Video Clip: Rufiji litangazwe kuwa ni eneo la hatari na Serikali iwahamishe wananchi mara moja

Hatukatai kumwaga maji kutoka kwenye bwawa, bali tunasema wananchi wahamishwe kutoka eneo hatarishi. Shirikisha kichwa chako kabla hujaanza kuandika
Hakuna eneo hatarishi mkuu, kuna watu walioenda shule wametafiti na kujenga lile bwawa.

Na walijiongeza kwamba mafuriko huwa yanatokea, ndio maana kuna milango 9 jiulize kwanini isiwe milango 30 au 5 au 1 .

Wale waarabu waliojenga kwao walijenga bwawa lenye kina cha pili kwa urefu duniani. Miaka kibao iliyopita.

Nyie watalaam wa matusi na wanasiasa ndio mmegeuka ma injinia wa kukejeli elimu za watu.
JPM alitoa tenda ya kimataifa na walioshinda tenda walikutana na watalaam wa hapa na baadhi ya takwimu zinazotumika kufanyia kazi ni pamoja na takwimu za mvua na za mto za muda mrefu na hii sio El nino ya kwanza kutokea hapa nchini.
 
EIA iliyoelezwa na wale waliopiga kelele ilikuwa ni athari za kutaka miti na uoto kwa asilimia 1% ya Mbuga ambapo miti ilipatwa kwa eneo la ukubwa wa DSM.

Miongoni mwa waliopinga huu mradi ni pamoja na Kipara ambaye akaja kuapishwa kwa mfumo wa kufutana machozi. Na huyo ambaye anautamani sana ukuu wa nchi hii hakuona kama ni busara kusimamia huu mradi kwa ufanisi na alichokifanya huko hakina tofauti na alichokifanya kwenye miundombinu ya TANESCO. Unapofikia mahala mtu halali akafanya mambo haramu halafu anaendelea kulindwa na kuheshimishwa maana yake ni kwamba serikali inawafitini wananchi.

Kipara na mabeans wawekwe chini ya uangalizi kwa haya matokeo waliyoyatengeneza. Waliingia kuharibu ndo maana wakaondolewa baada ya kugundulika uhuni wao. Huwezi ukafanya vizuri kisha ukaondolewa eneo hilo.

Waendelee kulindana lakini ikumbukwe KARMA haina rufaa
 
Ukweli ni kwamba serikali ilihamisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye maeneo yenye mafuriko (REJEA OPERATION VIJIJI MWAKA 1974 WALILETWA KTK ENEO SALAMA ) BAADA YA HAPO WATU WALIANZA KURUDI KTK MAENEO HAYO KINYEMELA NDIO WALIOATHIRIWA SANA NA MAFURIKO HAYO SIO KAMA ENEO LOTE LA WILAYA h YA RUFIJI MAJI YANAFIKA. KUNA SEHEM NIMESOMA MDAU MMOJA ANATAJA SHULE YA SEKONDARI MKONGO NA UTETE ZIFUNGWE NILISHANGAA SANA SHULE YA MKONGO MAFURIKO YA KUFIKA PALE TUTAITA SIO MAFURIKO TENA NI GHARIKA
 
Haya yote ni matokeo ya ubishi wa Jiwe.
Mtu hakuwa anasikiliza washauri wake.

Angekuwepo leo sijui angekuwa anajisikiaje kwajinsi watu wasiyo na hatia wanateseka
 
Hao wanyama wana eneo kubwa tu la kuhamia Selous ni kubwa sana inakutana na Mikumi na inasambaa mikoa ya Lindi, Ruvuma, Morogoro na Pwani
Tuangalie binadamu wenzetu ambao wanapoteza maisha
 
Mleta mada acha kuwachanganya watu kwa hiyo video. Hiyo video ninayo muda mrefu sana mimi na wala siyo ya leo wala jana.ila naona umeamua tu kuja kupigia propaganda hapa jukwaani kwa sababu zako binafsi.
Wewe ni bwege sana,unaleta uchawa wako kwenye mambo muhimu yanayohusu maisha ya binadamu?

Hivi nyinyi viumbe mmeumbwaje?
Mlete Uzi ameeleza vema kabisa juu ya hatari zinazo mkabili binadamu mwenzetu pale Rufiji.
 
Kwanza,
1. wewe ni mvivu wa kufikiri, ni mtumwa wa matatizo, UNESCO ikikufungia bandani unakaa humohumo hadi ufe.
2. Hii clip ipo mtandaoni siku nyingi.
Je haina ukweli kwa yanayotokea hii leo?
Jana tu tayari tumetangaziwa watu 2 wameshapoteza maisha.

Huoni kuwa mleta mada ameuleta kwenye muda muafaka?
 
Nyie Mmmbwa wa Tz hamnaga zuri kwenu, Kila jambo mnalitengenezea ubaya, Me nikazani utashauri hao wananchi wa eneo hilo ndo watafutiwe pa kwenda we unakosoa bwawa ambalo lina umuhimu kwa Taifa!!!
Kwahiyo bwawa lina umuhimu kuliko maelfu ya watanzania wenzetu wanaopoteza maisha?
 
Nafikiri umetukana bila kusoma ushauri. Heading tu inaitaka Serikali iwahamishe watu wa hapo. Imagine wangekuwa ndugu zako, je ungeandika ushuzi kama huo?
Hajitambui huyo kisa anaitetea ccm
 
Mkuu tumekuelewa sana wachana na hao wafia chama cha kijani
 
Kama unataka kutuaminisha kuwa hizo kuta haziwezi kubomoka kisa zimejengwa kwa muda wa miaka 2 nikwanini wanafungulia hayo maji?
 
Kwahiyo bwawa lina umuhimu kuliko maelfu ya watanzania wenzetu wanaopoteza maisha?
Kenge nyie,,juzi mlikiwa mnlia umeme mkawa mnaahidiwa kuwa bwawa Hilo ndo marobaina..mkakesha mkikenua meno humu kwba mama kaupiga mwingi sasa mnageuka kitu Gani au mnagilimbwa
 
Tangu lini mwananchi alithaminiwa?
Huko Lindi mwananchi akiuwawa na tembo serikali inatoa pole ya laki 5 ila mwananchi akimuua tembo serikali inamfunga miaka 50 na fidia milioni 50. Unfortunately askari wa TAWA wanakuua kabisa
Aibu sana
 
Hapa, umeongea! Hii 'point' ni nzuri sana ! [emoji120][emoji1666][emoji2936]
 
Hapo ndipo sasa kuhusisha wataalamu wa elimu ya mazingira kunapoonyesha umuhimu. Dikteta alisema mambo ya Environmental Impact Assessment yanachelewesha miradi!! Na nyinyi mkamshangilia
Acha chuki,at the beginning hata nchi zilizoendelea hivi vitu vinatokea,ni swala la kuweka mambo vizuri na baada ya muda kila kitu kitakua sawa.Hivi umeshajiuliza,leo hii uchumi wa nchi ulipofikia kusingekuwa na hili bwawa hali ingekuaje,waasisi waliona mbali sio unabeza kila kitu.Soma hii-(In total, China's domestic dams are reported to have displaced 23 million people as well as significantly affected water availability and environmental quality (International Rivers, 2012).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…