Inahitaji jicho la tatu kuliona hili.
Kwanini nchi imejaa wamachinga wengi kuliko wanaofanya biashara rasmi madukani?!
Ukiishajibu hilo,twende kwenye conclusion,je Tanzania ni nchi yenye wamachinga zaidi au wafanyabiashara rasmi zaidi?
Je,tunataka nchi ya wamachinga au wafanyabiashara rasmi?
Tuna mikakati gani kutomuua au kutompoteza mmachinga na badala yake kumgeuza kuwa mfanyabiashara rasmi?!
Kiwango cha elimu,maarifa,mipango ya maendeleo ya jamii na uchumi katika taifa hili na utekelezaji wake kinatengeneza workforce ya aina gani,skilled au unskilled?!
Aina hiyo ya workforce ina mchango gani kutengeneza machinga au mfanyabiashara rasmi?!
Tuna workforce ya aina gani sasa(majority),tunataka workforce ya aina gani baadae na tunaipataje bila kuathiri uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja?!(smooth transition)?
Haya ni mambo ya kuzingatia.
Tusiingize migambo mitaani na kujifanya sisi ni wamarekani tuliosheheni mabilionea watakaoweza kuinvest,tukavunjavunja ALL THAT WE HAVE tukijivunia kuleta kitu ambacho ni priviledge kwa mhindi,mnaijeria,mkenya,mzungu etc na wale unawaona kero kumbe ndio workforce yako pekee uliyo nayo ambayo unapaswa kuilea kama yai.
Tukifukuza machinga,je,hawa machinga kuna siku tutawakuta wanamiliki maduka wao,au watanzania wenzao?!au tutakutana na wageni wakimiliki njia za uchumi za nchi?!
Suala la machinga ni pana na kiashiria cha tatizo kubwa la nchi kuliko tunavyowaza short sighted.
Tuweke siasa za magufuli-Samia,ccm-chadema kando,tusiwe blinded na ego.
Tuwaze kama watanzania,ni kama mzazi mwenye mtoto mtukutu nyumbani,jambo la kwanza unawaza kumbadili awe mwema,na sio kumtimua.
Tusizungumze kama tunaongelea aliens from another country,planet etc.
Tunazungumzia vijana wa kitanzania,wanaotumia nafasi finyu ya uwekezaji kujikwamua kiuchumi.
Tunazungumzia baba na mama wa wale watoto unaokutana nao kituoni wamevaa uniforms wanakwenda shule!
Angalia upande wa pili wa shilingi.Huko ndiko nchi iliko,ndiko vijana wenu wengi waliko,ni machinga barabarani,machinga maofisini.
Ubinafsi usikufanye uwe blind.
Nina biashara zangu rasmi nalipa kodi nyingi za serikali hapa mjini,na sijawahi kumchukia machinga asiye na duka kama mimi hata siku moja.It pains me kuona mnazungumzia mambo ya kutimua binadamu anayejitafutia riziki kirahisi tu!Yaani mnaona rahisi tu mambo haya ya uwekezaji na uchumi mtu kahangaika wee hadi kaweka banda lake,timua hao!You guys?!😡😡
I expect mtandao kama huu uwe na mawazo critical zaidi,yasiyopatikana kirahisi.
Wajengeeni maeneo yao,warasimisheni kazi zao,wapeni financial support,waelimisheni watanzania waweze kuwa competitive na mataifa mengine then watahama tu bila vurugu kuja mnakokutaka.
Wekeni na simamieni mipango miji kila mtu anayetaka kufanya lolote ajue anafanyia wapi na vipi,na taratibu zikoje,na ziwe condusive kwake,sio alimradi tu.