Haiwezekani vijana ,wamama na wababa wa kitaa wakukatae wote ,kuna kitu hakipo sawa kwa Mwakinyo.
Yule jamaa ni mwizi kweli ila sheria haziruhusu kumpiga mwizi ,vipo vyombo vya kisheria vinavyoshughulika na wahalifu ,Mwakinyo aombe tu yule mwizi apone ,akivuta kamba mwakinyo atakabiliwa na kesi ya mauaji ila kwasasa kesi yake ni shambulio la kudhuru mwili.
Mwizi amehojiwa anasema kwamba alikuwa anapita tu njiani akaziona nazi 6 akaokota then mbwa walivyopiga kelele mwakinyo ndiyo akatoka na kumkata ,je mwakinyo atajinasuaje kwenye maelezo ya mwizi? Ndiyo umuhimu wa kufunga CCTV camera unapoonekana.
Kama Mwakinyo amefunga CCTV camera lazima footage ya tukio litakuwa limeonekana.