Zanzibar 2020 VIDEO - KAMPENI ZANZIBAR: Tundu Lissu awapa somo muhimu Wazanzibar na Watanganyika juu ya Muungano. Je, Magufuli - CCM anaijua historia hii kweli?

Zanzibar 2020 VIDEO - KAMPENI ZANZIBAR: Tundu Lissu awapa somo muhimu Wazanzibar na Watanganyika juu ya Muungano. Je, Magufuli - CCM anaijua historia hii kweli?

Watz wa leo sio wa 2015 kuaminishwa upuuzi kama huu
Sio upuuzi na wewe unajua ni kweli nisemacho. We unafikiri kikinuka Lissu atakimbilia Ikungi? Big NO, mzee atasepa na familia yake Ubelgiji, kazi atatuachia Mimi na wewe na ndugu zetu
 
Ni ngumu sana kwa JPM kwenda kuzima moto huu, kwa sababu hata ndani ya chama wanajua masuala ya Muungano huwa yanaleta msuguano sana. Unakumbuka mjumbe wa bunge la Muungano toka Zenji jinsi alivyotetea maslahi yao na kutimuliwa bungeni?
Baada ya kuteuliwa Mwinyi Kama mgombea , Kuna mjumbe wa Zanzibar alitoka mkutano mkuu akiwa analia
 
Hata ningekuwa wa Lesotho, nimeuliza swali muhimu Sana kwa mustakabali wa Tanzania. Huyo mgombea wenu anatakiwa aungane na wanaharakati wenzie. Amethibitisha kuwa hana sifa hata robo za kuwa mkui wa nchi
Muuliza swali ndiye anayeona kuwa swali lake ni muhimu sana!!
Maajabu haya. Kilaza anapota kuonekana mbele ya jamii kuwa yeye yupo vizuri kichwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa hajawahi kuupenda Muungano wale hajawahi kumpenda Nyerere anamchukia sasa.

Sioni mantiki ya candidacy yake, kama anaona Muungano ni batilii.

He is a threat to our national security..
 
..tatizo lenu ccm huwa hamumsikiliza kwa umakini Tundu Lissu.

..mnamjibu vitu visivyokwepo, na matokeo yake mnampaisha.

..TL amesema msimamo wake ni SERIKALI TATU.

..na hayo pia ni mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba.

..Tume ya Warioba ilikuwa hata na wajumbe waZanzibari wasioutaka muungano, lakini waliweza ku-compromise na kupendekeza serikali 3.
Misukule imeambiwa ijibu hoja,wao badala ya kuelewa hoja,wanasikiliza kwa ajili ya kujibu badala ya kuelewa.
Chama cha mbogamboga kinawapenda sana hawa wanufaika wa mfumo jinga wa elimu wa CCM,kwani hawajui kuhoji wala kuwa na utashi wao.
Malipo kidogo tu,wanafanya chochote kama maroboti au misukule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM kindakindaki ndo nn? mwaka huu hata shetani akisimama tutampa kura kuliko binadamu mwenye ndimi mbili
CCM kindakindaki ndio wale wanaofanya usafi na kusukuma mafile pale Lumumba na White House. Wao wakiambiwa wafanye hiki au kile kwa ajili ya chama chao,wanatenda kama "headless chicken".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko umemfikisha mbali sana,hata kuiona hajawahi. Hawa masikini misukule ya mbogamboga ni walinda matumbo ya mabosi wao tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Residentura,

Kwa hashima tuu nikujibu Tena kwani nilishamjibu muhusika

Kwako na kwa wengine wote, ifahamike kuwa mimi ninasoma kwelikweli, sibahatishi.

Mchakato wa katiba mpya mpaka kufikia katiba inayopendekezwa, naujua mwanzo mwisho. Nimesoma na kuelewa kila kitu.

Ilani za uchaguzi ninazo za CCM, ACT- Wazalendo na CDM.

#Am heavyweight bro
 
Huyu kweli anastahili kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Kwa kauli hizi, si ni wazi ameonesha kuwa atavunja Muungano?
Muungano unanyanganya Uhuru wa watu ni muungano gani,Huyu anataka kuuboresha uwe bora zaidi kwa kila pande ya muungano
 
Anayekoleza na kufurahia Muungano wetu usiwepo badala ya hoja za nini kifanyike, huyo ni wa kupuuzwa na huenda akili yake iko tumboni
Rasmu ya pili ya katiba inaeleza nini kifanyike mkuu.we are so sorry if huwezi kujisomea
 
Hayo maneno anayoyasema Lissu sio mapya. Yameshahubiriwa na wengi huko nyuma na hayana impact.
 
Baada ya kuteuliwa Mwinyi Kama mgombea , Kuna mjumbe wa Zanzibar alitoka mkutano mkuu akiwa analia
Naikumbuka sana hio scenario bro. Yule ni mwakiishi halisi wa hisia za Wazenji. Ndio sababu baada ya Mwinyi kuteuliwa, zile amsha amsha hazikuwepo kabisa pale Dodoma, kwa sababu wenye nchi yao walitaka aidha awe Mbarawa ama Nahodha. The same kwa yule mwanasheria wa bunge la katiba aliyepingana na msimamo wa serikali yake.
 
Rasmu ya pili ya katiba inaeleza nini kifanyike mkuu.we are so sorry if huwezi kujisomea
Tukiondoa uvyama! To be honest, this should not be an agenda to pray for votes through provocation and to show the way for Zanzibaris to break our union! Mkuu, hili halina Afya hata kidogo, halina manufaa Kwa Vyama pinzani Wala Kwa CCM na Chama chochote

Bali linaondoa mshikamano wetu, Jiulize, ikitokea Zanzibar imevunja muungano huu, na ikaamua kukataa mazungumzo yoyote kuhusu kuboresha muungano, Je, Zitto atakuwa na faida ipi? Je mh Lisu atakuwa na faida ipi? Je Vyama vyao vitanufaika nini sasa, Nataka nikuhakikishie Liitokeo Hilo huku Bala, Lisu anaweza kuongeza maadui wengi ambao ni wazanzibar wanaonufaika na muungano wetu, na watanganyika walioko Zanzibar hawatamwelewa huyu mtu

Hoja hiyo, ilikuwa ni Baada ya ushindi kupatikana ni kuitana Ili kuondoa kasoro zilizopo na sio Maneno ya kichochezi hadharani kiasi hiko
 
Lissu anazidi kujipotezea sifa na uhalali wa kuwa Rais wa Tanzania.

Kwa kauli yake hiyo anawachonganisha na kugombanisha Watanganyika na Wazanzibari ambao ndio kwa pamoja wanaunda Tanzania ambayo yeye anajinadi achaguliwe kuiongoza....Nadhani hata hajui kama Sasa anataka urais wa Tanganyika au wa Tanzania?

Rais kama huyu ni wa kumwogopa kama ukoma kwani ataiweka nchi reheni na atakuwa anachochea mifarakano ya kijamii kila uchao kwa kukubali kutumiwa na mabeberu, wanaofikia dau lake. Bila shaka Mola atatunusuru na majaribu ya dumbwana hili.
Kaongea ukweli mchungu na huu ukweli utabaki kuwa ukweli milele.
 
Back
Top Bottom