GE2025 Video ikionesha Watu Wasio na Asili ya Tanzania wakiwa mtaani na mabango yenye Picha ya Rais Samia wakisifu sera zake

GE2025 Video ikionesha Watu Wasio na Asili ya Tanzania wakiwa mtaani na mabango yenye Picha ya Rais Samia wakisifu sera zake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Video inasambaa mtandaoni ikionesha Watu Wasio na Asili ya Tanzania wala hawajui Kiswahili wakiwa mtaani na mabango yenye Picha ya Rais Samia wakisifu sera zake

Inaelezwa kuwa diaspora wa Tanzania waishio Marekani wanaandamana leo huko kuipinga serikali ya Rais Samia hususani kuhusu utekaji, upoteaji wa Raia, na kuuwawa kwa raia katika mazingira yanayohusiana na utekaji au yanayotatanisha. Lakini wakati huo huo diaspora wa nchi nyingine (wasio Watanzania) wanaandamana kwa kulipwa ili kuiunga mkono serikali ya Rais Samia.

Je, diaspora ambao ni raia wa Mexico waishio Washington DC, Marekani wamelipwa ili wakae kwa muda wa saa moja kuonyesha kuwa Rais Samia anapendwa? Je, hizi pesa za walipa kodi huku Tanzania zinakwenda Marekani kuwalipa watu wasiokuwa na ajira au Watanzania walio na pesa huko ndio wanafanya mambo hayo?

Ina maana kuwa 'Wadosi' wa Mexico wanapata 'dei waka' au kibarua cha siku kwa kulipwa ili washiriki maandamano ya kumuunga mkono Rais Samia?
 
Video inasambaa mtandaoni ikionesha Watu Wasio na Asili ya Tanzania wala hawajui Kiswahili wakiwa mtaani na mabango yenye Picha ya Rais Samia wakisifu sera zake
Njmeipenda hii. Haijalishi ni wa Mexico au Wahindi au Warundi lakini wamebeba mabango ya Samia. Hii ndiyo siasa, unamkabili adui kwa namna alivyokuja.

Tofauti ya hawa na akina Mange iko wapi ? Maana nao hawakai hapa lakini wanataka kuipaka nchi matope wakati wako Marekani.

Kila mmoja ashinde mechi zake
 
🤣🤣 ivi huyu mama anachokitaka nini haswa sijawahi ona mtu mwenye uchu wa madaraka kama huyu mama toka tz iumbee
Kwa hiyo hutaki ajibu mapigo? Yaani nyie mumbagaze Marekani kizembe wakati watu wakulipwa USD 10 kwa siku wakiwa na mabango wapo?? Kama mlimuonea Magufuli basi tambua mna deal na mwanasiasa mkomavu. Nyambaaaaaf
 
Soo...sooo shameful, hapa napo zilizotumika kuwalipa hawa mexicans ni kodi za watanganyika daah?

Na huyo dada hapo
anayejibishana na jamaa ndio organiser wa hili tukio?

Kwamba alipewa kabisa fungu la kuwakodi hawa mabwanyenye wa kimexico hili waje na hii counter defensive approach ya maandamano yaliyoandaliwa na akina Mange?.... daah mama Abdul mbona anatapa tapa sana?

Hivi huyo mama huwa anapokea tu kila aina ya ushauri anaopewa na machawa eti ehee?

Sasa si ni vituko hivi jaman? Umewahi kuona wapi maandamano ya kumpongeza raisi ugenini? Hakika ccm imejaza mafisadi na mazero brain..

Bila shaka huu ni ushauri wa Bashite.
 
Huyu mama ataokota makopo siku si nyingi. Jeshi linatakiwa kuchukuwa hatua haraka sana na asilimia 95 ya wananchi itaunga mkono.
 
Kwa hiyo hutaki ajibu mapigo? Yaani nyie mumbagaze Marekani kizembe wakati watu wakulipwa USD 10 kwa siku wakiwa na mabango wapo?? Kama mlimuonea Magufuli basi tambua mna deal na mwanasiasa mkomavu. Nyambaaaaaf
The end (of her) is nearer than you think.... And i am talking about maandamano ya 29. BTW hawa siyo watu wa kulipwa dola 10. Nakuhakikishia kwamba wamelipwa fedha ya kutosha
 
Wengi tuta mshambulia Samia lakini kuna watu wanafanya hivi kwa maslahi yao binafsi ya kufanya ufisadi ili kuonekana wanam support Samia.
 
Back
Top Bottom