Video: Hizi drones Bayraktar TB2 za Uturuki ni shida, Waafrika tutafika lini huku?

Video: Hizi drones Bayraktar TB2 za Uturuki ni shida, Waafrika tutafika lini huku?

Putin anajutia hadi balaa, sheikh, na tayari wanajeshi wake wameanza kuiba chakula, njaa inawatesa.....
Wazee wa makanzi wenzio wamepiga kimya wote.
Huna hoja, waleta porojo za kwenye vijiwe vya ghahawa.

Jana tu ALJAZEERA imeripoti kuwa ktk masaa 24 yaliyopita, majeshi ya Russia yamedungua na kuziangamiza hizo drones 6 aina ya Bayraktar TB-2 (zilizonunuliwa toka Turkey) zilizokuwa zinatumiwa na majeshi ya Ukraine.

Hizo porojo nyingine peleka kwa rafiki zenu Alshabbab, ndio huwa mnaelewana lugha.

SmartSelect_20220316-193106_Chrome.jpg
 
Hopefully we know better na pa kufika ni kuwekeza kwenye irrigation na resources of development and welfare na sio destruction...

Kabla hatujawaza vifaa vya kuangamizana kwanza tuhakikishe tuna vifaa vya kuhakikisha matumbo yetu yana chakula, before mabomu / silaha hazijatuangamiza huenda njaa itakuwa ishatuondoa

Famine is a greater and a more realistic problem than an attack from invaders, and most invaders / threats nowadays are enemies within which no drone can succumb...
 
Mkuu nenda telegram upate habari moto zisizo chujwa.achana na huu utopolo wa propagannda za kimagharibi.mwenzako Zelensky anaomba poo .serikali ya Kiev inaanguka muda si mrefu.
Aliingizwa chaka na USA

Nilitegemea serikali yake kuanguka baada ya siku tatu za Mrusi, siku zote nilijua Mrusi ni hatari sana, nilimuona kama level moja na Marekani, kumbe ni bonge la dhaifu, bure kabisa.
 
Nilitegemea serikali yake kuanguka baada ya siku tatu za Mrusi, siku zote nilijua Mrusi ni hatari sana, nilimuona kama level moja na Marekani, kumbe ni bonge la dhaifu, bure kabisa.
Vp Marekani na allies wake walitumia siku ngapi kuingusha Talebani, Sadam Hussein na Gadafi? Vipi marekani amesha muondoa Assad pale Syria?
 
Vp Marekani na allies wake walitumia siku ngapi kuingusha Talebani, Sadam Hussein na Gadafi? Vipi marekani amesha muondoa Assad pale Syria?

Wote hao hakuna jirani wa Marekani, jameni sikujua Urusi wako dhaifu kiasi hiki, ni kama darasani ukute kuna jamaa huogopwa kisa mkubwa kimwili, ila siku apigane na kajamaa kadogo aishie kuaibishwa, kuanzia hapo atachokozwa na kila mtu.
 
Jamaa wameketi ofisini kazi yao kubonyeza bonyeza na kuondosha vifaru utadhani video game, Waafrika tumejiandaaje kwenye utaalam kama huu au bora liende tu.

Halafu tatizo hizi drone sio rahisi kuzigundua kwa radar, jamaa anachagua kifaru kipi amekichukia kwenye msafara wa Warusi anabonyeza na kukiondosha.

Haya mambo husababisha nihisi huruma kwa ajili ya bara letu Afrika, huku hakuna taifa hata moja lenya manowari/sub-marine, aina ya utaalam wa enzi za akina Hitler hatujaufikia, kazi yetu ni wajeda kupasua matofali siku za maonyesho tunashangilia na kujiona wababe.

Hollywood at its best[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
..... Yeah [emoji106] ni kweli kwa sababu Russia wameshakata tamaa kwani waliingizwa chaka na Putin kwa kuambiwa kazi ilikuwa ni ya siku mbili tu na sasa mwisho wake haujulikani na wapiganaji zaidi ya 12,000 wameshapoteza maisha wakiwemo majenerali watatu na vifaa kibao.
Kuna kipindi tuliambiwa majenerali 8.

Kumbe ni kweli wanafufuka.
 
Kuna kipindi tuliambiwa majenerali 8.

Kumbe ni kweli wanafufuka.
Majenerali waliokwisha kufa hadi sasa ni wanne kwani mwingine kafa juzi somebody Oleg yeye ndiye kamanda aliyekiteka kisiwa cha Crimea mwaka 2014.

Hao wanane ni wale waliofukuzwa kazi majuzi na Putin baada ya kuona mambo hayaendi kama walivyokuwa wakifikiria.

Please be advised accordingly.
 
Jamaa wameketi ofisini kazi yao kubonyeza bonyeza na kuondosha vifaru utadhani video game, Waafrika tumejiandaaje kwenye utaalam kama huu au bora liende tu.

Halafu tatizo hizi drone sio rahisi kuzigundua kwa radar, jamaa anachagua kifaru kipi amekichukia kwenye msafara wa Warusi anabonyeza na kukiondosha.

Haya mambo husababisha nihisi huruma kwa ajili ya bara letu Afrika, huku hakuna taifa hata moja lenya manowari/sub-marine, aina ya utaalam wa enzi za akina Hitler hatujaufikia, kazi yetu ni wajeda kupasua matofali siku za maonyesho tunashangilia na kujiona wababe.

du kwa maana hiyo unataka kutuambia kuwa mrusi ameshindwa vita,kwa sababu ya hizo drones au siyo,na vifaru vyake vinaangamizwa?
 
du kwa maana hiyo unataka kutuambia kuwa mrusi ameshindwa vita,kwa sababu ya hizo drones au siyo,na vifaru vyake vinaangamizwa?

Sio drones tu, ni mkanganyiko wa shughuli ambayo Mrusi hakua amejiandaa, hivi vita Putin alivipa jina "special operation", alidanganywa kwamba ataingia na kubadilisha uongozi wa Ukraine ndani ya siku chache, na kwamba atalakiwa na wananchi wa Ukraine, sasa alichokumbana nacho kimemtia aibu hajui pakutokea, vifaru vimeliwa shaba vingi sana kwa kutumia drones, javelin missile na mbinu zingine nyingi tu.

Jeshi lake limeingia kwa kushambulia ndani ya nchi ya watu, wanafyatua fyatua bila uhakika wa wapi pa kupiga, ghafla wanaona vifaru vyao vinalipuka.
 
Back
Top Bottom