Video: Fatma Karume Kwenye Mhadhara wa Kimataifa Asimulia Unyama wa "Kinyago Tulichokichonga Wenyewe"

Tofasiri yake unaijua? Herode alikuwa ni mwenye mamlaka, lakini alipingwa na Yohana mbatizaji kwa madhambi yake, Yohana akachinjwa. Jitahidini kujua ya kutii mamlaka vinginevyo mtakuwa wapotoshaji tu. Wale vijana watatu wacha Mungu, Daniel, Meshack na Abdinego walimgomea Mfalme Nebkadneza wakatupwa kwenye tanuru la moto, Swali: Nebkadneza hakuwa na mamlaka kuu?
 
Yule nduli aliepita lazima asemwe kwa nguvu zote. Hitler, Bokassa, Amini, Mobuttu wanasemwa kwa mabaya yao,

Sasa iweje Magufuli akisemwa iwe nongwa?!
 
Hoja nzito sana hizi.
Safi sana
 
Anatakaje?

Yupo oslo kutafuta sympathy?

Ama bado sijaelewa motive yake?

Tumshtaki Magufuli huko kaburini ama?
 
Nakwambia hivi, two wrongs do not make a right.

Yani hata kama Fatma kawa selective kumsema Magufuli, kama tuhuma zake dhidi ya Magufuli ni za kweli, zitabaki kuwa kweli tu.

Sasa hapa suala ni, je, tuhuma za Fatma dhidi ya Magufuli ni za kweli?

Huko kwa Karume hata mimi nayajua maovu aliyoyatenda.

Na wala sijasema kwamba Fatma is infallible. She is from a political family after all.

Lakini, Karume kufanya mabaya hakumaanishi kwamba Magufuli hakufanya mabaya.

Kwa nini mnaleta distraction ya Karume kama vile inaondoa mabaya ya Magufuli?

Sasa wewe unayajua mabaya ya Karume, na unaona ni muhimu yasemwe leo, halafu kazi ya kuyasema mabaya ya Karume unamuachia mjukuu wake?

Unaona habari hiyo ina mantiki?
 
Anatakaje?

Yupo oslo kutafuta sympathy?

Ama bado sijaelewa motive yake?

Tumshtaki Magufuli huko kaburini ama?

..Magufuli hata angekuwa hai asingeweza kushtakiwa kwasababu Maraisi wana kinga ya kutoshtakiwa.

..Lakini kuna wahusika waliopokea na kutekeleza maagizo ya kuteka, kutesa, na kuua. Wahusika hao wanatakiwa kushtakiwa.
 
Fatuma kenge tu utawala wa babu na baba yake walikufa wengi sana
 
Humu kuna watu hawataki yasemwe kwa uwazi mabaya aliyofanya Magufuli..
Kila binadamu ana udhaifu fulani na ndio maana kila muda kwenye nyumba za ibada tunakumbushwa kuomba toba.

Magufuli kama binadamu aliyepita inabidi asemwe kusudi iwe fundisho kwa vizazi vijavyo kwa namna ya kupata viongozi wenye busara na ngozi nene ( kuhimili changamoto za kiuongozi)

Magufuli hakuweza kuhimili changamoto na hivyo kujikuta anaumiza watu kwakuwa alikuwa na cheo kikubwa kilichompa kiburi.

Lazima Magufuli asemwe kwakuwa hakufuata sheria.. Alipenda sifa binafsi na kujiona kwamba yeye ndiye mwenyewe yupo sahihi.

Lazima asemwe ili iwe fundisho kwa taifa hasa kupata kiongozi mwenye utimamu wa akili katika kuongoza watu na taasisi zake kwa kufuata sheria.. Na kuondoa UMIMI kwa kila jambo mpaka taifa kujikuta amevuruga kila kitu.. Kuanzia ajira, biashara ( kaharibu sekta binafsi Sana), mahusiano ya kimataifa, siasa za manunuzi, siasa za risasi, siasa za zidumu fikra za mwenyekiti..
Alikwenda kufanya Mahakama ziwe hovyo sana hasa pale Serikali ikiwa inalalamikiwa..

Magufuli hakufaa kuwa Rais, alijaa roho ya visasi sana
 
Kumfikisha marehemu kwenye vyombo vya haki?
 
Ni mamlaka zilizopatikana kihalali pekee la sivyo hata waliojitwalia mamlaka kwa kutofuata utaratibu nao watajiona wana haki.
 
Papai halizai embe.
 

Anazani watanzania ndyo watamuelewa?? aliye tu na uhakika hata akigombea leo na huyo anaemponda wtu watachagua kivuli kuliko yy
Sikusikia anatafuta kura.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…