Video: Kwa Hali Hii Viongozi Mnapata Wapi Ujasiri wa Kutuhimiza Tulipe Kodi?

Video: Kwa Hali Hii Viongozi Mnapata Wapi Ujasiri wa Kutuhimiza Tulipe Kodi?

Ila afrika watu wanapata tabu jamani..utafikiri wako utumwani kumbe nchi yao wenyewe.
Dosari, kasoro na changamoto zilizopo ziwe fursa za za kubuni mipango na mikakati ya kuondokana na hali hiyo, daima tulalamike bila kukata tamaa tukizifanyia kazi shida na matatizo yanayotukumba 🐒

Iwe tu kama kumenya au kukatakata kitunguu, ni kikali kinawasha machoni lakini ni kiungo kitamu chenye ladha nzur sana kwenye chakula 🐒
 
Tlaatlaah, Etwege, na ChoiceVariable wameshika bomba hapo kurudi kimara bonyokwa halafu wakifika wanaanza kusifia.
binafsi niko kanda ya kati, makao makuu ya nchi nikichapa kwa bidii sana kazi ya wanainchi na wenzangu......

hata hivyo,
mbia mpya wa usafirishaji mabasi ya mwendokasi sambamba na UDART ataanza kutoa huduma hiyo, katika muda usio kua mrefu wakati wowote kuanzia sasa 🐒

ustahimilivu na subra ya wanainchi unahitajika kidogo tu. Jambo hili linafanyiwa kazi kwa nguvu sana na govt🐒
 
Likipiga mzinga na hiyo nyomi lazima bendera ipepee nusu mlingoti na vile huwaka na moto!

LATRA wako wapi?
 
kodi ni jambo la Lazima sio hiyari hata kidogo....

halihitaji kuhimizwa wala kushinikizwa, huo ni zaid ya ustaarabu na kujali.

na hiyo hali ikubadilika itakua mbaya zaid 🐒

Lipa kodi kwa hiyari bila shuruti, kwa ustawi wa Taifa, Tujenge Taifa letu kwa kulipa kodi kwa hiyari 🐒
Bila transparency na accountability kwemye matumizi ya kodi zetu mtasubiri sana.
 
Nchi ina kodi nyingi huduma hafifu. Agiza gari ndiyo utajua kodi zinavyokusanya. Almost bei ya kununua ndiyo kodi utayolipa.
Ukiagiza gari uwe na uwezo wa kulinunua mara mbili😂! Utalinunua Japan na likifika TPA utalinunua upya hapo ndio utakuwa umeweza kumiliki hio gari.
 
Watu wa Dar unaweza sema wanakula maisha ila kiukweli maisha yanawakula
Nenda pale Kimara na Mbezi mwisho asubuhi kama wapiga kura ...Unakaa foleni lisaa zima kwenda kazini bado kuminyana kama hauna nguvu habari yako kwisha.
 
Bila transparency na accountability kwemye matumizi ya kodi zetu mtasubiri sana.
transparency na accountability ni lazma ianze na mwanainchi binafsi moja moja, sio unajificha kuwajibika kulipa ushuru, na kukwepa kulipa kodi, au unajificha kwa kwa kutoa, kuomba au kuopkea rushwa, then umekaa mahali, tena kwa kuvizia unasubiri serikali iwajibike na kuwa wazi kukuletea maendeleo, wakati wewe umejificha, tena umejificha na kodi unayowajibika kuilipa na huku ukiomba, ukitoa au kupokea rushwa ya kujificha au kukwepa kulipa kodi, kwajili ya maendeleo yako 🐒

we must be responsible if we want development, and for real, if we real want transformations. Haki na maendeleo vinakwenda sambamba na wajibu 🐒
 
Hakuna raia atafanya hivyo ikiwa ukienda Hospitali pamenyooka hambaguliwi kwa mafungu wa bima na wenye cash treatment ni tofauti.

Siku ambapo report ya CAG itaheshimiwa na watu kupelekwa jela seriously, hakutakuwa na sababu ya kukwepa kodi. Leo nimesikia Billion 41 zimechezewa huko kwenye mfuko ila hutaskia wahusika wamekemewa hata kidogo.

Kiufupi wananchi wametekeleza wajibu wao kwa muda mrefu ila serikali haiwajibishi watu wanaochezea kodi za raia. Imefikia watu wamechoka sasa.

We fikiri mfano unatafuta hela kwa nguvu na shida kubwa familia iondokane na umaskini halafu mke anatapanya hela hizo bila kujua uchungu wake. Halafu ashikilie bango kwamba jukumu lako ni kumtunza mtu ambaye kwa makusudi anakuvurga haiko sawa.

This is the same kind of practice ambayo serikali inafanyia raia wake na bado inaona ina uhalali wa kudai kodi.
 
Back
Top Bottom