Pre GE2025 Video: Lissu amchabanga mwandishi wa Clouds, 'unaonekana hufuatilii kabisa maneno ninayozungumza na Media'

Pre GE2025 Video: Lissu amchabanga mwandishi wa Clouds, 'unaonekana hufuatilii kabisa maneno ninayozungumza na Media'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ila huyo dada Mbona Kama hana ufahamu wa siasa za Lissu? Ilitakiwa asome kwanza na kujiandaa.
Ni mtupu mno na alienda na maswali ya kutumwa nayo bila kufanya utafiti wake.
 
Nahisi kapewa maagizo ya kumbana Lissu, nimefuatilia hayo mahojiano hilo ni dhahiri.

Angekuwa yule Kabaye ndiye angeiweza hiyo kazi, huyu akili ndogo na ana mihemuko kafeli.
Maagizo au ndy mweupe kichwani
Hii taaluma sahivi imevamiwa!
Huyu dada alitakiwa akawahoji
Waimba singeli wakina shilole huko habari za umbea udaku

Ova
 
Amedhalilika halafu hataki kukubali, Lissu kamuonea huruma kampa somo kwamba ukienda kumuhoji mtu fuatilia mahojiano yake mengine.

Na Lissu katumia busara zaidi kwa kumtajia vyombo vya kimataifa vilivyomhoji BBC na DW, kwamba Clouds ni chombo kidogo afahamu hilo.

Sasa Kija anapomwambia Lissu hawezi kufuatilia kila kitu ni vitu gani anavyoona anaweza kuwa mzania sawa na Lissu? Mambo anayofuatilia Lissu atayaweza?
Mpumbavu sana huyo dada.
aqil kubwa wewe Nifah
 
Katikati ya mahojiano yaliyofanywa na kituo cha televisheni cha Clouds mapema leo na Tundu Lissu ambaye ameonekana akimkosoa mwandishi wa kituo hicho Kijakazi Yunus ambaye katika uulizaji wake wa maswali Lissu amedai hajui baadhi mambo akimtaka kufuatilia zaidi dhidi ya yanayoendelea katika uchaguzi wa CHADEMA.

"Unapokuja kumuinterview mtu, unapaswa angalu uwe unajua kwenye hayo masuala ambayo unataka kuyajua"
View attachment 3203354
"
Unajua maana ya "Kumchabanga" lakini? Mimi nimekuja mbio nikifikiri Lissu amempiga mwandishi kumbe ni upupu mtupu!! Shuleni ulienda kusomea ujinga au?
 
Eti siwez kufuatilia kila kitu 😢😢😢 huyu ni mwandishi. CMG wekeni watu heavy mentally kwenye vipindi serious na watu serious kama Lissu
 
Huwa namuangalia kwweli hiki kipindi hakiwezi amejaa ujuaji mwingi usiokuwa na maarifa ni kama vile anaenda kumfanyia mtu kazi..
Analysis ya kwanza
1. Anapenda kujibizana na wahojiwa wake kwa kujifanya anajua kila kitu. Mtu umemwita kwwnye kipindi chake mwache aeleze anachokijua au kukielewa Acha kumkatisha katisha ovyo huku ukitaka kutekeleza agenda zako
2. Nilifuatilia mahojiano ya jebra kambole na Yericko Nyerere kuna point ambayo Yericko Nyerere aliipopint kuwa vyombo vingi vya habari kwa muda mrefu mliacha kuiongolea chadema Lakini baada ya Tundu lissu na Mbowe kugombea nafasi moja vyombo vyote vimeonyesha interest na Chadema...kakaja juu etii ohhh si kweli oohhh sijui tumefanya hili, lile etc... wakabishana ila nadhani busara za mhojiwa akanyamaza, lkn ukweli unajulikana
2. Jana kamhoji Gerva Lyenda hivi hivi yaani haachi mtu aongee mtazamo wake anatka kumpeleka kwenye angle yake na hii Gerva naona ikawa inampa shida kiasi fulani lkn alijitahidi sana kujiweka kwa nafasi yake. Anapendq kuuliza maswali ambayo hayako relevant.

3. Sasa leo kakutana na kisiki cha mpingo lissu hajamkopesha nadhani kati ya interview za ovyo ambazo anaweza kuiona yeye ameshindwa kudeliver ni hii ya Leo. Lissu kamoutshine kabisa. Wale co-host wamejitahid lkn ni kama vile walikuwa hawajiamini kumhoji lissu. Yeye kija leo kabaki kuwa msikilizaji zaidi kwani maswali yalikuwa panched hta kabla hajayamaliza. Ni hicho kilichotokea leo. Ajifunze kuhoji watu wakubwa kama kina Tundu Lissu ukiwa umefanya homework vizuri. Amuangalie mwenzake masoud kipanya anavyokuwa katika uhojaji. Hiki kipindi kilimhitaji zaidi masoud kipanya kuliko hao 360.
leo clouds walikua ovyo kabisa, huyu kija ndo kaaibisha clouds utafikiri alikua na maelekezo toka ccm.
ruge alikua mtaalam wa ku spot vipaji na kuwapangia vipindi, sasa huyu hili eneo haliwezi aalitakiwa awe msoma habari tu, kuhoji sio kazi ya kila mtu
 
Katikati ya mahojiano yaliyofanywa na kituo cha televisheni cha Clouds mapema leo na Tundu Lissu ambaye ameonekana akimkosoa mwandishi wa kituo hicho Kijakazi Yunus ambaye katika uulizaji wake wa maswali Lissu amedai hajui baadhi mambo akimtaka kufuatilia zaidi dhidi ya yanayoendelea katika uchaguzi wa CHADEMA.

"Unapokuja kumuinterview mtu, unapaswa angalu uwe unajua kwenye hayo masuala ambayo unataka kuyajua"
View attachment 3203354
"
Kampa za ugoko safi sana.. Waandishi wengi hawanaga maandalizi ya kutosha kwenye interview
 
Back
Top Bottom