POTOSHI Video: DRC watekeleza mauaji kwa vijana 120 walioshiriki jaribio la uhaini

POTOSHI Video: DRC watekeleza mauaji kwa vijana 120 walioshiriki jaribio la uhaini

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Naomba nisiwekemaneno sana. Pitia video hii ujue nini kimejiri Kinsasha DRC.
Miongoni mwa waliouawa hadharani ni raia wawili wa Marekani na mmoja wa Uingereza




Afrika ni mwendo wa kuuana. Anayewini ni yule mwenye timing kali
 
Tunachokijua
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ni nchi inayopatikana katika jumuiya ya Afrika Mashariki, Kongo imekuwa ikikabiliwa na mizozo ya mara kwa mara kutoka kwa vikundi vya waasi ikiwemo kundi la M23.

Uhaini ni kosa la jinai ambapo mtu anafanya kitendo chenye madhara makubwa kwa nchi yake Kwa mfano, mtu anaweza kuisaidia nchi nyingine ipigane vita dhidi ya nchi yake kwa kutoa taarifa za siri.

kumekuwapo na kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kikiwaonesha vijana waliovalia sare wakipandishwa kwenye gari, huku kikiwa kimeambatana na madai mbalimbali. Tazama hapa na hapa


Uhalisia wa madai hayo upoje?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii kinaonesha vijana ambao wamehukumiwa kunyongwa kwa makosa ya uporaji na si kwa makosa ya uhaini.

Vyanzo mbalimbali viliripoti kuhusu tukio hilo la zaidi ya vijana 170 wamehukumiwa kunyongwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mathalani CNN waliripoti kuwa kwa mujibu wa mamlaka nchini humo wanaume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 waliokuwa wanajulikana kama ‘kulunus’ ama ‘majambazi wa mjini’ wamehukumiwa kunyongwa kwa makosa ya uporaji na haijaelezwa ni lini tukio hilo litatendeka.

Kipande cha video kinachosambaa kinawaonesha baadhi ya vijana waliohukumiwa adhabi hiyo wakiamishiwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi la Angenga. Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International kupitia taarifa yao ya tarehe 7, Januari 2025 waliyoichapisha katika tovuti yao walimtaka Rais wa Kongo Felix Tshisekedi kusitisha utekelezaji wa hukumu hiyo.

“DRC: Rais lazima asitishe mauaji ya halaiki ya zaidi ya watu 170

Zaidi ya watu 170 wanaodaiwa kuwa ni ‘majambazi’ walihamishwa hivi majuzi kutoka Kinshasa hadi katika gereza la mbali la Angela. Wote walio katika tishio la kifo wanaripotiwa kuwa na umri wa miaka 18-35”
MUNGU awasaidie sana

Waarabu na WA Africa hawanaga akili kabisa
 
Naomba nisiwekemaneno sana. Pitia video hii ujue nini kimejiri Kinsasha DRC.
Miongoni mwa waliouawa hadharani ni raia wawili wa Marekani na mmoja wa Uingereza


View attachment 3198602

Afrika ni mwendo wa kuuana. Anayewini ni yule mwenye timing kali
Mbona mnapotosha, hao ni KULUNAS ni kama panya Road wa Tanzania. Wakikukuta njiani ni mapanga tu ndio sheria mpya ikawekea kwamba wakidakwa ni kuuwawa tu. Wala hakuna uhusiano na mapinduzi

Jamiicheck siku hizi imelala sana

Official source
 
1736595592016.png
 
Hao sio wale wa uasi wazee hao ni yale makundi kama huku yalivyo panya road na miaka ya komando Yoso hivyo serikali ya Drc kwa kuhofia lisije kuwa kundi kubwa ndio likapitisha sheria ya damu kwa damu , na wamefanya kusudi kuachia video wengine waogope kitu ambacho kwa namna fulani sio sahihi sana na usahihi unakuja kama nao pia wanamwaga damu za raia wasio na hatia hovyo hovyo basi kisu tuu
 
Back
Top Bottom