Uchaguzi 2020 Video : Maalim Seif apokelewa kwa kishindo Moshi Mjini

Uchaguzi 2020 Video : Maalim Seif apokelewa kwa kishindo Moshi Mjini

Unajua walipoenguwa madiwani na wabunge wa upinzani walidhani tutasusia uchaguzi kama wa serikali za mitaa ,waliduwaa mno siku ya ufunguzi wa kampeni ya chadema mbagala Lissu aliposema wanadhani tutasusia hiyo wasahau.

Pia chadema walicheza karata vizuri kumkataa Membe pamoja na umaarufu wake imagine wangemsimamisha halafu asuse kampeni kama anavyofanya huko ACT ,pia Zitto Kabwe na Seif ni majembe sana hawanaga uwoga
Kumbe Zitto ni mzuriii?
 
Hahaha huyu Membe ndio maana anafukuzwa, mwenyeketi wake na kiongozi wa chama chake wameshasema watampigia kura ya urais Tundu Lisu, yeye anadai bado ni mgombea wa urais wa JMT kupitia ACT.

Maalim Seif yuko jukwaani na Lisu yeye kule anawaita waandishi wa habari, akifukuzwa sijui ndio atanuka?!
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
Mpo wengi mnalipwa shillingi ngapi aisee
 
Hahaha huyu Membe ndio maana anafukuzwa, mwenyeketi wake na kiongozi wa chama chake wameshasema watampigia kura ya urais Tundu Lisu, yeye anadai bado ni mgombea wa urais wa JMT kupitia ACT.

Maalim Seif yuko jukwaani na Lisu yeye kule anawaita waandishi wa habari, akifukuzwa sijui ndio atanuka?!
Strategy hio, Membe alikuaa alternative Lissu akikatwa.

Yeye mwenyewe atakuwa anajua hawezi shinda kura za act zote Itaenda chadema.

Anachofanya ni kupinga hadharani sababu amepata ruzuku za kampeni za urais atammungaje mkono mwenzake
 
Kana kuna kitu kinanipa raha uchaguzi huu ni kuwa tuna wagombea wa kweli wa upinzani. Hakuna kampeni zilinitesa kama zile zilizopita za yule mzee tapeli aliyerejea ccm. Safari hii nina raha ya ajabu maana tunapambana na ccm, tena baada ya wapinzani kufanyiwa ukatili, uhayani na unyama wa wazi ili tufutike. Uchaguzi huu ndio umeonyesha wazi upinzani ni imani na haumalizwi kwa ujenzi wa bwawa la umeme, au wachumia tumbo kadhaa kununuliwa na ccm kwenda kuunga juhudi.
Tena wagombea wenye akili na weledi wa mambo ya siasa.
 
CCM wamejipanga sana mitandaoni. Wapo active sana kujibu kila hoja ya wapinzani. Hili ni jambo jema sana.
 
Back
Top Bottom