Video inafikirisha sana

Video inafikirisha sana

Nikiwaambiaga kuwa DUNIA si sehemu salama ya kufanya uzao wanakataa.
Yaani mimi, mimi hapa eti mimi na akili zangu zote bado naleta watoto kwenye dunia ya hovyo namna hii?
Labda nife nizaliwe tena.
Tunapoelekeza kujinyonga itakuwa kawaida sana ,yaani mtu akiona chenga maisha hayaendi anajinyonga tu kuliko kuwa mtaji wa wanasiasa.
 
Kwa hiyo huyo anaye leta watu, Aliwaleta waje wateseke?

Na aliumba dunia yenye mateso ilhali uwezo wa kuumba dunia isiyo na mateso anao na alikuwa nao?
Lakini pia alituleta bila idhini yetu kuteseka Duniani. Inafikirodha na kuumiza sana. Tunateseka bila sababu yoyote.
 
Hapo ukute dili zote za siku zimekataa, nyumbani kuna familia inasubiri kula ikiwa yeye mwenyewe hajala, mwenye nyumba anadai kodi yake na hana dira yeyote ikizingatiwa siku imeisha.

Hii dunia haipo fair kabisa. Unaweza kuta kuna mtu anakula mpaka kusaza na mwingine hajui mlo wake wa siku anaupatia wapi.

Japo kuna utapeli na ulaghai mwingi, kuna wakati ukiombwa msaada na una uwezo wa kutoa ni bora kuutoa. Unaweza kuta kwa kidogo utakachotoa itakuwa umeokoa familia nzima.
 
Uzi umejaa mawazo ya waliokata tamaa...

Pambaneni maisha ni kugangamala na hayapi tayari kumuonea huruma mtu dhaifu...

Ukiwa dhaifu tu, unageuka kuwa chakula ya maisha...
 
Kuna jamaa mmoja wa taasisi moja nilikua napiga nae soga akaniambia mwalimu wa tuisheni mimi luku ya laki moja haitoshi kwa mwezi mmoja, niliwaza sana maana kuna mtu anafanya kazi kwa siku 30 na bado asipate hiyo laki moja

Kuna muda niliwaza kwanini mzee wangu (apumzike kwa amani) kwanini hakuwa hata mwanasiasa kama kina mkwere huwa sipati majibu, hiyo video imebeba ujumbe mkubwa sana
 
Hapo ukute dili za siku zote zimekataa, nyumbani kuna familia inasubiri kula ikiwa yeye mwenyewe hajala, mwenye nyumba anadai kodi yake na hana dira yeyote ikizingatiwa siku imeisha.

Hii dunia haipo fair kabisa. Unaweza kuta kuna mtu anakula mpaka kusaza na mwingine hajui mlo wake wa siku anaupatia wapi.

Japo kuna utapeli na ulaghai mwingi, kuna wakati ukiombwa msaada na una uwezo wa kutoa ni bora kuutoa. Unaweza kuta kwa kidogo utakachotoa itakuwa umeokoa familia nzima.
Dunia inahitaji watu kuoneana huruma kutoa sadaka na zaka kwa wasiojiweza ,kwa sababu duniani sisi binadamu ndio tunategemea na kuna matabaka ili kusaidiana .

Kuleta usawa duniani wa kimaisha ni wale matajiri (tabaka la juu kabisa) kusaidia tabaka la chini kabisa(mafukara) ,hawa tabaka la kati wanajiweza kimtindo ...Huu mfumo ndio duniani hatuufuati kabisa thus why madhila ya kimaisha ni mengi sana.

Hapo kuna mtu kaingia labda million kwa siku na ukute msela akipata hata elfu 5 familia inakula , kawaida yule wa million moja ampe hata hiyo elfu 5 maisha yaende.
 
Back
Top Bottom