Video: Hotuba ya Sugu kwenye msiba wa Mwabulanga yawaacha wana CCM wakijiinamia kwa aibu

Video: Hotuba ya Sugu kwenye msiba wa Mwabulanga yawaacha wana CCM wakijiinamia kwa aibu

Hivi sasa hivi anafanyashughuli gani au amerudi kwenye kazi yake ya kuimba!!
Ila elewa miaka 5 tu ya ubunge imempa maisha ,usimbeze,hutamfikia hata chembe.Lini wew utalipwa mshahara milioni 12 na posho kibao.Yule siyo mwenzio.Watu kwa ufinyu wa kufikiri mnajidanganya sana.
 
Hapa ndipo tumefika ambapo hata misiba inakuwa ni sehemu ya kupashana!

Si dalili nzuri kwa wale wanaoelewa!
Kama watu watakosa mahali sahihi pa kucheulia nyongo, basi maeneo kama haya ndio huwa majukwaa sahihi ya kupata relief kwa yale yaliyokujaza moyoni!

Ni msiba wa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA, usitarajie ukasikia yale unayoyadikia ya CCM zaidi ya yale ya CHADEMA!

Tufungue majukwaa ya kuongea siasa, tukiendelea kudharau haya yatakua mpaka katika majumba ya ibada, majumbani na hatimaye kuvunja umoja wetu.
 
Siasa zinatengeneza kitu kibaya Sana kwenye jamii

Inamaana hata kwenye msiba kunafanywa siasa?

Ni upumbavu ambao ukilelewa mwisho wake watu watatwangana makonde Mbele ya mwili wa marehemu,

Naomba kutumgwe Sheria ya kuheshimu na kutoleta mizaha kwenye misiba
Linawezekana usemalo, Kama mmeweza kutunga Sheria ya kutoshitakiwa mkitoka madarakani itashindikana hii?
Tena huku mkijua kuwa mnatenda mabaya katika nchi yetu
 
Linawezekana usemalo, Kama mmeweza kutunga Sheria ya kutoshitakiwa mkitoka madarakani itashindikana hii?
Tena huku mkijua kuwa mnatenda mabaya katika nchi yetu
Mbali na makosa mengi ya CCM, Je Hilo la siasa Mbele ya maiti nalo unaunga mkono?
 
Hapo ndipo mimi hupenda misiba ya waislamu
yaani SUGU NA HAO WAIMBA SIASA MSIBANI WANGETOKA NA NGEU

Mtu akifariki huwa hawataki ujinga

Wakristo misibani tuko loose hapo Sugu na hao wapambe walitakiwa wakemewe na kiongozi wa dini mara moja
 
Sugu anamapungufu ya akili aliyoyapata baada ya kupigwa vitunguu vya kutosha na Dr.Tulia kwenye uchaguzi mkuu.
 
Siasa zinatengeneza kitu kibaya Sana kwenye jamii

Inamaana hata kwenye msiba kunafanywa siasa?...

Siasa hiyo hiyo ndio ilitumiwa na ccm kufanya mauaji kwa wafuasi wa upinzani, hapo ni ukweli umewekwa wazi tu. Sioni haja yoyote ya wanaccm kuhudhuria msiba wa mwanacdm, ama kinyume chake.
 
Unajua hii dunia, sijui inakwenda wapi? Yaani kila mtu akishindwa, anasema matokeo yamechakachuliwa. Mpaka Trump anabisha kuwa hakushindwa. Sasa sijui kwenye uchaguzi huwa wanakwenda kushindana, au huwa wanakwenda kwenye uchaguzi ili wao tu washinde? Alivyoshinda yeye 2015 ndio ilikuwa halali, si ndio??? Sasa hivi kashindwa, matokeo yamechakachuliwa. Basi hata 2015 yalichakachuliwa pia, ndio maana alishinda.
Hakuna mpinzani anaweza kuchakachua matokeo maana hana vyombo vya dola na taasisi za kimamlaka kumsaidia kufanya hilo. Kilichofanyika kwenye uchaguzi ule tumekiona kwa macho yetu. Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Back
Top Bottom