Video aliyorusha Miss World kuhusu hali ya umaskini Tanzania; Mama Salma na wenza wa viongozi wa Tanzania bado wanaona ni sahihi kulipwa mabilioni?

Wageni wakija kwetu wanatushangaa na umaskini wetu, ajabu sisi na viongozi wetu hatuna habari miguu juu, na hata miss Tanzania wetu aliyetumwa huko naamini nae atakuwa anamshangaa huyo miss world kushobokea mambo yetu ya ndani.
 
Seriously unatetea ule ujinga wa yule Mama?

Sitashangaa miss world akirudi tena huku akienda kwao atakuhurumia nawe kwa huu ujinga wako..

Time will tell.
 
Mkuu umewalaani kabisa?
Dunia hivi sasa ni kama tu kijiji, "limit is only the sky", ni lazima Watanzania tujipime sisi wenyewe kupitia tawala, viongozi na wananchi wa nchi nyingine. Pamoja na uwepo wa haki, maadili, kinga, pamoja na majukumu ya mbunge na bunge. Lakini, Je! Maamuzi yao kwa kiasi gani yana tija kwa mwananchi wa kawaida!?

Suala la wenza wa viongozi kupewa mafao maalum lina ukakasi mwingi sana. Mathalani, Je! Vipi kuhusu wenza wa maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, ambao muda wote wa ajira zao huwakabiriwa na tishio la kudumu la uhai wao, kwa kuwa viapo vya kazi huwafanya wawe tayari kufa wakati wowote ule kwa ajili ya uzalendo kwa nchi yao!?
 
Umeongea point sana yani nchi imejaa unafiki sana mtu ukiongea ukweli unaonekana mpinzani ukweli kama huu viongozi wetu hawautaki tupo kinafiki sana unakuta mwalimu analalamika ajalipwa hela ya likizo mwalimu huyo huyo anachanga hela ya kumchangia kiongozi ya kugombea uraisi mwakani
 
Picha, tafadhali..!

Miss World 2024 WINNING akizungumza: Krystyna Pyszková kutoka Czech Republic kuhusu ndoto ya elimu inayopotea jinsi inavyoumiza kama mkuki moyoni

Mrembo aliyeguswa na ndoto za mtoto wa kitanzania jinsi zinavyozidi kupotea kwa kukosa fursa ya kuendelea na elimu kutokana na sababu mbalimbali, na si mtoto tu hata wazazi nao wanaina kipaji katika mtoto wao lakini kutokana na sababu kadhaa ndoto hiyo hufa. Jamii inatakiwa kujitolea ili fursa hii ya msingi kabisa ya elimu isiishie njiani anasisitiza mrembo miss World 2024 Krystyna Pyszková kutoka Czech anapigia chapuo mradi huo wa elimu hadi mtoto ashindwe mwenyewe na siyo kutokana na vikwazo vingine.

Miss World 2024 WINNING answer: Krystyna Pyszková from Czech Republic


View: https://m.youtube.com/watch?v=qoXQfBlIvnYKrystyna Pyszková is a young woman from Třinec who has a passion for learning and exploring. She is 181 cm tall and has a slim figure with 86-59-89 measurements. She is currently pursuing a law degree at Charles University, as well as studying marketing in Austria. She has a creative side and enjoys painting and playing musical instruments such as the flute and the violin. She is also a model and has a humanitarian project to educate children in Tanzania. She loves to travel and learn about different cultures, people, and places. She also likes to keep fit, ride horses, and improve herself.
Source : Prague Post.
 
uafrika ni LAANA
 
Listen before you thank me..

Simply Mama Salma ni mjinga, aliyekuwa na wazo la kijinga, akalipeleka kwa wajinga wenzie, wakalipitisha...

Sasa kwanini unamkingia kifua huyo chirf wa ujinga?!
🙏📝
 
Hakuna link
Hakuna picha
Hakuna video

Huu uzi haujafunguliwa na mtu anayejitambua.

Unajidhalilisha kwa maandiko mareefu yaliyojaa uongo na uzandiki
 
Unazani mwenye shibe huwa anamkumbuka mwenye njaa? Mpaka uwe na ufahamu wa ziada wakuzaliwa nao, si uliona mwingine anasema no.za magari zinaongezeka hivyo watu pesa wanazo, halafu usiwaseme wanawake tu sema mijitu maana wanaume ndiyo wenyewe huyo mama ni tone tu.
 
Tatizo la msingi hapa nchini ni UJINGA na huu wameukumbatia watawala

Kuna mtu kasema hapo juu kuna waziri kapongeza hiyo makala ya miss kwa kuitangaza Tanzania duniani

Siyo sifa njema kutangazwa kwa umaskini hata kama wewe ni maskini

Hili swala lingetakiwa liwasikitishe viongozi wetu kwamba wemeshindwa kutatua matatizo yetu mpaka binti mdogo toka mbali yeye na marafiki zake wanakuja kututatulia changamoto zetu na serikali hipo bunge lipo wanachowaza ni posho marupurupu na ten pacent.
 
Wanasiasa wa kiafrika wanajifikiria wenyewe tu
 
Kupitia sheria ile jiulize familia ya Mwinyi inalipwa kiasi gani?

Jiulize familia ya JK inalipwa kiasi gani?

Few years to come utakuta familia moja inalipwa zaidi ya bilioni kumi kwa mwaka mmoja bila kufanya kazi wamekaa tu nyumbani kama wastaafu.

Hawa wanasiasa wanawake wanatamaa sana kwa sababu hakuna hata mmoja mwenye biashara yoyote anayoendesha. Wote hawa hakuna anayelazimika kulipa kodi wanaishi mostly kwa utegemezi that's why wanawaza wakistaafu wataoshije......huko duniani madaraka yanakabidhiwa kwa familia zenye kulipa kodi na zinazofahamu maana ya kutafuta fedha.

Sorry to say but wanawake wamegeuka kuwa na tamaa ya vitu vya bure na hivyo kuongeza utegemezi.....wanawaza kuhudumiwa
 
Kosa lake ni ulafi. Zaidi ya kulala kitanda kimoja (kama ilikuwa) na JK amechangia nini Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…