Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Wenye vibanda barabarani wakikaa hapo kwa miaka kama kumi watajiona kama wana umiliki wa hayo maeneo watajenga mpaka frem za zege kabisa na kupangishiana

watu watakuwa wanachukua kodi kabisa tukitaka kupanua barabara tutaambiwa ni bora angekuwa Magufuli na blah blah nyingi watahitaji fidia jambo ambalo haliwezekani ukibomoa ni kizungumkuti, kuwaambia wahame pekee yao hawawezi kuhama
 
Mwendazake akutengeneza solution ya kudumu kuhusu machinga yaani kuwapitia maeneo sahihi bali aliwatengeneza awatumie kisiasa.
Siyo mwendazake hata waliyomtangulia pia
Na mpaka sasa hawajajua wafanye nini kuhusu wamachinga

Ova
 
Wenye vibanda barabarani wakikaa hapo kwa miaka kama kumi watajiona kama wana umiliki wa hayo maeneo watajenga mpaka frem za zege kabisa na kupangishiana

watu watakuwa wanachukua kodi kabisa tukitaka kupanua barabara tutaambiwa ni bora angekuwa Magufuli na blah blah nyingi watahitaji fidia jambo ambalo haliwezekani ukibomoa ni kizungumkuti, kuwaambia wahame pekee yao hawawezi kuhama
Kodi za barabarani wanazochukua ni ofisi ya mtendaji kata ,sasa sijui kama hela wanayochukua ni official au pesa ya juu kwa juu

Ova
 
Warudi machinga complex pale wafanye biashara hata juu ya palaa la machinga complex

Kabisa wametengewa maeneo mengi sana ya kufanya biashara lakini hawataki kwenda,wamachinga ni kero sana,tatizo wanajiona wana haki wanaweka biashara zao kati kati ya barabara....Waondolewe wote.
 
Wanafanya kusiwe na umuhimu wa kuweka maeneo ya soko, stand wala mall, mahakama, kanisa, na maduka maana vitu vinamagwa tu kila sehemu mbele ya majengo na mabarabarani hakuna haja ya kuwajibika tena hela ya pango ni mwendo wa kumwaga tu vitu vyako nje unaanza kuuza, na viongozi wanaona tu watu wazima waliojigeuza kujitoa fahamu baada ya kukimbia vijijini.

Imagine hata hao wageni wanaokuja kutembelea Kama watalii wakute watu wamekusanyika barabarani bila huduma kama vyoo na mabafu wakati huo huo viwanda tunalazimisha viwe na vyoo na mabafu na watunze mazingira hata watu wa mazingira wamekuwa legelege kwa hili wangepeleka propasal kwa Raisi hata yeye angewasapoti.
 
Lowassa alijisemea tu,nitakuwa rafiki wa maxhinga,mama ntilie na boda boda,basi Mwendazake akingianmzimamzima,wakati ukawa walifanikiwa kyisafisha kariakoo
 
Sio vibanda tu, wawaondoe hata wanaopanga bidhaa chini. Lazima kuwe na sehemu maalum ya kuuza vitu sio kila mahali.

Na sisi pia tunawaendekeza. Unaanzaje kusimama barabarani kununua na kujaribu viatu au shati? Tusingenunua wasingekaa barabarani. Tubadilike pia maana kama kuna mnunuzi muuzaji lazima atajitokeza
 
Good idea. Hata mtu binafsi anaweza akafanya hivyo akapata kodi ya maana tu
 
Jana nilikuwa mbagara Zankem ile ni roho ya kishetani kabisa hamna pa kupita inalazimika upite barabarani uangalie bodaboda +gari kweli kiubidamu si sahihi.
 
Hao wanaotolewa maeneo hayo wanatarajiwa kuhamishiwa wapi?. Mtihani mpya kwa wale waliochukua mikopo haswa kina mama wanaotegemea vikoba na pesa za aina hiyo.
Umetoka lini bleed? Soma tangazo vizuri, halafu uache kulia kulia kwa kutanguliza jinsia yako ya mwanamke eti haswa kina mama wanaotegemea vikoba wakati ninyi ndo Rais wa nchi.
 
Mkuu kweli Mbezi Luis imezidi mno kwa uchafuzi wa mazingira nadhani hali hii imechangiwa na uwepo wa Magufuli Bus Stand. Ile Stand ya daladala kuanzia saa 12 jioni inageuka na kuwa soko, nawahurumia sana wahudumu wa ufasi.
Kwa upande wa uongozi ndipo lilipo tatizo, hao wachuuzi hapo stand wanajiamulia watakavyo kwa kuigeuza stand kuwa soko, but sheria hairuhusu kitu kama hicho, swali la kujiuliza ni hili "viongozi husika hawajui wajibu wao?

Jiji linatia aibu sana, na hiyo stand ya Magufuri imeshachafuliwa na chinga
 
Gari la tangazo linapita kutangaza ya kuwa ifikapo tarehe 18 mwezi huu hakitakiwi kibanda chochote kuonekana kando kando ya barabara katika jiji la Dar es Salaam...
Naunga mkono hoja. I think as a nation we can do better than this.
 
kila nabii na kitabu chake.... Ila nabii huyu anafuta vitabu vya wenzake kwa sipidi ya mwanga.....
 
Mamlaka na hili la malori pia muliangalie
Yaani malori kariakoo ni shida kuliko hata hao wamachinga
Kila nyumba ni ofisi ya usafirishaji
Yaani kariakoo imekuwa kama haina mwenyewe aisee ni shida sana
 
Back
Top Bottom