Vibendera vya Israel kwenye magari ya Wabongo

Darmian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
17,289
Reaction score
46,624
Wakuu heshima kwenu.

Naomba tu kuuliza japokuwa najua kufuatilia mambo ya watu sio mchongo wala nini.

Huwa naona vibendera vya taifa la Israel kwenye magari ya watu ambao naamini kabisa ni Wabongo wenzetu.

Sasa wakuu naomba tu kuuliza what is the motive behind this? kunakuwa na affiliation gani na hili Taifa la Israel?

Au ni Waisraeli weusi wanaoishi bongo?
 

Wengi huwa ni Wakristo, na huamini kupeperusha bendera ya Israel ni sawa na kuonesha wanakubaliana na Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo(Isreal)
 
Wengi wao ni religious fanatics hususani new born again Christians, wakati wa Israel wana upinga ukuristo.

Africa is a continent of confused fellows
 
Wengi wao ni religious fanatics hususana new born again Christians..........wakati wa Usrael wana pinga ukuristu!!!! Africa is a continent of confused fellows
Nimeshangaa sana kuona statistics zinasema ni asilimia mbili tu (2%) ya Waisrael ndo wakristu..

Nilidhani zaidi ya asilimia tisini watakuwa wakristo,kumbe nilikuwa opposite vibaya sana..

Wakristo tumeingizwa chaka nini na biblia?
 
Nimeshangaa sana kuona statistics zinasema ni asilimia mbili tu (2%) ya Waisrael ndo wakristu..

Nilidhani zaidi ya asilimia tisini watakuwa wakristo,kumbe nilikuwa opposite vibaya sana..

Wakristo tumeingizwa chaka nini na biblia?
Hao wa nabii wapya ndo wana potosha vijana wenye elimu duni na msongo wa mawanzo, eti nchi ya ahadi ni Israel wakati israel hiyo imeundwa 1948.
 
Nothing but mental slavery
 
Mambo ya imani mkuu,

Ni kama ww unavyotamani kwenda kuhiji mecca
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…