VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

Namshukuru Mungu kwa kuonekana kwao maaana huku mitaani maneno ya yalikuwa yamesha kuwa mengi kwa serikali. Mungu anaipenda serikali yetu. Hongera JPM kwa kuwa na wapelelezi walio bobea Mungu akubariki aminaa
Acha ujuha ndg, wapelelezi gani wakati wso ndio wahusika wakuu
 
tukubalii ukweli kwamba watanzania tuliopo nchinimwetu hatupo salama....
 
????????????????????????????
Napata shida Pale ninapo tafuta jibu la swali rangu na kwanini ROMA pekee ndio anaonekana mwenye kuumia??????? Daaaaaaaaaah ata sijuwi wapi TANZANIA inapoelekea ACHA NIKAE KIMYA Lakini Mh!!! Hapana

WALIKUWA WAPI WAKINA ROMA???????
 
Walikuwa jandoni na ya "jandoni yanabaki jandoni".
 
Subiri Press ya Roma kesho
 
Asante mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Dsm kwa kutimiza ahadi yako,kweli kabla ya Jumapili Roma kapatikana. Mkuu hiyo ni trailer,sasa tuna mtaka Ben Rabiu Wasanane ili hii sintofahamu iishe na end of the movie ijulikane.

Miezi mitano imemtosha,family yake inamhitaji,Watanzania tunamhitaji pia kuondoa dhana kuwa pamoja na Dsm kuwa na mwenyekiti shupavu wa ulinzi na usalama,makao makuu ya jeshi la polisi,makao makuu ya JWTZ,makao makubwa ya usalama wa taifa na ikulu yetu bado Dsm si salama kwa maisha ya wananchi wake.

Kama movie ndiyo kwanza imeanza, maisha ya Ben na wengineo ni maisha ya Watanzania wengine yanahitaji ulinzi madhubuti kwa usalama wa maisha yao,tukiruhusu unyamulenge nchini mwetu tutaiharibu amani yetu.

Mwisho,kwa umuhimu wa kipekee,tunaomba kuwajua waliomteka Roma na wenzake ikiwa pamoja na kujulishwa chimbo walilofichiwa. Mauaji ya Stakishari wahusika walijulikana,chimbo lao pia lilijulikana,hawa nao waliohusika tunataka kuwajuwa lakini pia kuangamiza kambi yao ili haki ionekane ikitendeka. Acha tuweke akiba ya maneno ilikupisha maandalizi ya kumrudisha Ben Rabiu Wasanane.

##bring back Ben alive.
 
Kwanza nimpe pole sana mshikaji wangu Roma na wenzake kwa madhila waliyoyapata, kwa hakika mashetani haya yameshindwa na yataendelea kushindwa tu.Nayaita maharamia haya mashitani kwa sababu kitendo cha kutekwa na koptezwa kwa msanii huyo kilikua cha kishetani na kiharamia.Niende mbali zaidi kwa kusema kua huenda yalikua magaidi kama walivyo Alshababu.

Baada ya kutoka kule kituo cha polisi ambapo walienda kutoa ushahida,msanii Roma na wenzake waliotoka kuelekea majumbani kuonana na familia zao ingawa waliokua dhoofu bin hali.
Alipoulizwa na waandishi wa habari waliokua wapi?alishikiliwa na nani?amefanyiwa nini?ameona nini na anasemaje? Amesema hawezi kuongea chochote kulingana na masharti ya kuachiwa kwao ispokua mengi atayasema siku ya jumatatu.

SWALI,

1.Hivi ni kweli Roma ataweza kua na ujasiri wa kusema lolote juu ya masharti aliyopewa zaidi ya kuwapgopa watesaji hao? je, kama watesaji walikua ni maharamia tu na sio vyombo vyetu vya dola atapgopa nini kuwataja au kufunguka wazi?

2.Au atasingizia kua anapisha uchunguzi na upelelezi wa kipolisi hivyo hawezi kusema chochote juu ya yaliyompata?

3.Sio ataogopa kupotezwa mazima?Maana juzi hata baada ya msanii Nay wa Mitego kuachiwa tu akasema kua yeye hana chama ilihali umma unaijua kadi yake.

4.Tuna vyombo vyenye dhamana ya kulinda usalama wa raia, Roma awe muwazi tu kuuambia umma tu alikua wapi maana kwa sasa yuko salama na anatambua kua lazima kuanzia sasa awe na tahadhari kubwa.

5.Ujasiri wa Roma Mkatoliki tuujuavyo utakuwepo tena? Au alikua akiongea na kuimba kwa vile hayajawahi kumkuta?Rejea wimbo wake wa "Mkanitupe Segerea"
 
Ukitaka kumjua mtekaji na mtesi wao jiulize haya maswali
  1. Kwa nini Babu Tale mtoto wa mjini alimface moja kwa moja Bashite kuhusu hili swala badala ya kamanda au waziri mwenye dhamana?
  2. Kwanini police hawakutoa taarifa ya sehemu walipokutwa kina Roma na hadi kufika Osterbay?
  3. Kwanini RC aliwahakikishia atapatikana kabla ya jumapili ili hali hajui aliyemteka wala hajui mahali alipo?
  4. Kwanini kina Roma wamezuiwa kuzungumza chochote na waandishi wa habari japo kutaja hata sehemu waliyokua?
  5. Kwanini Roma hajalishukuru jeshi la police wala kiongozi yeyote wa serikali kwa kupatikana kwake wakati tunaambiwa police ndio waliomfikisha pale Osterbay?
  6. Kwanini Roma alie kwa uchungu baada ya kutoka kuongea na waandishi wa habari badala ya kufurahi kurudi uraiani? Hii inaonesha bado ni mateka wa hao watesi.
 
Du kwenye viongozi wa dini umenigusa sana nilikuwa nawategemea sana ila ukimya wao kipindi hichi unanifanya niamini wanacho fundisha awakijui au hawakiamini au wanaogopa ila wakinyamaza mawe yataongea
 
Vijana wapo baina ya kifo na uhai....wametenganishwa na kiuzi chembamba ...lazima wachague moja.

Unafikiri watachagua kipi? Lazima wachague kuishi..wana familia zinawategemea.
 
Mkuu hariri Uzi wako. Kuna makosa madogo madogo ya kiuandishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…