Zanzibar 2020 VIDEO - KAMPENI ZANZIBAR: Tundu Lissu awapa somo muhimu Wazanzibar na Watanganyika juu ya Muungano. Je, Magufuli - CCM anaijua historia hii kweli?

Kwa sababu za ulinzi hatuwezi jitenga na Zanzibar. Sehemu ya bahari pia itakayoimiliki Zanzibar baada ya kutengana inatulazimu kuhakikisha Zanzibar ni part ya Tz. Kijografia hizi hazikupaswa kuwa nchi mbili sema ndio tayari ipo hivyo.
 
Anayekoleza na kufurahia Muungano wetu usiwepo badala ya hoja za nini kifanyike, huyo ni wa kupuuzwa na huenda akili yake iko tumboni
 
Mimi Ni CCM kindaki daki, Ila kwenye hili niwe muwazi. Nimeweka uchama pembeni, nikiwa Kama mtanzania nasema kwa dhati ya moyo wangu, Tundu Lissu hastahili kuwa Rais wetu
Ni hafai kabisaaa
 
Mimi sio mwanasheria "Ni yeye" ni mwanasheria nguli. Anajua kuwa Kati ya mambo ambayo ni very sensitive ni pamoja na suala la Muungano.

Hivi akiambiwa athibitishe kuwa "Hayati Karume alilazimishwa kusaini hati ya Muungano, atathibitisha"?.
 
Kwa sababu za ulinzi hatuwezi jitenga na Zanzibar. Sehemu ya bahari pia itakayoimiliki zanzibar baada ya kutengana inatulazimu kuhakikisha Zanzibar ni part ya Tz. Kijografia hizi hazikupaswa kuwa nchi mbili sema ndo tayari ipo hivyo.
Kabisa
 
Kwa sababu za ulinzi hatuwezi jitenga na Zanzibar. Sehemu ya bahari pia itakayoimiliki zanzibar baada ya kutengana inatulazimu kuhakikisha Zanzibar ni part ya Tz. Kijografia hizi hazikupaswa kuwa nchi mbili sema ndo tayari ipo hivyo.
Muungano ni muhimu saana, Tanganyika na Zanzibar zikitengana usalama wa kila upande utakua mashakani, na mizozo ndo itaibuka mingi
 
Bara na visiwani tumeshakuwa ndugu. Tuna muingiliano wa damu na kijamii.

Muungano nao ni muhimu sana kwa usalama wa pande zote. Lissu analeta mentality za kikoloni kwani anataka turudi kwenye kifungo cha mipaka ya kikoloni kwasababu za kisiasa.

Changamoto za Muungano zishughulikiwe kwa umakini na ustaarabu wa halinya juu

Amenishangaza Sana huyu mwamba
 
Tuliona hili nikaandika huu uzi

CCM versus Opposition: Political Lessons to Learn
 
Historia ya watu wa KLM/ Kanda ya kaskazini inajulikana? Unajua Base on history hakuna kitu kinaitwa Tanzania.

Well hii haiondoi ukweli kuwa Tl ana akili, akili nyingi.

kuna madhara pia ya kuwa na akili nyingi. Na hili analolihubiri la Wanzanzibari na nchi yao ni moja ya madhara ya kutumia akili nyingi kuongoza ilihali unaongoza watu wa kawaida kabisa.

Raia wa Tz na Zanzibar hawana shida na namna ya muungano au jina lilivyo sijui mfumo wa madaraka, hilo si tatizo kwao.

Watu wenye akili ya ziada kama Tl wana uwezo wa kuwafanya raia wakabadili fikra zao, na baada ya kubadili fikra na kuanza kupigania majina kuwa huku ni zanzibar na kule ni bara wakafanikiwa na kushinda hiyo vita ya majina bado matatizo waliyonayo yataendelea kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…