Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
nimeisoma hii kesi leo, aisee huyu maza kapoteza sana. alifunga ndoa ya kikristo wakati ndoa ya awali bado ipo hai, kwahiyo ndoa ya pili na likwelile ilikuwa batili na ilichukuliwa kuwa ni uhawara tu, hata presumption of marriage haiwezi kuchukuliwa kwasababu takwa mojawapo la presumption of marriage ni kwamba lazima pasiwepo ndoa inayoendelea nyengine (kwa wakristo), kwahiyo mali zoote zilizopo hata kama alichuma na likwelile, hatapata kitu, kwasababu yeye sio mrithi halali. sijui mnanielewa?hawa wanaccm ifike mahali wawe wanapeana semina wao wa wao huku namna ya kuishi na watu, wanatia aibu sana na kutia aibu chama chao. manake wengi hasa hao wanawake wanaonekana kama ni wadangaji tu na gold diggers. waacheni watoto washangilie ushindi wa nyumba za baba yao.
kwenu ninyi mnaorukia ndoa za watu. mrukie ndoa ya awali ikiwa imekufa kwa talaka, kama haijafa, ninyi ni mahawara tu na sio mahawara mnaodondokea kwenye presumption of marriage, kwasababu mojawapo ya sharti la presumption of marriage ili mpate mgao hata kama hamkufunga ndoa, hapatakiwi kuwa na ndoa iliyo hai. mfano wake ni pale vijana ambao wote hawajaoana wanakutana na kuishi kinyumba kwa miaka miwili au zaidi mfululizo, wakiamua kuachana, wanaweza kuwa presumed wanandoa ili kugawanya walichopata au matunzo ya watoto, ila kama mmoja wao alikuwa na ndoa inayoendelea kama likwelile, presumption of marriage haiwezi kumwokoa vicky.