Mfundishe mwanao asiwe mwizi, akiwa mwizi atachomwa moto mbele yako na usifanye chochote. Yaani huyo dogo anasema alikutana na nazi akaokota hizo nazi zilitoka wapi? Je kama yeye angeingia ndani na kumvamia na kumuua huyo mwenye mali ungesemaje.
Kuna mwenzako aliingia kwangu kachukua vitu maana alijua watu wote wamesafiri maana mimi sikai home kumbe mimi nimerudi. Nilimvinya vya kutosha kwa mazoezi wala sikumgusa ila wakashindwa kutembea vizuri.
Alivyo toka nje kaa siku tatu sijui walishaulina nini na watu wake eti wanakuja kudai mimi nilimkamata akiwa anapita njiani nikamwingiza ndani ya gate. Kwahiyo watanishitaki nikasema nenda huko mnakotaka, hawajui kuwa nime install cctv camera tena kwa ujinga wao ni yale makamera yanayo onekana kabisa, nikamwita mjumbe nikamuonyesha alivyokuwa anaruka ukuta, anabeba vitu na vibaiskeli vya watoto. Wakabaki wanashangaa kumbe kanipaka mbaya kuwa mimi ni katili kibaya zaidi ni mzawa na mimi ni mgeni.
Hata siku moja usicheke na mtu anaye kuja kukuibia na hakuna mwizi mdogo wala mwizi mkubwa wote ni wezi wakikupata kwenye 18 zao wanakuua bila huruma