Mkuu, ukiwa unatanguliza usomi wako, unakuwa unazidi kuharibu kama walivyoharibu wasomi wenzako wengi walioko serikalini!
Amekosa nini?
Anajua kuwa kuna waliotumika na serikali physically kwa miaka zaidi ya 30 na wanalipwa 30m tu kama kiinua mgongo kwa miaka hiyo yote na kisha kupewa 33% ya mshahara wake kama monthly pension kwa miaka 12 tu? Ilhali yeye, MUME wake analipwa 80% ya mshahara wa aliyeko madarakani?
Yeye akipewa TAASISI iliyokuwa inavuna pesa kwa jina la serikali na nafasi ya mume wake!
Unajua kwanini Magufuli aliamua kushusha mshahara wake? Akilipwa yeye tsh 9m, maana yake wastaafu wanalipwa 80% ya 9m, akilipwa tsh 35m aliyoiacha Kikwete, ina maana jamaa wanachukua tsh 28m, kisha na yeye anataka alipwe ngapi ikiwa alinufaika kwa asilimia kubwa sana ya madaraka yale?
Angeweza kujimilikisha mali zote bila hiyi nafasi?
Unadhani mwalimu au mkurugenzi wa wilaya anayo nafasi ya kupeleka hoja ya kuwanufaisha wenza wao na ikapita?
Unadhani wehu wanaoingia mjengoni ni watu wanaweza kubadilika na kuwa timamu?
Unadhani akina Doto magari, Mwijaku, Baba Levo n.k.wanaweza kuwa think tank? Maana ndo hao walio mjengoni!
Mwisho, ni dhahiri shayiri na wewe ni mwanachama!