Iran ni nchi tajiri yenye silaha za maangamizi sio kikundi kama Hamas, ni wazungu ambao hivi sasa wanakutana na kuomba cease fire. Angalia TV acha kujidanganya, nyuma ya Iran kuna Russia, China na Turkey wote watatuma silaha Iran zikafanyiwe majaribio Israel. Iran wameonya Israel isijaribu kujibu wataangamia.
Bado huijui Iran ambayo Marekani inahangaika nayo kuzuia uzalishaji wa silaha za nyuklia ambapo wanasayansi wake sita wa nyuklia wamewindwa na kuuawa.
Marekani wameiambia Israel haitajiingiza katika vita iwapo watajibu mapigo. Hawamo!!
Waziri mkuu wa Israel hadi sasa yuko kimya na si kawaida yake.
Huko mashariki ya kati kunatisha hivi sasa baada ya makombora ya Iran kurushwa jana, na mengine wameona yalitoka Syria na Iraq.
Wazungu wameambiwa wasiende huko kwasasa kunatisha.
Hii ni vita ya tembo na athari zake zitafika duniani kote hadi bongo.
Source : Al Jazeera TV
Amka