Video: Hatimaye wana CCM majasiri waanza kujitokeza na kusema Samia amevunja katiba ya chama kujiteua mgombea u - Rais. Atakiwa kujiuzuru

View: https://youtu.be/Gl_enK_qbVg?si=XGMbUj8hTJxGpgyp
➡Hatimaye matunda ya kilichofanyika Dodoma tarehe 19/01/2025 kwa Bi Samia Suluhu Hassan kujiteua mgombea u - Rais huku akimwingiza kwenye mkumbo huo Dr Emmanuel Nchimbi kama mgombea mwenza wake, yaanza kujidhihirisha na kupingwa waziwazi..

➡Mzee Malisa (mwanachama mtiifu na mwaminifu wa CCM) ktk video hii, hajajificha bali kajitokeza waziwazi na kusema Samia na wenzake walikosea, walivunja katiba ya CCM na ya nchi kwa kujiteua kuwa wagombea u - Rais huko Dodoma na kutumia "mamlaka yake ya U - Rais" kuu - blackmail mkutano kinyume cha taratibu na kanuni za chama kujilazimisha kuwa wagombea u - Rais...

➡Mwisho kwa sbb ya kusimamia uvunjaji wa katiba na kanuni za CCM pamoja na katiba ya nchi, amemtaka Bi Samia Suluhu Hassan kujiuzuru mara moja nafasi ya uenyekiti wa CCM taifa kwa sababu hafai tena kuendelea kukiongoza chama hicho...

Tazama na sikiliza mwenyewe video hiyo..

Ya siku nyingi hii na hakuna lolote lililofanyika. Hayo yalitakiwa yasemwe na mwanaccm mwenye ushawishi sio hao wavimba macho.
 
Samia na wenzake walikosea, walivunja katiba ya CCM na ya nchi
Aliyevunja katiba ni mzee wa Msoga, huyu mzee ana maslahi binafsi kwa bibie kubaki ikulu...

Bibi Titi ni kama mbuzi wa kafara tu wala hakujiteua na hana uwezo wa kujiteua.. Mchezo mzima umechezwa na mstaafu so kama ni mashtaka basi ashitakiwe mzee wa Msoga mvurugaji atumiaye bahasha...

Nyerere alimtaja huyu mkwere kuwa ni mhuni ila Nyerere alipokufa mhuni akaingia ikulu kihuni - maana alitembeza bahasha kwa wajumbe wakampitisha.
 
Kumeanza kuchangamka....na walivyo hawapendi kuambiwa ukweli kwa vile walishakigeuza chama kama taasisi ya ukoo na usultani basi kazi anayo bwana malisa
 
View: https://youtu.be/Gl_enK_qbVg?si=XGMbUj8hTJxGpgyp
➡Hatimaye matunda ya kilichofanyika Dodoma tarehe 19/01/2025 kwa Bi Samia Suluhu Hassan kujiteua mgombea u - Rais huku akimwingiza kwenye mkumbo huo Dr Emmanuel Nchimbi kama mgombea mwenza wake, yaanza kujidhihirisha na kupingwa waziwazi..

➡Mzee Malisa (mwanachama mtiifu na mwaminifu wa CCM) ktk video hii, hajajificha bali kajitokeza waziwazi na kusema Samia na wenzake walikosea, walivunja katiba ya CCM na ya nchi kwa kujiteua kuwa wagombea u - Rais huko Dodoma na kutumia "mamlaka yake ya U - Rais" kuu - blackmail mkutano kinyume cha taratibu na kanuni za chama kujilazimisha kuwa wagombea u - Rais...

➡Mwisho kwa sbb ya kusimamia uvunjaji wa katiba na kanuni za CCM pamoja na katiba ya nchi, amemtaka Bi Samia Suluhu Hassan kujiuzuru mara moja nafasi ya uenyekiti wa CCM taifa kwa sababu hafai tena kuendelea kukiongoza chama hicho...

Tazama na sikiliza mwenyewe video hiyo..

Japo kasema ukweli lakini atapotezwa mazima na hii serikali katili kabisa
 
Mkutano mkuu ni mkubwa kuliko vikao vyote vya CCM

Waweza amua lolote mradi maamuzi yawe ya wengi wajumbe wa mkutano mkuu

Huyo atakuwa Chadema aliyenunua kadi ya CCM

Mkutano mkuu ukishaamua jambo limeisha hilo kinachofuata utekelezaji
Mkutano mkuu uliamua lini kutengua katiba,? Ule ni uhuni ndugu
 
Mkutano mkuu waweza amua lolote sababu ndio huamua hata katiba

Katiba ya CCM huwa haipigiwi kura na wanachama nchi nzima

Madaraka yamekasimiwa kwa mkutano mkuu mradi yakubaliwe na wajumbe walio wengi
 
Hiko chama huwa hawataki ukweli usemwe hadharani. Chama cha wanafiki
 
Mkutano mkuu waweza amua lolote sababu ndio huamua hata katiba

Katiba ya CCM huwa haipigiwi kura na wanachama nchi nzima

Madaraka yamekasimiwa kwa mkutano mkuu mradi yakubaliwe na wajumbe walio wengi
Sawa, mbona utaratibu haukufatwa. Zingetolewa fomu kisha ndio wapige kura.
 
Fomu hata ikitolewa inatakiwa mapendekezo yazurure koteeee mwisho wa siku mkutano mkuu ndio mwamuzi

Sasa pale mkutano mkuu wenyewe umependekeza na kuamua ambao una viongozi wote toka kila eneo la nchi bara na visiwani wawakilishi wao
 
Mbona Wezi huko uswahilini wanauawa na wananchi hawakamatwi?

Aweke vifungu tujiridhishe 🐼
Katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), mchakato wa kikatiba wa kumpata Mgombea Urais na Mgombea Mwenza umeainishwa katika Katiba ya CCM. Kwa mujibu wa Katiba hiyo, hatua zinazofuatwa ni kama ifuatavyo:

1. Uchukuaji na Urejeshaji wa Fomu
Wanachama wenye nia ya kugombea urais huchukua na kurejesha fomu za maombi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na chama.

2. Uchambuzi wa Awali na Uteuzi
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) hupitia majina ya wagombea na kuchagua majina matatu ya wanachama wanaofaa kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3. Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa
Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa hupokea majina matatu yaliyopitishwa na NEC na kupiga kura kumchagua mgombea mmoja atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
4. Uteuzi wa Mgombea Mwenza
Baada ya kupitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa, mgombea urais hupendekeza jina la mgombea mwenza kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa ajili ya kuidhinishwa.

Kwa maelezo ya ziada: Ibara ya 108(6) ya Katiba ya CCM, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ina jukumu la "kuteua majina ya wanachama watatu wanaofaa kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Majina haya huwasilishwa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa ajili ya kuchagua mgombea mmoja.

Aidha, kwa mujibu wa Ibara ya 109(3), Mkutano Mkuu wa Taifa "utachagua mgombea wa CCM wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka katika majina matatu yaliyopendekezwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa."

Kuhusu uteuzi wa Mgombea Mwenza, Ibara ya 108(7) inaeleza kuwa "mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakayeteuliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa atapendekeza jina la mgombea mwenza kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa ajili ya kuidhinishwa."
 
View: https://youtu.be/Gl_enK_qbVg?si=XGMbUj8hTJxGpgyp
➡Hatimaye matunda ya kilichofanyika Dodoma tarehe 19/01/2025 kwa Bi Samia Suluhu Hassan kujiteua mgombea u - Rais huku akimwingiza kwenye mkumbo huo Dr Emmanuel Nchimbi kama mgombea mwenza wake, yaanza kujidhihirisha na kupingwa waziwazi..

➡Mzee Malisa (mwanachama mtiifu na mwaminifu wa CCM) ktk video hii, hajajificha bali kajitokeza waziwazi na kusema Samia na wenzake walikosea, walivunja katiba ya CCM na ya nchi kwa kujiteua kuwa wagombea u - Rais huko Dodoma na kutumia "mamlaka yake ya U - Rais" kuu - blackmail mkutano kinyume cha taratibu na kanuni za chama kujilazimisha kuwa wagombea u - Rais...

➡Mwisho kwa sbb ya kusimamia uvunjaji wa katiba na kanuni za CCM pamoja na katiba ya nchi, amemtaka Bi Samia Suluhu Hassan kujiuzuru mara moja nafasi ya uenyekiti wa CCM taifa kwa sababu hafai tena kuendelea kukiongoza chama hicho...

Tazama na sikiliza mwenyewe video hiyo..

Mzee Malisa ana tofauti gani ya Luhaga Mpina?!!!
 
Fomu hata ikitolewa inatakiwa mapendekezo yazurure koteeee mwisho wa siku mkutano mkuu ndio mwamuzi

Sasa pale mkutano mkuu wenyewe umependekeza na kuamua ambao una viongozi wote toka kila eneo la nchi bara na visiwani wawakilishi wao
Hiyo sio sababu ya kukiuka utaratibu.
 
Back
Top Bottom