Video: Mdada aenda saluni kusuka wakati hana hela. Alichofanyiwa na mwenye saluni tunaomba Dkt Gwajima aingilie

Video: Mdada aenda saluni kusuka wakati hana hela. Alichofanyiwa na mwenye saluni tunaomba Dkt Gwajima aingilie

Sitetei ila tujifunze kuheshimu kazi za watu utapeli mnaofanya kwa wanaume mnapeleka huko huko kwa wanawake wenzako wanaotoka nyumbani asubuhi kutafuta chochote kitu .Tabia mbaya sana hii huwezi kusuka nyoa
 
Katika phonebook yake huyo dada hana hata watu watano wa kuwapigia simu kuepukana na aibu ndogo ndogo hizi?
 
Tunifunze kukata nguo Kwa kadri ya Ukubwa wa miili yetu..
Hata hao tunaowaona wanatafuta Kuna wanaowategemea nyuma Yao,so tusichukulie kirahisi biashara za watu

Pia jikague kabla hujaomba huduma ka unacho kiwango tajwa ama labda umedondosha mahali pesa yako bila kujua.itakusaidia kutodhalilika

Mwenye biashara ukikutana na mteja wa hivi usimdhalilishe plz,mkague kama ana kitu chochote chenye thamani kichukue kama bond,muamuru akatafute Hela yako ndipo umrudishie.
Mmetumia Rasta zenu,muda wenu,nguvu na ujUzi wenu.mkimnyoa mnaambulia Nini?
 
Duh! Hadi huruma
Kwani kusuka rasta ni lazima, mambo mengine kujitakia tu.
Hahaa!!

Nilikua na demu alikua ananifilisi sana hizi mambo za kusuka.

Mie nilimpendaga akiwa na nywele fupi ila akazifuga, kila nikimshauri unapendeza ukiwa na nywele fupi anakuja juu. Kibaya zaidi hela ya kwenda kusuka mwenyewe hanq, hivyo mimi ndio nasimamia show.

Nikakaa chini nikachora mchoro mwepesi, wa kudeal na hii ishu.

Siku kaja kulala nikamnyoa kimya kimya hovyo hovyo(demu lenyewe lalavi hata halikustuka) halafu na mie nikajinyoa, asubuhi tumeamka ikaja tafsiri tumenyolewa na wachawi na uzuri wanawake wa uswazi wanaamini sana ushirikina wala hakugundua.

Ikabidi aende salon tu kupiga low cut
 
Kapendeza kunyolewa. Hana haja ya kwenda saluni bila pesa.
Dawa ya deni ni kulipa.
Ukisha pata huduma inakua deni inabidi ulipe.
Janja ya kutaka kukwepa haifai
 
Unaomba pesa una ambiwa sina una lazimisha utazani zako basi utaambiwa nenda kasuke takutumia ndo imeisha iyooo😅😅😅
 
Acheni kusumbua watu kwa vitu vidogo. Waziri ana mambo muhimu ya kufanya sio watu kunyoana nywele. Hao wenye wasusi hawana utu kumuachia mtu mmoja inakupunguzia nini? Ningekuwa karibu hapo ningemlipia huyo dada.
A share from your vast fortune.
 
Yaani vitu vya ziada ndo Waziri aingilie kati ili iweje?
Anapelekaje kichwa chake salon bila kuwa na hela?
 
Hapana wengemwambia atafute pesa pale pale au akope popote huenda huyo dada ndo pigo zake kuwakimbia wasusi

Au angeacha simu yake bondi. Akatafute hela kisha arudi kuikomboa. Ila simu yenyewe iwe smart sasa sio kitochi.
 
Back
Top Bottom