Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Bahari Zanzibar Shekha Ahmed Mohamed, amekiri kupokea taarifa za kujirusha baharini kwa kijana huyo Mahmoud Mwalim Saleh ‘30’ wakati akiwa kwenye Boti ya Zanzibar 3 iliyokua ikitokea Pemba kurejea Zanzibar
Tukio hilo limetokea majira ya saa 4:30 asubuhi wakati Boti hiyo ikitokea Pemba ilipofika eneo la Fungu Mayale ndipo kijana huyo alipojirusha.
Boti hiyo ilizunguka maeneo hayo mara tatu kwaajili ya kufanya doria ya kumtafuta lakini haikufanikiwa kumuona, pia Kikosi cha KMKM kilifanya juhudi za kumtafuta lakini hakuonekana.
Daah inasemekana jamaa alikuwa mgonjwa wa afya ya akili na kabla hata ya safar alimpigia mama yake simu akimweleza kwamba anaumwa sana mama yake akamsihi sana atulie na inaonyesha huyo jamaa aliyevaa tishezi nyeupe ndie aliyekabidhiwa kumchunga ila ndio hivyo sijui alisinzia ama vip
mental health is real.....kule Facebook kuna wagonjwa wengi wa akili....ukitaka kulifahamu hilo nenda Facebook tafuta group la vyakula vya kitanzania....nafikili hata admins wao ni wagonjwa ila suala la muda tu....
Hata tembea yake tuu inaonyesha ni mgonjwa...mm ninavyoogopa maji ndo nikajirushe humo lol...maji mengii hivyo meusiiiiiii...mbona kifo kibaya sana hiko?