Video: Kijiji kizima kimenaswa kimeiba umeme Mbeya

Haiwezekani Kijiji kizima wawe wezi pasipo msaada wa watumishi wa TANESCO.Je mwananchi akitumia utaratibu wa kawaida,atatumia muda Gani kuwekewa ummeme?Tusidanganyane vishoka wametumia fursa ya tanesco kuchelewa kutoa huduma bila shuruti na kuwarubuni wananchi.
 
Je waliunganishaje kutoka kwenye chanzo kikuu cha umeme?

Je walikuwa hawanunui Luku? Na kama wananunua si pesa ilikuwa inaingia moja kwa moja?
Habari

Uunganishaji umeme unaanzia pale ilipoishia njia ya umeme wa msongo mdogo(existing LV Line).

Aidha, Wananchi hao walikuwa hawanunui umeme Kwani mita zao zilikuwa mbovu kwa lugha nyepesi zilikuwa Kama picha tu.

Hivyo hakuna pesa ilikuwa inaingia, na kwa kitendo hicho wameliingiza shirika hasara.

Asante. ^MY
 
Ahsante MY
 
Waliokamata ndio waliowawekea umeme na mita mbovu za Tanesco, ni mchezo wa wafanyakazi wa Tanesco.
 
Tunasema kila siku hawa waabudu masanamu wameihujumu hii nchi tokea enzi ya nyerere mpaka leo shule hazina vyoo halafu wanajiita wasomi vibaka wakubwa hawa
Hiko kijiji nina uhakika hakuna shehe hata mmoja
 
Watu8

Habari

Hakuna uhalali wa mtu kuvunja sheria iwe ni TANESCO au mwananchi. Uunganishaji umeme unaenda kwa utaratibu ndiyo maana serikali ilianza na vijiji ambavyo ni zaidi ya elfu 12 na kupeleka umeme na tayari zoezi hilo limekamilika.

Na sasa ni zamu ya vitongoji ambavyo ni zaidi ya elfu 64 na hadi sasa nusu yake vimefikiwa na miradi mingine inaendelea. Lengo la serikali ni kuwa ifikapo 2030 kila kitongoji kiwe na umeme.

Kwa kuzingatia mipango hiyo ni muhimu kujua usambazaji umeme ni mipango na bajeti ndiyo maana lazima upangilie muda na gharama.

Aidha, Katika kuharakisha hilo serikali kupitia wakala wa umeme vijijini REA wamefanya kazi kubwa, kulielewa hilo lazima uzingatie hiyo Tathimini ya vijiji vyote ujue na vitongoji vilivyopo nchini na siyo sahihi kubeza juhudi hizo.

Asante
 
Aidha, Wananchi hao walikuwa hawanunui umeme Kwani mita zao zilikuwa mbovu kwa lugha nyepesi zilikuwa Kama picha tu.
Mnatumia utaratibu gani ku disposal mita mbovu na nyara nyingine.

Imekuwaje hizo mita mbovu zimeangukia kwenye mikono ya wananchi.

Shida inaanzia kwenye utendaji wa shirika. Wafanyakazi wa wenu wamechukua mita mbovu na kwenda kuwaunganishia wananchi.

Aliyehujumu shirika apo ni nani ?

wananchi wametapeliwa na wafanyakazi wa TANESCO . Mnawaonea tu bure.

Mngelipa thamani shirika lenu. Kama lilivo la thamani.
 
Hivi ukishalipia kuungwa huduma ya umeme.....inachukua muda gani kuja kuungwa?

Nahisi kuna shida uko tanesco.....na apo kwenye shida vishoka ndo wanapopatia upigaji
 
Je waliunganishaje kutoka kwenye chanzo kikuu cha umeme?

Je walikuwa hawanunui Luku? Na kama wananunua si pesa ilikuwa inaingia moja kwa moja?

Ili uweze kununua LUKU ni lazima uwe na mita namba iliyo hai...

Na ili uwe na mita namba iliyo hai ni lazima wewe mwenye mita na mita yenyewe viwe vimesajiliwa kwenye mfumo wa wateja/LUKU...

Hawa walikuwa na mita za LUKU kama kanyaboya, pale mahali kwenye input terminals za umeme wa Tanesco unapoingia kwenye LUKU pamewekwa jumper kubypass mfumo wa meter reading na kwenda moja kwa moja kwenye terminal za kupeleka umeme ndani...

Hapo Tanesco wasipofanya ukaguzi kama huo, utakula umeme wa bure maisha yako yote...

Ila sasa jumba bovu litakuja kukuangukia siku ikitokea shida au ukaguzi, maana hautakuwa na records zozote za manunuzi ya umeme, na hapo ndipo utajikuta unafunguliwa kesi kubwa ya Uhujumu uchumi...😃
 
Aidha, Katika kuharakisha hilo serikali kupitia wakala wa umeme vijijini REA wamefanya kazi kubwa, kulielewa hilo lazima uzingatie hiyo Tathimini ya vijiji vyote ujue na vitongoji vilivyopo nchini na siyo sahihi kubeza juhudi hizo.

Bobu usiwatete sana hao REA pamoja na kwamba juhudi zao zimeonekana na wamefanya kazi nzuri ukilinganisha na kipindi hakuna REA...

Lakini si muda mrefu walikuwa wanajifanya kana kwamba kazi ya kusambaza umeme vijijini imemalizika, kiasi kwamba wakawa wanataka waanze kupewa kazi za kusambaza nishati safi ya gesi/ na gesi asilia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…