Hujui na huelewi..
Na kwa taarifa yako mimi pia ni yatima sina baba wala mama, wote walishafariki..
Lakini hoja wala siyo haya mawazo yako butu na yenye kutu..
Hoja ni hii, kwamba, kwanini wewe usielewe kuwa ktk nchi yetu tuna mfumo wa utoaji haki kwa ajili ya watu wote wakiwemo yatima, wajane, waliodhulumiwa chochote sio ardhi tu?
Nimesema toka awali kuwa, kila mtu anajua kuwa mfumo wetu huu wa utoaji haki kupitia mahakama zetu uko compromised na serikali (executive) kiasi cha kuathiri HAKI ZA WATU..
Lakini walioiharibu mahakama na mfumo mzima wa utoaji HAKI ni hawahawa kina Jerry Silaa na serukali yao kupitia chama chao CCM kilichoshika hatamu serikalini..
Na cha ajabu ni wao haohao tena wanatoka na kuanza kuilaumu mahakama na Majaji/mahakimu kuwa hawatoi haki sawasawa..!
Ina wewe
Lukub hulioni tatizo kweli?
Na kweli kabisa unadhani Waziri Jerry Silaa au Rais mwenyewe anaweza kuingilia na kutengua hukumu ya kisheria ya mahakama pasipo kufuata utaratibu huohuo wa kimahakama?
Mimi nakuambia haiwezekani hata kama hukumu hiyo imetolewa kwa kuonea upande mmoja. Na hata kama aliyeonewa ni yatima, mjane, mfiwa au yeyote..!!
TIBA YA HIKI ANACHOKILALAMIKIA Waziri Jerry Silaa sio cheap statement kama hii ya kwako ya kujificha nyuma ya u-yatima au u-jane au u-fiwa na mengine yanayofanana na hayo. Bali tiba ya kweli na ya kudumu ni;
1. Kuwaambia CCM na serikali yao kuwa wao ndio wameiharibu mahakama kwa kuwapa maelekezo mahakimu na majaji kuamua mashauri kinyume cha sheria na haki. Hilo limejengeka na kuwa utamadauni. Sasa utamaduni huo unaanza kumtafuna na kumwathiri kila mtu wakiwemo hao yatima na wajane wako. Hivyo tuwaambie waache unafiki na warudi kwenye mstari..!
2. Wao kina Jerry Silaa na CCM na serikali yao ndio wanaoteua majaji ambao wengine ni makada wa CCM na wako kule kuwalinda wao na kuharibu mtiririko mzima wa utoaji haki kwa kulea rushwa na upendeleo. Sasa wanamlalamikia nani. Mfano huyo Jaji anaemlalamikia si kawekwa pale na Rais na mwenyekiti wake wa CCM? Alikuwa hajui status yake?
3. NI LAZIMA SASA NA NI WAKATI wa kujenga mfumo mpya wa kikatiba, kisheria na kiutawala utakajenga mfumo huru wa utoaji haki (judicial system) na kuzifanya mahakama zetu kuwa huru bila kuingiliwa na mhimili wa utendaji - setikali (executive). Hii inawezekana tu kwa kuirekebisha katiba yetu ya mwaka 1977 inayompa madaraka mtu mmoja aitwaye Rais kuteua kila Jaji au kuifuta kabisa hiyo na kuandika nyingine mpya..
HIYO NDIYO SULUHU. Na kamwe suluhu sio hiyo ya unafiki wa wana CCM akiwemo waziri Jerry Silaa au wewe
Lukub unayeficha udhaifu wa mfumo wa utoaji haki kwenye status ya u - yatima au u-jane..!