Viatu na Kivuli cha Magufuli kwa Tanzania ya Samia - Kuna cha Kuhofia?

Umerudia kuandika kwenye magazeti? kama kipindi cha Mkapa na Kikwete? Yule Nzi atarudi sasa sio?? Ukabira ni kitu kibaya sana ni ngumu kwa waafrika kujinasuwa,miaka yoote hiyo upo Marekani bado una ukabira na udini? Ama kweli ukichukuwa fimbo na kuitia Baharini, it would never become a fish...
 
Nataka ninukuliwe vizuri kabisa ...legacy ya JPM ni ngumu kuivaa! Huko mbele atakumbukwa kuliko hata alivyozikwa! Tena wasiompenda sasa ndio wataoanza kukiri na kutubu! Naomba mtunze hii comment.
Chadema wanaponda kwamba JPM hana la kukumbukwa nalo, wamejikuta wameamia ccm kumuunga mkono Samia wakifikiri wanamkomoa mtu aliye kaburini.

Mimi nawaambia kuna siku itatakiwa sauti ya mamlaka kunyoosha mambo na itakosekana watu watamlilia Magufuli kama kwenye msiba wake.

Mama Samia tayari ni rais wa kwanza mwnamke hiyo ndio legacy yake kubwa ambayo aina mjadala.

JPM atakumbukwa kama kiongozi mwenye ujasiri, mthubutu, mtu asiyetaka mzaha na raslimali za watanzania na anayepigania tabaka la chini lifaidi matunda ya nchi yao. Huyu mtu wa hivi kuna siku atakosekana.
 
Sawa kabisa,,ya magufuli wao tupa kulee
 
Mwanakijiji nimependa sana andiko lako, limesheni mambo mengi ya busara na hekima na ushauri mwema.

Nimefurahi sana matokeo ya upinzani kwa mama Samia, amepokewa kwa bashasha na upendo wa hali, pia ameonyeshwe ushirikiano. Yaliyobaki tunamwachia yeye atuthibitidhie kilichopo kifuani na kichwani mwake ( ndani ya moyo na akili yake )

JPM tulimpokea kwa kukataa matokeo ya Uchaguzi na kutaka kuitisha maandamano nchi nzima kulazimisha matokeo yafutwe na uchaguzi urudiwe.
Tulipinga hatua zake nyingi za kisiasa alizochukua na tulizibeza hatua zake za kiuchumi alizochukua. Yawezekana tulimuonyesha hatumtaki tangu mwanzo na kumlazimisha achague upande wa kuegemea. Yeye akaamua kama alivyo amua, yawezekana sisi ndio tulimsukuma awe mkamiti juu yetu.

Mama Samia ame pata wa saa mzuri wa kurekebisha mapungufu ya mtangulizi wake na kutuonyesha upendo ambao tuliusahau.
Unapomkosoa mwenye má lakini ni vizuri kujivunia kumtupa na, kumbe za, kumdhihaki na kumdharau kwa kuwa lazima tujuwe yeye anaweza kubembeleza na kuadhibu.

Pamoja na yote hayo muda ni mwalimu mzuri, tumepata elimu ya kutosha kupitia Rais aliyepita kwa pande zote mbili kwa ujumla wetu, Watawaliwa na Watawala.
 
Reactions: Ame
Hahitaji kuvaa viatu vilivyoachwa na mtu ambavyo vinanuka. Vitamuambukiza magonjwa ya miguu. Nasema hivi, Magufuli amefariki biashara yake imeisha. Hayo mambo ya kuambiana sijui viatu kama alivisahau huku duniani basi mpelekeeni haraka maana hatuvihitaji hata kidogo. Mama yetu Samia ameshanunua vya kwake vipyaaaaa!
 
Atakumbukwa kama kiongozi aliyevunja misingi ya umoja wa Taifa letu iliyojengwa kwa muda mrefu , ikalindwa na kutetewa kwa gharama kubwa

Atakumbukwa kwa kuua taasisi za nchi na yeye kuwa taasisi peke yake.

Atakumbukwa kwa kushindwa kuthamini utu hata kutotishika viroba na sandarusi zilipookotwa mto Ruvu na Coco Beach.

Atakumbukwa kama kiongozi aliyejenga chuki na ukanda.
Kiongozi anayesimama na kusema ni wakati wa kanda fulani kusubiri maendeleo ni ajabu

Orodha ni ndefu
 

Uko sawa na mitazamo yangu, siku 100 tutapata picha halisi ya uongozi wake.
 
Nataka ninukuliwe vizuri kabisa ...legacy ya JPM ni ngumu kuivaa! Huko mbele atakumbukwa kuliko hata alivyozikwa! Tena wasiompenda sasa ndio wataoanza kukiri na kutubu! Naomba mtunze hii comment.
Never! Yani ikifikia point naanza kumkumbuka Jiwe SIJUI!
 
Yani nikwambie ukweli. Magufuli atakumbukwa kwa matukio ya hovyo kutokea ndani ya utawala wake. Hakuna la zaidi na ndiyo maana Mungu aliamua amuondoe. Hivi nawaza eti angekuja kuandika na yeye kitabu chake. Hahahahahahaaaa huyu kiongozi ama kwa hakika alikuwa zaidi ya katili!
 
Kinyungu, Kinyungu. Naomba ujue ya kwamba, mapenzi yangu kwa JPM are "untainted".
Ni kweli kabisa maana ulifaidika na utawala wake wa kidhalimu, kwa kuwa member wa lile kundi lake la watu wasiojulikana.
 
Nataka ninukuliwe vizuri kabisa ...legacy ya JPM ni ngumu kuivaa! Huko mbele atakumbukwa kuliko hata alivyozikwa! Tena wasiompenda sasa ndio wataoanza kukiri na kutubu! Naomba mtunze hii comment.
Maisha yako, lako tumkumbuke kama Hitler anavyokumbukwa na wajerumani, ama Kaburu Pieter Botha wa Afrika kusini. Maana mpaka sasa legacy yetu kwake ni udhalimu.
 
Shetani ameshindwa hakika.
Endeleeni kujifariji wajane.
 
Mwache Samia akae na magufuli is gone forever accept it, maana maandiko yako ni ya kumuombea ashindwe, keep guessing mama Samia na Magufuli ni vitu viwili tofauti

Bora umeliona hilo kwa mleta mada, huyu mleta mada aliamua kumtetea Magufuli, na akaingia kwenye ushindani wa kisiasa humu mitandaoni, saa hii anajiweka kwenye mazingira kuwa SI Unit ya urais eti ni Magufuli. Kwa taarifa yake Magufuli alijikita kwenye miundombinu tu na sio kazi ya urais, anataka kila mtu aamini kuwa rais aliyejikita kwenye miundombinu ni rais bora.

Lakini ukimwambia aseme rais bora kati ya Mandela ambaye hakujenga miundombinu ya maana, na rais Pieter Botha aliyejenga miundombinu kibao huko Afrika Kusini, atakuja na majibu tofauti! Amwache huyo mama afanye kazi na sio kuleta habari za Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…