vinaongozwa na waislamu viongozi wake wangekuwa ni wataalamu wa lugha ya kiarabu.Lugha ya kiarabu inajitosheleza kimaana haraka na hivyo matumizi ya vifupisho kama AQIM,ISIS na majina mengi yenye vifupisho vya namna hiyo hayawezi kuwa yametokana na waislamu.
2.Kama ni mkutano wa kuchagua viongozi ulifanyika wapi na ulihudhuriwa na nani.
3.Hizo vidio za matamshi ya viongozi hao mbona hazionekani popote na hata ukiingia kwenye mtandao wa SITE hakuna kitu.Kwa kukosekana kwa picha halisi vyombo vya habari hurudia picha hiyo hiyo iliyopigwa eneo fulani miaka na miaka kama kwamba hao waliokuwemo hawajazeeka.
4.Inapoelezwa wanagambo hao wamesema kwenye mtandao wao.Huo mtandao anuwani yake ni ipi ili na wengine wathibitishe.Kama mtandao upo nani host wake na nani analipia name server ili mtandao uendelee kuwa hewani.Kwa sababu hakuna mtandao unaokwenda hewani bila kujulikana na ICAN . Kama anajulikana anayelipia kwanini asifuatiliwe akaonesha mapango ya walipo wenzake wanaoteka na kuuwa wanadiplomasia wa magharibi na ili waokolewe wale wanaowashikilia.
5. Iwapo kila siku wanamgambo wa kiislamu wanapigwa na kuzingirwa kwanini vita havina mwisho.Wao hawashindi na wala hawashindwi.
Kwa kukosa majibu masuali hayo ni dalili ya kuwepo watu wanaotuchezea akili zetu na wanaoupaka matope uislamu na wanaopata sababu za kuendeleza vita maeneo mbali mbali duniani kwa maslahi yao.
Na kwanini iwapo taarifa hizo haziaminiki na hazina chanzo madhubuti kwa nini wanahabari wanazipa umuhimu na hawasemi kama tulivyowaambia wauza barakoa kwamba wakawatangazie mama na baba zao kwanza.