Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Wasiwasi wangu ni baadae hata hizo meza kusema waondoe
 
Wasiwasi wangu ni baadae hata hizo meza kusema waondoe
Huyo mkuu kajichanga kutoa maamuzi, hakuna sheria inayoruhusu kuweka meza ya biashara kando ya barabara, hivyo alipaswa kusema vibanda, meza ni marufuku.

Hawa wenye mamlaka sijui wanakwama wapi?
 
Huyo mkuu kajichanga kutoa maamuzi, hakuna sheria inayoruhusu kuweka meza ya biashara kando ya barabara, hivyo alipaswa kusema vibanda, meza ni marufuku.

Hawa wenye mamlaka sijui wanakwama wapi?
No, Sheria ni sawa hakuna ata kuweka izo meza lakini kuna ile kwamba Serikali inawasaidia hawa wafanyabiashara wadogo wadogo ili maisha yaende, kule Zanzibar Dr Shein aliondoa vibanda vyote maeneo ya darajani ambapo ndio eneo mashuhuri la biashara Zanzibar lakini Mwinyi kasema HAPANA watu wamerudi kiasili biashara kirindanda, jambo hili linatoa motisha kwa kiongozi aliye madarakani angalau kupunguza chuki kwa wananchi
 
Kwa hiyo sheria inarusu wananchi hasa wanyonge wazibe njia za waendao kwa miguu, waweke biashara popote watakapo?

Walianza kama mzaha tu pale kariakoo ('soko la kimataifa' [emoji23]) leo hii hapapitiki kuna meza zisizo hamishika yaani panakeraa sana.

Mimi naamini wanao haribu majiji yetu (hasa Dar) ni viongozi wenye dhamana
 
Ukiona hivyo serikali yenyewe imeshindwa kutoa ajira sasa wananchi lazima watafute namna na wakijaribu kulazimisha ndio yale madhara ambayo ni mabaya zaidi yatatokea wizi, watu kufa njaa, umasikini uliokithiri na kama hayo

Wewe unakereka kupita njia lakini wenzako wanateseka kimaisha mtu ata mlo 1 kwa siku inabidi akazungushe zungushe hapo kariakoo akale na watoto., jambo hili kwa nchi masikini huwezi kuliepuka. Na shida kubwa kwamba 'Aliyeshiba hamjuwi mwenye njaa'

Nchi zilizoendelea huwezi kukuta hizo interference kwenye miji kama huko kwenu sababu tayari ambaye hana kiajira kwenye kampuni au government basi angalau anapata bonus mwisho wa mwezi kutoka Serikalini, kuna njia nyingi za kutafuta kipato
 
Kama serikali imeshindwa kurekebisha hilo tatizo la wanyonge kushindia mlo mmoja ama kukosa kabisa basi haina budi kuachia ngazi
 
I hail the decision. They are a high environmental pollutant.
 
Rahisi. Watengewe maeneo "special" na siyo hovyohovyo ilivyo kwa sasa.
Tatizo lipo kwetu wanunuzi. Wakitengewa eneo hatuendi kununua huko tunabaki kununua barabarani, ndio maana wanaacha maeneo waliyotengewa wanarudi barabarani. Imeshatokea machinga complex na sehemu nyingine nyingi tu
Tuache kununua barabarani tuone kama watabaki.
 
Hii ni kero kubwa kiasi wanunuzi na wapita njia hatuna pa kupita, bidhaa zimepangwa hadi barabarani, hatari ya kiusalami ni kubwa inaongeza usumbufu jiji limekuwa kama dampo la vibanda
 
Hii ni kero kubwa kiasi wanunuzi na wapita njia hatuna pa kupita, bidhaa zimepangwa hadi barabarani, hatari ya kiusalami ni kubwa inaongeza usumbufu jiji limekuwa kama dampo la vibanda
Jiji limekewa kama kambi ya wakinbizi
 
Hao wanaotolewa maeneo hayo wanatarajiwa kuhamishiwa wapi?. Mtihani mpya kwa wale waliochukua mikopo haswa kina mama wanaotegemea vikoba na pesa za aina hiyo.
Soma vizuri wameambiwa watumie meza zinazohamishika kwa wepesi badala ya kuweka vibanda kabisa.
 
Na huku Mbezi mwisho pia tunahusika au ni katikati ya mji tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…