Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Nilishalipa 2,000tsh kisa nilikanyaga machenza... Walitandika barabara nzima,hakuna sehemu ya kuweka mguu,ikabidi niruke juu ya matunda..ikawa kosa. Wale jamaa wana umoja,acha tu kuanzia bodaboda wao....ikabidi ninunue machenza bila kupenda....hata sikubeba..nikalipa,nikaendelea...
Waondoke,wapelekwe sehemu husika....iwe endelevu. Paul Makonda angeweza hiyo kazi,ila huyu RC kunenge...sijui
 
Waache bana usiwastue bana, wanadai wao wanaweza kupambana na majirani kwenye professionalism! Wabongo hawa hawa ambao wanaenda lunch saa 7 na kurudi ofisini saa 9 huku wengine wakibebishana na kusinidikizana kwa story.
 
Hao wanaotolewa maeneo hayo wanatarajiwa kuhamishiwa wapi?. Mtihani mpya kwa wale waliochukua mikopo haswa kina mama wanaotegemea vikoba na pesa za aina hiyo.
Haya ni mawazo ya kijinga kuanza kufikiria kwamba watahamia wapi...Huwa hakuna bargaining na mtu anayevunja sheria...

Hao watu waliojenga mabanda, ukitazama wengi wamejenga juu ya hifadhi ya barabara ambapo ingelikuwa umejenga nyumba ingebomolewa haraka mno

Kuna maeneo mtu anayetoka pembeni kuingia barabara kuu anapata shida kuona magari kwa sababu mabanda yamezuia kabisa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini yalipeleka ugali kwenye nyumba za masikini wengi sana nchini
Yah ngoja tuone tofauti sasa ya kukumbatia matajiri 600 au maskini 6,000,000 effect yake kiuchumi na kimaisha kwa ujumla 😂😂😂 mimi sitii neno maana katika uwiano tu wale 600 waliweza kuishi hata baada ya hawa 6,000,000 kupewa support! Ila je hawa 6,000,000 watatoboa kweli! Ndio kwanza kumekucha back to square 1
 
Hayana ujinga wowote hayo mawazo! Ubinafsi kama huu ndio haufai sababu hao walioweka vibanda wakija kuiba taa za gari nyumbani kwako hutalifurahia mzee!

Lazma tuwe na nidhamu ya kuangalia hali za wenzetu hata kama yetu yanaenda
 

Kufuata sheria ni kuwachukia maskini. Umaskini wako ni wako na sio kigezo cha kuvunja sheria. Kimara watu hawakuvunjiwa nyumba ili nyie mjenge mabanda. Sheria ifuatwe hakuna kulia lua hapa.
 
Kufuata sheria ni kuwachukia maskini. Umaskini wako ni wako na sio kigezo cha kuvunja sheria. Kimara watu hawakuvunjiwa nyumba ili nyie mjenge mabanda. Sheria ifuatwe hakuna kulia lua hapa.
Barabara si zipo tunaziona kule Kimara
 
Ingawa walikua wanapata riziki na familia zao ila naunga mkono waondolewe ilikua ni hatari sana kwa sisi waenda kwa miguu na watumiaji wa vyombo vya moto
 
Zamu ya wanyonge kuishi kishetani
Mwalimu alianzisha Gezaulole, Kibugumo, Tegeta n.k. Watu waliona kama wanaonewa wakati huo, lakini waliokubali kwenda huko leo je? Walijipatia maeneo burebure leo wanayauza kwa bei mbaya!! Serikali ianzishe Gezaulole mpya machinga wapelekwe huko. Maisha ya mjini hawayawezi!
 
Masoko yapo kila wilaya na tarafa huwa hawataki kwenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…