Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Sasa kuna miamba wanapiga kila siku , nchi hii [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],mno yanayofanyika humo viwandani yanatisha sana ,nimewahi fanya kazi kiwandani kama fundi mitambo so ninaelewa balaa wanapokutana nalo manual labourers , ni hatari zaidi ya hatari
Huko viwandani wafanyakazi wasio manual laborers mfano mafundi mitambo maslahi yao pia ni madogo ??
 
Vijana mpo siriasi kweli yaani unafanya Kazi masaa 12 then unalipwa sijui elf 6.
Huu mda vipi ukiutumia kufanya shughuli zako binafsi.
Mfano
1.Kuuza matunda
2.Kutembeza umachinga
3.Kuuza vitafunio
4.Kuuza mboga mboga
5.Kusomba maji
6.Kukusanya taka
 
Kuna jamaa yangu aliona makaratasi ya ajira viwandani wamebandika katika nguzo za umeme mshahara kwa wiki ni laki 275,000/= .jamaa akajitosa akawahi asubuhi saa 12 yupo getini kufika mida ya saa 5 asubuhi namuona jamaa huyu hapa gheto namuuliza mbona umewahi kurudi mapema yote hii kulikoni?
Jamaa akaniambia brother acha tu uliona wapi watu wawili mmekabidhiwa Lori scania 10 zimejaa mzigo wa gypsum board muushushe mzigo wote kwa siku moja?[emoji2]
Jamaa alipiga kazi mpaka saa 5 asubuhi alivyoona hakuna dalili ya mzigo kuisha akaamua kutoroka.
Daaaah hahahahahahaha
 
Tatizo ni usomi hafifu. Hili suala la ajira lilifanuliwa vizuri na Carl Max na Angels. Wakasema faida ya tajiri ni kile kiasi anachomyonya mfanyakazi.
Mengine nendeeni.
Ilishanzungumzwa miaka 300 zamani
Kuna mwalimu wetu mmoja wa literature alikuwa anatuambia principle ya kuajili ili uendelee ni hii

1..Make them work hard ( wafanye kazi kwa nguvu)
2.. Pay them little ( Walipe kidogo/ujira mdogo)
3.. If they complain say nothing ( Kama watalalamika usijibu chochote/ kaa kimya)
 
Mnapakia lori 8 kwa siku ndoo za mafuta ya kula. Roli moja linabeba ndoo elf 8.
Mnapakia viroba vya unga roli 10 kwa siku then unalipwa elf 5.
Masaa 10 ya kazi.
Pesa inaishia kula na nauli daah.
Aisee si bora niokote chupa na nailoni mtaani nikapime.
Ishu ni suala la mind na sio limitations ya fursa
 
Hao mamlaka si ndio wakiingia viwandani si ndio utoka na bahasha plus ndoo za mafuta, sabuni,viroba vya Mchele na sukari atakukumbuka wewe kweli
Unakuta watu wa mamlaka hawajui gharama za mafuta ya kula, sabuni wala unga wao hupelekewa tu home. Ili wauchune tu. Hio ndio tabia halisi ya mtanzania akipata cheo, ubinafsi kwanza.
 
Tza tunanyonyana Sana aisee. Check wadada wa Kazi uanza Kazi saa 11 alfajiri kulala saa nne au sita usiku. Mshahara elf 50.
Achilia stress za maboss zao wao ndio wahanga wa hasira walizotoka nazo kazini.
Halafu serikali inawazuia wadada wasiende Kazi uarabuni eti wanateswa kwann huku nyumbani wanapata raha. Alivyo mwarabu ndivyo alivyo mwafrika.
 
Back
Top Bottom