Video: Kijiji kizima kimenaswa kimeiba umeme Mbeya

Aiseee 😃
 
Suluhisho la kiutuuzima:
Hao inaonekana ni wahitaji wa umeme na huenda mbambamba za tanesco ndiyo zimefanya wapite na option hiyo. Hao waunganishiwe umeme kikawaida tena bila malipo na wapewe onyo, hizo hatua kali wanazoongelea wanataka kuwapiga faini babu zetu washindwe kulima mwaka huu? Viongozi na ma tycoon wanaila nchi kila siku wanakijiji nao wakiionja kidogo kuna ubaya gani? kama kuna mtu atarudia tena huyo ndo ashikiliwe sasa
 
Rudi kwenye mjadala wa tukio lililoko mbele yetu, jibu huo wizi ulifanyika usiku au ulifanyika kwa siku moja, je, nguzo na waya zilichimbiwa ardhini zisionekane kwa siku zote walizoweza kutumia? Ukweli ni wafanyakazi wa Tanesco wanahusika ila wanataka kujisafisha baada ya kupunjana mgao.
 
Kazi yote ulifanywa na wafanyakazi wa Tanesco kwa kutumia transifoma na mita mbovu zinazopatikana Tanesco na asiye wafanyakazi hawezi kuvitoa.
 
Hili tatizo la vishoka sioni kama TANESCO mko na nia ya dhati kupambana nalo.

Vijijini wafanyakazi wenu wamewaka ka kikundi ka kunufaika na jambo hili. Mfanyakazi mmoja anafanya kazi "chafu" kwenye kijiji akimaliza anaomba kuhama, kisha wenzie wanakuja kukagua wanawapa kesi ya kujiunganishia umeme.


Haya yote nimeyajua baada ya kumtumia pesa bibi kijijini aunganishiwe umeme wakamzungusha zaidi ya miezi tisa wanamwambia mita haijatoka. Nilivoenda likizo 'nikawasha moto' ofisini engineer wa mkoa kaingia kwenye mifumo anasema mita imeshafungwa kwa mteja (mtu mwingine) na ananunua umeme kama kawaida, uzuri aliesaini kuchukua vifaa kwenye mfumo walimjua . Kwa 'moto' niliouwasha pale ofini hazikupita siku tatu wakaja kumfungia mita bibi. Hapo ndio nikayajua mengi yanayoendelea vijijini.


Mkiwachukulia hatua kali wafanyakazi wenu wasio waadilifu (kama huyu aliechukua mita ya mzee akaenda kuifunga kwingine) na mkawa na utaratibu wa kutoa elimu kwenye vijiji/vitongoji vipya mnakopeleka huduma tatizo hili litapungua kama sio kwisha.
 
Habari, ndugu mteja.

Utaratibu wa disposal wa vifaa vyote ikiwemo mita upo vizuri na unazingatia taratibu zote za kufanya disposal ya vifaa visivyotumika.

Aidha, suala la uadilifu ni jambo mtambuka linaweza kumugusa mtu yeyote. Ndiyo maana sheria haitaangia/ haiangalii mtu kwa nafasi yake.

Pia Kama ikithibitika Kama mfanyakazi amehusika sheria inachukua mkondo wake.

Hapo hakuna anayeonewa Kama umekutwa na nyara utawajibika kwa kile ulichokutwa nacho na wewe ndiye utajua Nani mwingine kwenye mnyororo huo.

Rai yetu kila mmoja azingatie utaratibu sheria siku zote ipo wazi hivyo mtu asitengeneze mazingira hatarishi kwake, badala yake ajue kila kazi Ina matokeo yake​

Asante. ^RS
 
Habari, ndugu mteja.

Tukutoe shaka Kama kuna wafanyakazi wa TANESCO Katika hili , ukaguzi huu utasaidia kuwabaini.

Asante. ^RS
 
Habari, ndugu mteja.

Mita hizo hazikuwa zimesajiliwa Kama unavyosema wala TANESCO haina shida na mtu yeyote anayefuata utaratibu.

Asante. ^RS
 
Habari, ndugu mteja.

Uzingatiaji wa taratibu ndiyo suluhisho , Kama ulivyosema athari za kuiba au kujiunganishia ni kubwa. Hivyo tuzingatie utaratibu na njia za kuomba na kuwasilisha taarifa zimerahishwa zaidi.

Asante. ^RS
 
Asante kwa taarifa mkuu
 
Ndugu, ndugu mteja.

Asante kwa maoni yako Kama taasisi tutaendelea kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakayebainika.

Asante. ^RS
 
Habari, ndugu mteja.

Unaweza kuwa na hoja na bahati mbaya hoja yako inahitji kuthibitishwa.

Na kwakuwa waliyokutwa na huduma wapo ndiyo watakao saidia kuthibisha walivyopata huduma.

TANESCO inasimamia weledi na mtu yeyote anayeenda kinyume lazima achukuliwe hatua.

Asante. ^RS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…