Video inasambaa mtandaoni ikionesha Watu Wasio na Asili ya Tanzania wala hawajui Kiswahili wakiwa mtaani na mabango yenye Picha ya Rais Samia wakisifu sera zake
Inaelezwa kuwa diaspora wa Tanzania waishio Marekani wanaandamana leo huko kuipinga serikali ya Rais Samia hususani kuhusu utekaji, upoteaji wa Raia, na kuuwawa kwa raia katika mazingira yanayohusiana na utekaji au yanayotatanisha. Lakini wakati huo huo diaspora wa nchi nyingine (wasio Watanzania) wanaandamana kwa kulipwa ili kuiunga mkono serikali ya Rais Samia.
Je, diaspora ambao ni raia wa Mexico waishio Washington DC, Marekani wamelipwa ili wakae kwa muda wa saa moja kuonyesha kuwa Rais Samia anapendwa? Je, hizi pesa za walipa kodi huku Tanzania zinakwenda Marekani kuwalipa watu wasiokuwa na ajira au Watanzania walio na pesa huko ndio wanafanya mambo hayo?
Ina maana kuwa 'Wadosi' wa Mexico wanapata 'dei waka' au kibarua cha siku kwa kulipwa ili washiriki maandamano ya kumuunga mkono Rais Samia?