Video clip: Akili mnemba zimefikia level za hatari sana, tukizubaa, binadamu wote tutapoteza ajira

Video clip: Akili mnemba zimefikia level za hatari sana, tukizubaa, binadamu wote tutapoteza ajira

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Hebu angalia hizi slide mbili za video zilizotengenezwa na akili mnemba ndani ya dakika chache tu.., fully rendered. Kwa sasa wasanii na maprodyuza wa muziki ndio wanaipata pata.., ila huko tuendako, hata wahandisi na wabunifu majengo lazima tutakwenda na maji.

Hata madaktari (Medical) wajiandae, kuna maariboti yanafungiwa akili mnemba hao watakuwa balaa, yaani likikuangalia tu na jkataja dalili, anafunguka kila kitu…, hata sikui itakuwaje sasa aisee..


View: https://www.instagram.com/p/C9lw46LIomN/?igsh=MXdkNzM4aDE5NjV5Ng==

==========================
Akili Mnemba kukabidhiwa kiti cha Urais.

Akili Mnemba itakuwa installed na software ya katiba, na wote tutakagua kuhakikisha algorithm hairuhusu uvunjwaji wa katiba kabla mnemba hajaapishwa. Mnemba ataunganishwa moja kwa moja na ‘Gepg‘ (Government electonic payment gateway’, na hakuna hata transaction moja itakayofanyika bila yeye kujua na kuruhusu, na pesa za cash zote zitaondolewa, kila mtu atafanya malipo kwa namba yake ya NIDA iliyochapwa kwenye chipset itakayowekwa mkononi, hivyo hapatakuwa kabisa na ukwepaji kodi!

Mnemba anaweza hata akakutumia taarifa ‘telepathically’ kwa kutumia teknolojia mpya ya ‘Neuralink’ hata kama upo ndotoni..

Mnemba atakuwa connected na account zote za Bank za kila raia, hata zile za nje ya nchi, ufisadi utakuwa ‘impossible’…, kodi itakatwa na kulipwa automatically, maendeleo yatakuja kwa kasi ya 5G.., na wote tutaanza kuona kama tuko peponi..

Raia akivunja kanuni zilizowekwa kama miongozo ya Mnemba kwenye Algorithm, Mnemba anaweza akaishikilia NIDA ya raia huyo isiweze kununua wala kuuza chochote hadi pale raia huyo atakapofanya yale ambayo Mnemba anayataka na itakuwa ni kama amri, atakaebisha atakufa njaa huku anapesa kwenye bank.., hi itakuwa ni utii wa sheria bila shurti at its Finest. Yajayo yanasisimua sana..
=========================
11/09/2024


View: https://www.instagram.com/reel/C_xPf3usEwA/?igsh=MXh2ejhnd2Zic2hzYg==
 
Lakini tunaona wanaotoa ushuhuda kuhusu errands kibao zihusianazo na AI...Tesla zinachochora.....mara AI zinajibu ndivyo sivyo etc.

Well, hazipaswi kuwa na makosa kwa ukubwa huo!
Zinaboreka kila kukicha, very soon magari ya kibiashara yataendeshwa na akili mnemba, madereva wajiandae.., na ajali zitakuwa zero
 
Nasubiri siku akili mnemba itapopewa cheo cha Urais, yaani maamuzi yote ya serikali yafanywe na akili mnemba, maana Rais wa akili mnemba hawezi kula rushwa wala kuuza mbuga wala bandari.., yeye ni maendeleo tu..
Umenikumbusha mjadala bungeni na kwingineko kuhusu, DP world wahusika walivyo jizima data, yaani kuahirisha kufikiri kwa nafsi, (human herding)
 
Mleta mada si kweli kama AI itakuja kufikia utashi and reasoning ya binadamu.

AI unazoziona Leo ni Narrow AI means they are good in specific tasks but not general tasks

So msiwe na hofu...
 
Mleta mada si kweli kama AI itakuja kufikia utashi and reasoning ya binadamu.

AI unazoziona Leo ni Narrow AI means they are good in specific tasks but not general tasks

So msiwe na hofu...
Ndo maana Africa tunaumizwa siku zote. Imagine 2050 AI itakuwa imefikia wapi kama sasa hivi ukitaka ikutengenezee website inafanya yenyewe kwa kuiambia tu ni nini unataka kipungue au kiongezeke.
 
Back
Top Bottom