Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

This was a mistake to allow them to do business everywhere. Hawa watu wapangiwe maeneo ya kufanya biashara na waende huko. Hizi mambo za kuweka biashara kwenye barabara ni uchafu mtupu. Halafu watalipaje kodi sasa?
Yapo na hawataki eti hakuna wateja, Si kweli. watu watazifuata ziliko kama sasa mtu anatoka Tegeta kwenda Karume kufuata mitumba au sokoni Ilala. Watu wanakwenda kufuata nguo na bidhaa za sokoni huko tandika kutoka kimara.
 
Umenikumbusha kijana aliyeuawa na wamachinga kkoo baada ya gari lake kukanyaga fungu la nyanya barabarani, Iliniuma sana walivyochangia kumpiga. Sad.
Yaani mwendazake alitengeneza time bomb kubwa. Masikini Kijana wa watu!!!!
 
Huwa nawakubali MAMA na DADA zetu kwa Usafi aisee hii ndio nature yao na nililitegemea hili. ila ANGALIZO isije kuwa mambo ya "Tengeneza tatizo halafu Tatua tatizo "
Hakuna mkuu. Mambo yatakuwa safi tu.
 
Hao wanaotolewa maeneo hayo wanatarajiwa kuhamishiwa wapi?. Mtihani mpya kwa wale waliochukua mikopo haswa kina mama wanaotegemea vikoba na pesa za aina hiyo.
Zamani walikuwa wanapika vyakula majumbani mwao, then wanabeba wanaleta kwa wateja wao maofsini.

Sasa hivi IFM na pale Karimjee kuna vibanda vya MamaNtilie utadhani uko Buguruni au Vingunguti!!
 
Watakuja kusema"baba yetu kaondoka sasa wanatunyanyasa"
Mwendazake alikuwa anatafuta kura za huruma na HAKUWA na akili ya kuwatafutia pa kuwaweka.

Halafu wote hawa machinga ni matokeo ya sera mbaya za Mwendazake dhidi ya Matajiri wakubwa. Na kutoajiri vijana wanatoka vyuoni

Jiulize baada ya kumpiga vita Yusuf Manji je wale wafanyakazi 3,000 kwenye makampuni yake waliokuwa wanapata mshahara moja kwa moja walikwenda wapi?

Ndiyo hawa wamejaa mitaani wanafanya umachinga, maana ajira hakuna.

Mwendazake alikuwa LAANA kubwa, nafuu kaenda Jehanam kabla hatujaharibikiwa
 
Uchumi wa nchi hauwezi kujengwa na machinga hawa jamaa walikuwa wanazuia baadhi ya njia magari na watembea kwa miguu tusipite na kusababisha msongamano

Kuna faida kubwa machinga kuondoka mjini kwanza kwa wanaoshusha mizigo kwenye maduka yao itakuwa ni rahisi
Pili kodi za maegesho ya magari zitaongezega
 
Hivi hoja za ajabu kama hizi mnazitoa wapi? Nchi ifike mahali raia wafuate sheria , Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma, iweje sasa raia wengine Sheria iwe butu kwao kisa machinga? Raia kama hana shughuli ya Msingi ya Uzalishaji mjini kati anafanya nini? Warudi kwenye kilimo nchi ipate uchumi kukua, hii ya kufanya uchuuzi Nchi haifaidiki chochote kwa hawa raia wachuuuzi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Sawa mkuu nimekuelewa kiwa huhitaji kuona machinga wakizurula zurula, waende kuwa wakulima kijijini.
 
Serikali msifanye pupa ktk suala hili. Mlifanya makosa kuwaweka wafanyabiashara humo barabarani kinyume na kanuni za town planning.

Sasa ni vigumu kuwaondoa kwa AMRI tu. Hili ni zimwi lillilopaswa kufungiwa kwenye chupa na kutupwa baharini. Badala yake mmelilea ili mlitumie kisiasa.

Lakini JPM akaenda mbali zaidi, akalitoa ndani ya chupa na kuliweka 'SEBULENI' kwenu!
Mtajifunza kwa machungu, kwamba sio rahisi 'kulirudisha jini kwenye chupa'.

WAZO:
Badilisheni sera ya ELIMU ili iwe ya kiwango cha kimataifa. Ndipo vijana wataajiriwa na wawekezaji wakubwa wa ndani na wa nje. Elimu ya sasa ktk shule za serikali hata vyuoni haiwaandai wahitimu kushindana na wageni kwenye soko la ajira za kimataifa ndani na nje ya nchi.

Hili nalo litakuwa gumu kwasababu wakubwa (wanasiasa hasa WATAWALA) wengi, bungeni na serikalini ni zao la sera ya ELIMU ya sasa, kuikosoa ni kama kujikana wenyewe au mfumo uliowafikisha walipo.

Pili huwa mnawatumia hawa vijana kisiasa wakati wa uchaguzi kupitia CHAMA. Hamtaki kukiri kwamba chanzo cha tatizo la sera ya elimu yetu ni dhana nzima ya 'KUJIAJIRI' kwamba ni lazima itanguliwe na ELIMU Bora kwa wote, sio kwa wenye uwezo tu.
Ili kijana ajiajiri lazima awe na:
1. Elimu bora na/au Ujuzi katika fani husika.
2. MTAJI
Upatikanaji wa mitaji usifanywe kisiasa hata kama kupitia vikundi bila kuzingatia tija.
Unatoaje mkopo kwmfn kwa kikundi au mtu anaeweka biashara barabarani?
Hicho kikundi kama ni cha vijana au kinamama, ili kipate mkopo au kitambulisho lazima kiwe na eneo lililopangwa kufanya biashara husika.
 
Mkuu Kerubi naungana nawe kwa hoja zako, ila tambua kuwa humu Jf wengi ni athirika wa hawa wamachinga huko barabarani, mbele ya maduka yao n.k, hivyo ni vyema proposal zako ukazipeleka kwenye ofisi inayohusika kwa hatua zaidi. Hakuna mtanzania anayependa mtanzania mwezake anyanyasike ama anyanyaswe lakini kwenye mambo yenye mashaka mashaka lazima sheria zifutwe.
 
CCM oyee,subirini ukikaribia uchaguzi tutawarudisha tena pembezoni mwa balabala mufanyage biashala kama kawa.
 
Jiwe aliruhusu machinga watembeze biashara zao hata ikulu alafu akaifunga njia kule magogoni machinga wakatembeza biashara wakachoka wakaanza ujenzi kwa kasi sana service road zote kudadeki
 
Back
Top Bottom