Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Nimebahatika kutembelea viwanda na stoo kadhaa hapa dar kutokana na shughuli zangu za cctv camera ,networking, biometrics na computer issues , nikili wazi watu wanastruggle kwa ujila mdogo sana mtu analipwa 3000 unajiuliza anaibudget vipi asee hawa matajiri wa kihindi hawafai wanendelea kutengeneza taifa lenye maskini wengi na wakutupwa asee.
 
Emu elezea hii kidogo mkuu kuna kijana yupo pale daah anarudi amechoka balaa,
Ni mwendo wa kurusha creti za soda na kuzidaka usiku kucha na day shift Sana mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku , shift za masaa kumi na mbili ,unaziweza ? ,Uliza malipo sasa ,utalia.
Unakuta bonge la lorry semi trela mbili limejaa creti za chupa za soda au bia zinapakuliwa na watu wawili ,mama£ kama mtoto wa mama lazima unye
 
Kazi za viwandani hasa Tanzania ni hatari sana kwa afya na uhai wako ,do it for your own risk , safety zero ,vitendea kazi hamna ,mazingira mabovu na hatarishi kwa afya na uhai , ujira mdogo sana na usiofaa kabisa + manyanyaso na overwork .
Compliance ya OSHA (Occupation safety and health ) ni always zero ,hivyo ndio viwanda uchwara vya bongo.
Kuna mdau kaongelea kiwanda cha NONDO Nyakato steel-Mwanza , kile ni mfano mmoja wapo , mwaka jana hapo Nyakato steel bomu lilipuka humo ndani ,yote hiyo ni uzembe wa compliance ya masuala ya safety ,wao wanafanya biashara ya kuteyusha chuma chakavu yet hamna mifumo thabiti ya kuchunguza na kusort vyuma vinavyoletwa ili kuyeyushwa ,matokeo yake wanaokoteza kila aina ya chuma na kuvipeleka kwenye vinu /furnaces kuyeyushwa ,upuuz mtupu .
Hivi viwanda vingi bongo vinaoperate kama criminal cartels za mamafia ,Kwanza wengi wanaoendesha hivyo viwanda ni matapeli tu ,wanatapeli hata hivyo viposho vya elfu mbili mbili wanavyowalipa hao vibarua utakuta kuna muda hawawalipi ,mambo ya ovyo kabisa
Ni sahihi kabisa yaani pale nyakato ni kama jehanamu.[emoji706]
 
Kuna jamaa yangu aliona makaratasi ya ajira viwandani wamebandika katika nguzo za umeme mshahara kwa wiki ni laki 275,000/= .jamaa akajitosa akawahi asubuhi saa 12 yupo getini kufika mida ya saa 5 asubuhi namuona jamaa huyu hapa gheto namuuliza mbona umewahi kurudi mapema yote hii kulikoni?
Jamaa akaniambia brother acha tu uliona wapi watu wawili mmekabidhiwa Lori scania 10 zimejaa mzigo wa gypsum board muushushe mzigo wote kwa siku moja?[emoji2]
Jamaa alipiga kazi mpaka saa 5 asubuhi alivyoona hakuna dalili ya mzigo kuisha akaamua kutoroka.
[emoji1787][emoji1787]
Ni shida
 
Wanalipa elfu nne hadi tatu then Kazi ni kubeba viroba vya ngano kilo 50 na 25 Kuanzia asubuhi Hadi jioni na pia night shift hipo it about fucking job huyo Bakhressa Ni mpuuzi mmoja. Including Mo dewij and so called matajiri uchwara
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiyo 10k ipo ila sio kwa kazi kama hizo

Nadhani ukienda kwenye viwanda vya steel unaweza ukapata hadi 15k

Ila changamoto yake ni kwamba unaambiwa kila mfanyakazi unayemkuta pale ujue hiyo ni siku yake ya kwanza hapo kiwandani.

Ukishachukua malipo ya 15k ukitoka hapo utachagua mwenyewe ukapatiwe huduma kati ya Amana au Muhimbili

Au usizi home ujiuguze mwenyewe
Duuuuh maskiniiii, hatareeee sanaaa.
 
Tza tunanyonyana Sana aisee. Check wadada wa Kazi uanza Kazi saa 11 alfajiri kulala saa nne au sita usiku. Mshahara elf 50.
Achilia stress za maboss zao wao ndio wahanga wa hasira walizotoka nazo kazini.
Halafu serikali inawazuia wadada wasiende Kazi uarabuni eti wanateswa kwann huku nyumbani wanapata raha. Alivyo mwarabu ndivyo alivyo mwafrika.

Hao wasaidizi wa kazi za ndani ,hiyo elfu 50 inawatosha kabisa.

Kumbuka wanakula bure, wanalala bure,hawalipii umeme wala maji, wakiumwa maradhi ya kawaida matibabu wanagharamiwa na mabosi zao nk.
 
C
Pana mtoto wa kichaga asubui anawahi sokoni anajumuia karoti, hoho, vitunguu, njegere, nk
Mchana ana paki mixing package yaani anaweka karoti, hoho, nk anafunga kwenye vifuko kisha anatia kwenye begi anapita mtaa kwa mtaa kuanzia saa 10 jioni. Ndani ya masaa manne mzigo wote ushaisha kwa siku hakosi elf 60 faida.
Chai imezidi sukari.
 
Archana na bakhresa,huku pwani kuna kiwanda cha sabuni kinaitwa ked's kinazalishasabuni za doffi na kleesoft vibarua wanalipwa na wakala aliyeingia ubia na kampuni hii ....sasa utakuta wakala analipwa sh 12,000 kwa Kila kibarua Ila yeye analipa sh 8000 kwa Kila kibarua ...
Wanateswa Sana vijana...huyo wakala anaitwa EVAH MANPOWER SUPPLIES..kiongozi wao anaitwa kipara...
 
Archana na bakhresa,huku pwani kuna kiwanda cha sabuni kinaitwa ked's kinazalishasabuni za doffi na kleesoft vibarua wanalipwa na wakala aliyeingia ubia na kampuni hii ....sasa utakuta wakala analipwa sh 12,000 kwa Kila kibarua Ila yeye analipa sh 8000 kwa Kila kibarua ...
Wanateswa Sana vijana...huyo wakala anaitwa EVAH MANPOWER SUPPLIES..kiongozi wao anaitwa kipara...
Kipara si ndo alikua kipindi flani kama mkalimani wa wachina?
 
Archana na bakhresa,huku pwani kuna kiwanda cha sabuni kinaitwa ked's kinazalishasabuni za doffi na kleesoft vibarua wanalipwa na wakala aliyeingia ubia na kampuni hii ....sasa utakuta wakala analipwa sh 12,000 kwa Kila kibarua Ila yeye analipa sh 8000 kwa Kila kibarua ...
Wanateswa Sana vijana...huyo wakala anaitwa EVAH MANPOWER SUPPLIES..kiongozi wao anaitwa kipara...
Jamaa yangu mmoja aliambiwa atoe 50k apate kazi mpaka leo hajapata ameamua kusamehe. Kuna rushwa sana Keds na ukiritimba wa hali ya juu.
2017 nilihangaika sana kuomba kazi pale lakini wapi mpaka nikakata tamaa!
 
Back
Top Bottom