Mimi ningekuwa raisi ningekuwa kiongozi katili ambae hajawahi tokea ujinga kama huu nafutilia mbali wahusika.nitajibu kwa Mungu.
Ukiwa msafi hua unaruhusiwa kuadhibu Kwa Mujibu Wa Sheria.
Viongozi wengi au Hata wanaotoa hukumu wengi ni wavunja Sheria ndio MAANA hawana uhalali Wa kufutilia mbali maovu na waovu.
Yesu alisema,'Asiye na dhambi awe Wa kwanza kumpiga jiwe Yule Mwanamke mzinzi."
Tujenge jamii ya watu wanaofuata Sheria na desturi zetu Ili iwe rahisi kukemea.
Ukichunguza Kwa kina na Kama Mungu akasimumia ukweli ni kwamba Hata watunga Sheria wetu wengi SIO watu wema . Wabunge wengi wanawake hawana ndoa ,wanabadilisha wanaume kama nguo. Wabunge wanaume wengi nao ni hivyo Hivo ,MICHEPUKO na wake za watu ,Ulevi na majivuno,kiburi,ushirikina n.k. Watu waliokosa kiasi. Jamii ya namna hii haiwezi kamwe kusimamia maadili. Mungu aturehemu tu Kwa Huruma zake lakini hiki ni kizazi Cha zinaa.Ni kizazi cha Siku za mwisho. Yale yaliyotendeka wakati Wa Sodoma na gomora yanarudi Kwa Kasi kabla ya kiyama.
Maovu yote yanafanywa Kwa Kasi KUBWA sana Sio tu Ushoga ,Hata uzinzi, rushwa ,dhulma ,mauaji , kutengeneza mpaka vyakula bandia ,mafuta bandia ,madawa bandia, magonjwa ya kutengeneza n.k.
Serikali za Kidunia zimetoa Fursa NZURI Kwa waovu kushamiri na wema kuumia Kwa kusononenka na kutishwa . Waovu wanamwagilia miaoyo Yao Kwa chochote wanachoona kinawafaa Kuridhisha tamaa zao.