Video: Je, hiki ndio kimesababisha Kemikimba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji kutenguliwa?


Nashukuru sana umeliona hili, ni inferiority complex inawasumbua wanaume wengi pindi wamuonapo mwanamke kwenye uongozi, ndio maana mwanamke akikosea anasemwa kwa jinsia yake ila mwanaume akikosea anaonekana kateleza tu.
 
Huyu mama kazingua sana unadhani aliyeandika hicho kimemo amejisikiaje?! Huenda kimemo kilikuwa na ujumbe mzuri wa kujenga, pia wa kukumbushia jambo sema tu viongozi walio wengi hawapendi kufundishwa, au kuelekezwa wanahofia kuwa nafasi zao zitachukuliwa na aliye na uwezo mkubwa. Anasahau kwamba kiongozi anatakiwa ajifunze kuwa mnyenyekevu na msikivu.
 
Kumbe hata ww hujakiona lkn unaongea as if umekiona.

Yote kwa yote huyo maza anaonesha ni kiburi na jeuri kilichompata anastahili
 
Itakuwa ww ndie mpeleka kinote, lkn ukweli haufichiki yule mama hafai kuwa kiongozi
 
Kama alikuwa ni mtumishi atarejeshwa katika nafasi ya juu ya muundo wa kada yake. Anakuwa Afisa Mkuu Daraja la I. Anaendelea kutumwa na kuagizwa kazi na mkuu wake wa idara au kitengo.
Before alikuwa Mkurugenzi wa mojawapo ya kurugenzi pale Wizarani, kisha alipanda kuwa Naibu KM, then KM
 
Aina hii ya viongozi wapo wengi sana ni vile tu haijatokea matendo yao yakawa captured live on camera.

Hawajiamini, wana uwezo mdogo na wameegesha mambo hivyo ukiwaingilia kidogo tu unawavuruga.

Hawafai kuwa viongozi. Kuna namna nyingi sana za kudeal na insubordination (if that was truly the case) ila sio kuleta taharuki mbele ya watu namna ile.
 

Mkuu Gentamycine:

Umeangalia President Bush alipoletewa habari ya September 11 alipokuwa Sarasota Florida? Haikuwa note...alinong'onezwa sikioni akiwa darasa la chekechea.....Hakupanick hata kidogo kukatisha darasa, alivuta subira alitulia...akaongeza kama dk moja....Hata waliomchukia Bush wanakiri alionyesha utilivu wa hali ya juu......nikipata muda nitaiweka clip/video yake Mkuu.
 

View: https://youtu.be/enLdoTg9HBI
 
Tutegemee nini kwa mtu anaeitwa mikimba?

Kaiachia mikimba.

As a woman she is super stupid. Kazi haziendeshwi kwa "emotions". She's not composed at all.

Kama ndiyo sababu ya kutumbuliwa, anastahiki.
Ndugu yangu πŸ˜†πŸ˜† umenichekesha japo umetukosea. Kemikimba majina ya kwetu Kagera. Huyu dada ndugu yako katika imani ni mtu wa kwetu Kagera. Kwao washika dini swalat hamsa mnasema sio!?

Kwa hili anastahili kutolewa hapo. Anaonekana ana jazba na dharau sana. Hafai uongozi.
 
Majina yanaakisi vitendo.
 
Kikwetu, kama mtoto kakosea na ukawa umeshashika kiboko kwa ajili ya kumchapa, mgeni akibisha hodi, huyo mtoto anaweza kulimika au adhabu ikaahirishwa kwa muda. Ukimwadhibu mbele ya mgeni utakuwa umemdharau huyo mgeni. Waziri pale alienda kama mgeni. Alichokifanya KM ni sawa na kumwadhibu mtoto mbele ya mgeni.

Kikwetu, kugombana mbele ya wakubwa zako ni dharau. Waziri ndiye aliyekuwa mkubwa kuliko wote kwenye hilo kusanyiko. Asingepaswa kureact kiasi kile mbele ya mkubwa wake. Alichokifanya ni sawa na kumwonesha dharau mkubwa wake.
 
Huyu hastahili kuwa kiongozi. Mbona kuletewa ki note wakati unazungumza ni jambo la kawaida sana? Wanaletewa vi note hati kina Bidden, Trump na Obama? sembuse yeye? Yeye nani?
Kwahiyo Boss wake naye hastahili??
Kwani aliyeanzisha hiii staili ni Nani? Kwenye Mei Mosi 2022 she did the same.
Akiwa Kwenye Mikutano hataki Mabango wala walioonewa wamweleze jambo? So awe mpole anapoona wateule wake wanafanya kama yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…