Video: Bodaboda asababisha Ajali

Video: Bodaboda asababisha Ajali

Kumbe!!! Haya maisha,yaache.
Kuna vitu unaweza epuka,kimoja bodaboda. Mfano hapa mjini mtu anapanda bodaboda ili awahi tu au hataki daladala au Bajaj sio kwamba hana option.
Asubuhi njia ya kilwa road bodaboda kama nzige zinaelekea town wakati hio ruti ina daladala.
Bodaboda panda ukitoka main road kuingia kwako huko nje ya mji.
 
Rafiki yangu kampoteza mtoto wake katoka kumaliza masters degree tu, ni binti kapanda bodaboda kaingizwa uvunguni kwa lori. Wanawake ndio wanapenda sana bodaboda hawaelewi kabisa ukiwaambia.
Muda mwingine ni wa kuwaombea tu Mungu aweke mkono wake
 
Kuna vitu unaweza epuka,kimoja bodaboda. Mfano hapa mjini mtu anapanda bodaboda ili awahi tu au hataki daladala au Bajaj sio kwamba hana option.
Asubuhi njia ya kilwa road bodaboda kama nzige zinaelekea town wakati hio ruti ina daladala.
Bodaboda panda ukitoka main road kuingia kwako huko nje ya mji.
Mimi nilichopinga,ni hiyo kusema eti haitakaa itokee. Wakati mwingine,ndo ile kujiona umefika. Mbona wenye pesa myingi,kuna wakati wanalazimika!!! Mazingira yanaweza yakawa chanzo cha kupanda. Angeongelea uzembe wao. Binafsi nikipanda,nakuelekeza uendesheje. Hutaki,unaniacha. Au namtafta ninaye muona umri umesogea.
Na huyu sasa,asijikute ana ka IST,af anawaona wapanda pikipiki kama masikini
 
Wewe umeacha, ila Nina uhakika familia Yako haijaacha!! Akina mama,dada zetu, na watoto wetu wanaopandishwa bodaboda na mama zao ni hatarishi Zaidi!! Akina mama huwambii kitu na bodaboda!! Unakuta mijimama mwili mkubwa akili zero wamajipakiza bodaboda wakiwa majimishikaki!! Wawili na mtoto mdogo katikati, my Goodness!! Ila ndio mwanasiasa mkubwa alisema kama ni mtu na mpenzi wake wacha wafe Pamoja!! Sijui tunakwenda wapi
Mimi nilishawaambia wasipande bodaboda. Mtu akipata ajali ya bodaboda asinisumbue( nitamsaidia damu nzito ila nitamwambia I TOLD YOU)
 
Katika kitu nimefanikiwa ni kuacha kbs kupanda boda boda
Nikipanda wanajua ninamuendesha yeye mpaka napofika nakabidhi funguo yake arudi na vurugu zake .... Bodaboda aniendeshi labda wale watu wazima au namfahamu kabisaaaa uendeshaji wake...noma sana ... Tulibananishwa kati huku basi huku Lori la matunda ...noma sana
 
Mimi nilichopinga,ni hiyo kusema eti haitakaa itokee. Wakati mwingine,ndo ile kujiona umefika. Mbona wenye pesa myingi,kuna wakati wanalazimika!!! Mazingira yanaweza yakawa chanzo cha kupanda. Angeongelea uzembe wao. Binafsi nikipanda,nakuelekeza uendesheje. Hutaki,unaniacha. Au namtafta ninaye muona umri umesogea.
Na huyu sasa,asijikute ana ka IST,af anawaona wapanda pikipiki kama masikini
Sio suala la kuwa na pesa nyingi. Ni maamuzi ya mtu. Rafiki yangu mmoja anaacha V8 anadandia bodaboda na ashaanguka lakini haachi.
 
Rafiki yangu kampoteza mtoto wake katoka kumaliza masters degree tu, ni binti kapanda bodaboda kaingizwa uvunguni kwa lori. Wanawake ndio wanapenda sana bodaboda hawaelewi kabisa ukiwaambia.
Sasa ushawaona wana akili?
Hujaona mwingine anakula urojo tu
 
Nikipanda wanajua ninamuendesha yeye mpaka napofika nakabidhi funguo yake arudi na vurugu zake .... Bodaboda aniendeshi labda wale watu wazima au namfahamu kabisaaaa uendeshaji wake...noma sana ... Tulibananishwa kati huku basi huku Lori la matunda ...noma sana
Nakumbuka mara ya mwisho kupanda nliachwa na gari nkawa naliwahi aiseeee! Nlisali njia nzima 😂😂😂Mkuu lugha ya roho mtakatifu ni kwel😂
 
Ila maisha hayana formula ndugu zangu yanii hawa boda boda hapana aiseee tunapanda ila kifo nje nje.. kuna jamaa yetu alinunua gari week 2 zimepitaa juzi kati akasema aache gari akodi boda awahi mahali flani akwepe foleni daah kama ndoto aiseee...!!
 
Back
Top Bottom