Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Ipo Machinga Complex, Ilala.
Ilijengwa na Kikwete, hadi leo haijajaa.
Unawaelewa Machinga wewe?
Tatizo ni miundo mbinu ya pale! Aliekwambia machinga wanatakiwa wajengewe ghorofa nani?

Nani anataka tabu ya kupanda floor ya 5 kununua nguo ya mtumba wakati karume anapata nguo chini tu! Ina maana watakaofaidika zaidi pale complex ni walioko floor za chini zile na floor ya kwanza labda! Kuanzia floor ya pili na kuendelea ni kupiga mihayo tu huuzi!

Soko lijengwe la chini ili kila mtu awe na access na wateja! Kama ilivyo Boma au Pale Mawasiliano hapo watu watakaa! Sio kujenga ligorofa watanzania hatuna utamaduni wa kununulia bidhaa magorofani!

Kariakoo pale magorofa yamejaa ila wanaouza ni ground floor na floor ya kwanza sababu watu ndio watu wana access napo zaidi! Wanaouza floor ya pili wachache sana!
 
Masoko yapo kila wilaya na tarafa huwa hawataki kwenda
Tatizo masoko ya maghorofa hayana usawa! Imagine soko la magomeni pale usalama liko kama hospitali ya Mloganzila! Hivi mie nipande floor ya 5 nikanunue nyanya na bamia wakati kuna mtu anauza chini pale ground floor!

Ni nani mjinga atakubali akakae floor ya tano? Ndio maana watu hawataki kuingia mle complex na kwengineko! Soko liwe kama la kariakoo floor mbili pana ili kila mtu auze sasa soko kama hospitali mtaendelea kulaumu wamachinga tu!
 
Hayana ujinga wowote hayo mawazo! Ubinafsi kama huu ndio haufai sababu hao walioweka vibanda wakija kuiba taa za gari nyumbani kwako hutalifurahia mzee!

Lazma tuwe na nidhamu ya kuangalia hali za wenzetu hata kama yetu yanaenda
Mkuu ushawahi kufika maeneo kama Mbezi Mwisho ile barabara inayotoboa kwenda Airport/Kinyerezi...?

Kuna kipande fulani saia wameweka mabanda hadi juu ya lami, wameacha nafasi ya magari kupita tu...

Sasa hili wewe waona ni jambo sahihi?

Kwani wangelijenga pembeni zaidi huko kama miaka yote wala hakuna ambaye angeliona ni kero...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni kiki. Mwisho wa siku mama atasema, "waacheni mpaka mmewajengea maeneo sahihi nao wanatafuta riski". Atashangiliwa.
 
Barabara si zipo tunaziona kule Kimara
Kuna mama mmoja pale Mbezi Mwisho alivunjiwa ghorofa lake la biashara kwa sababu tu kuwa kajenga ndani ya hifadhi ya barabara...

Lakini ukipita leo hii, hilo eneo lillipovunjwa ghorofa ya thamani nyingi tu, kumejaa utitiri wa vibanda na serikali ya mtaa inakula kodi, plus halmashauri ya jiji inakula kodi ya parking...

Sasa ni sheria gani hiyo inayomuumiza mmoja na kumuacha mwingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ushawahi kufika maeneo kama Mbezi Mwisho ile barabara inayotoboa kwenda Airport/Kinyerezi...?

Kuna kipande fulani saia wameweka mabanda hadi juu ya lami, wameacha nafasi ya magari kupita tu...

Sasa hili wewe waona ni jambo sahihi?

Kwani wangelijenga pembeni zaidi huko kama miaka yote wala hakuna ambaye angeliona ni kero...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo ni sawa mkuu ni makosa ila hawa watu wanajipatia rizki je tukiwatimua tuwape na suggestions kwamba waelekee mahala fulani sio kutoa matangazo tu
 
Kuna mama mmoja pale Mbezi Mwisho alivunjiwa ghorofa lake la biashara kwa sababu tu kuwa kajenga ndani ya hifadhi ya barabara...

Lakini ukipita leo hii, hilo eneo lillipovunjwa ghorofa ya thamani nyingi tu, kumejaa utitiri wa vibanda na serikali ya mtaa inakula kodi, plus halmashauri ya jiji inakula kodi ya parking...

Sasa ni sheria gani hiyo inayomuumiza mmoja na kumuacha mwingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua maybe vibanda ni temporary structures na wamevunja ili barabara ipitie na imeshachongwa bila shaka!
 
Hadi baadhi ya barabara zinakua nyembamba, haziwezi kupishana gari 3 kisa vibanda, naunga mkono watafutiwe maeneo maalumu....mji umekua mchafu sana.
Bora umesema watafutiwe eneo maalum ingawa kwa kariakoo pale ulaji ni mkubwa sana
 
Hilo ni sawa mkuu ni makosa ila hawa watu wanajipatia rizki je tukiwatimua tuwape na suggestions kwamba waelekee mahala fulani sio kutoa matangazo tu
Siku zote sheria inamtaka anayetaka kujenga mahali iwe ni banda au nyumba, ai-consult serikali kujua kama hapo mahali pamepangwa kujenga anachotaka kujenga au lah, na si otherwise...

Na ndio maana serikali yenyewe huwa ikikuta upo mahali si sahihi, inakubomolea tu kwa sababu hukuitumia haki yako kwenda kuuliza kabla ya ujenzi...

Leo hii tunalia kwamba nchi yetu haina maendeleo, lakini tunasahau kwamba chimbuko la maendeleo huanza na 'Ustaarabu'...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchumi wa nchi hauwezi inuliwa na machinga bali kwa uzalishaji.
Machinga na bodaboda ni madalali wa viwanda vya china kukuza uchumi wa China
Hao wenye maduka pia wao ni madalali wa uchumi wa wapi mzee maana 80% ni asian countries products
 
Hizi akili za kibavicha hatari, sasa hujui ukimbimolea kesho atakuvamie akuibie hata kandambili nyumbani kwako
Wataendelea kung’oa taa za magari usiku na side mirrors!
 
Naomba sana hili lifanyike kwenye majiji yote

Yaani jiji la kitalii Arusha ukipita barabara ya kuelekea stand kuu unakutana mpaka na vitanda, magodoro, makabati yaliyofubaa n.k

Vibanda viondolewe vyote
 
Sisi tumelipia na kitambulisho cha machinga sasa mtuguse tunuke🐒
Afande Mourautau hawa huku.. Wawahi wanataka kipigo cha mbwa mwizi eti. Njoo uwashughulikie au hawakujui nini!!!
 
Tayari wameshatafutiwa au watoke kwanza,
MAANA kilio chao toka zamani ni kuwa maranyinhi huwa wanapelekwa au kutengewa maeneo yasiyo na tija kwa biashara zao
Duh sijui itakuwaje
Hivi hoja za ajabu kama hizi mnazitoa wapi? Nchi ifike mahali raia wafuate sheria , Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma, iweje sasa raia wengine Sheria iwe butu kwao kisa machinga? Raia kama hana shughuli ya Msingi ya Uzalishaji mjini kati anafanya nini? Warudi kwenye kilimo nchi ipate uchumi kukua, hii ya kufanya uchuuzi Nchi haifaidiki chochote kwa hawa raia wachuuuzi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom