Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Hali ilivyo sasa hakuna kwa kukimbilia ukienda kanisani unakutana na kina lakwatare na mzee wa kawe aliyefukia watu ishirini huko moshi kijiji cha majengo..

Ukirudi serikalini mzee baba hashikiki hasikii la bara wala la pwani...bungeni ndo huko wanajadili live kumuua mbunge mwenzao..nje nako bun zinaendelea na zitazidi kuendelea...

Huenda labda mwisho wa Tanzania ya asali na maziwa umefika ...now ni kuishi kwa password

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mama ni kada/kibaraka wa shetani. Sijui wanaoenda kusali kwenye vijiwe vyake vya kijasiliamali wanadanganywa na nini? Au anawavuta kwa miungu yake ya gizagiza.
 
Mtoa mada unatusumbua,we hujui huyu mama ni mama kisur suri,
 
Pohamba,
Kwani Magufuli kwa Lissu alisemaje? si alitumia maneno hayo hayo na huyu ni aliyekuwa campain manager wake, yawezekana mauaji ni sera ya siri ya ccm na serikali ya awamu ya tano
 
Inahuzunisha kuona kiongozi wa dini kushangilia kusikia mtu kuuliwa,sijui atakuwa anatumia maandiko gani yenye kuruhusu mtu kumuua mwenzake
 
nzagambadume,
Kuna viashiria vyote kuwa, nchi yetu nzuri ya Tanzania tuliyopewa na Bwana Mungu - Yehova inaelekea kwenye upotevu na maangamizi iwapo hatutashtuka na kuchukua hatua stahiki....

Haiwezekani viongozi kama hawa watoe kauli ya kutoa uhai was binadamu kwenye platform kama ya Bunge, yet tudhanie ni jambo la kawaida tu....

Tena kauli iliyo nje kabisa ya mapenzi ya Mungu kwa vipimo vyote vya ki-Biblia inatolewa mbele ya mwakilishi wa Mungu anayeitwa "Mch. GETRUDE RWAKATARE", na badala asimame kwa ujasiri na kumkemea " kondoo" anayeonekana wazi kukengeuka, yeye naye (Mchungaji) anashangilia....!!

Sijui anatoa picha gani kwa anaowaongoza kwenye kanisa lake? Si hivyo tu, bali inapelekea watu tunaanza kujiuliza huyu ni Mchungaji kweli kweli was Mungu au ndiyo walewale sawasawa na kina Nabii Mwamposa aliyesababisha vifo vya watu karibu 40 huko Moshi - Kilimanjaro?

This is too sad!!
 
Bulembo Ni Pimbi wa kutupa 2015 alisema ccm haikabidhi nchi kwa karatasi kura.
 
Back
Top Bottom