- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Naomba nisiwekemaneno sana. Pitia video hii ujue nini kimejiri Kinsasha DRC.
Miongoni mwa waliouawa hadharani ni raia wawili wa Marekani na mmoja wa Uingereza
Afrika ni mwendo wa kuuana. Anayewini ni yule mwenye timing kali
Miongoni mwa waliouawa hadharani ni raia wawili wa Marekani na mmoja wa Uingereza
Afrika ni mwendo wa kuuana. Anayewini ni yule mwenye timing kali
- Tunachokijua
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ni nchi inayopatikana katika jumuiya ya Afrika Mashariki, Kongo imekuwa ikikabiliwa na mizozo ya mara kwa mara kutoka kwa vikundi vya waasi ikiwemo kundi la M23.
Uhaini ni kosa la jinai ambapo mtu anafanya kitendo chenye madhara makubwa kwa nchi yake Kwa mfano, mtu anaweza kuisaidia nchi nyingine ipigane vita dhidi ya nchi yake kwa kutoa taarifa za siri.
kumekuwapo na kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kikiwaonesha vijana waliovalia sare wakipandishwa kwenye gari, huku kikiwa kimeambatana na madai mbalimbali. Tazama hapa na hapa
Uhalisia wa madai hayo upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii kinaonesha vijana ambao wamehukumiwa kunyongwa kwa makosa ya uporaji na si kwa makosa ya uhaini.
Vyanzo mbalimbali viliripoti kuhusu tukio hilo la zaidi ya vijana 170 wamehukumiwa kunyongwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mathalani CNN waliripoti kuwa kwa mujibu wa mamlaka nchini humo wanaume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 waliokuwa wanajulikana kama ‘kulunus’ ama ‘majambazi wa mjini’ wamehukumiwa kunyongwa kwa makosa ya uporaji na haijaelezwa ni lini tukio hilo litatendeka.
Kipande cha video kinachosambaa kinawaonesha baadhi ya vijana waliohukumiwa adhabi hiyo wakiamishiwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi la Angenga. Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International kupitia taarifa yao ya tarehe 7, Januari 2025 waliyoichapisha katika tovuti yao walimtaka Rais wa Kongo Felix Tshisekedi kusitisha utekelezaji wa hukumu hiyo.
“DRC: Rais lazima asitishe mauaji ya halaiki ya zaidi ya watu 170
Zaidi ya watu 170 wanaodaiwa kuwa ni ‘majambazi’ walihamishwa hivi majuzi kutoka Kinshasa hadi katika gereza la mbali la Angela. Wote walio katika tishio la kifo wanaripotiwa kuwa na umri wa miaka 18-35”