Asante mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Dsm kwa kutimiza ahadi yako,kweli kabla ya Jumapili Roma kapatikana. Mkuu hiyo ni trailer,sasa tuna mtaka Ben Rabiu Wasanane ili hii sintofahamu iishe na end of the movie ijulikane.
Miezi mitano imemtosha,family yake inamhitaji,Watanzania tunamhitaji pia kuondoa dhana kuwa pamoja na Dsm kuwa na mwenyekiti shupavu wa ulinzi na usalama,makao makuu ya jeshi la polisi,makao makuu ya JWTZ,makao makubwa ya usalama wa taifa na ikulu yetu bado Dsm si salama kwa maisha ya wananchi wake.
Kama movie ndiyo kwanza imeanza, maisha ya Ben na wengineo ni maisha ya Watanzania wengine yanahitaji ulinzi madhubuti kwa usalama wa maisha yao,tukiruhusu unyamulenge nchini mwetu tutaiharibu amani yetu.
Mwisho,kwa umuhimu wa kipekee,tunaomba kuwajua waliomteka Roma na wenzake ikiwa pamoja na kujulishwa chimbo walilofichiwa. Mauaji ya Stakishari wahusika walijulikana,chimbo lao pia lilijulikana,hawa nao waliohusika tunataka kuwajuwa lakini pia kuangamiza kambi yao ili haki ionekane ikitendeka. Acha tuweke akiba ya maneno ilikupisha maandalizi ya kumrudisha Ben Rabiu Wasanane.
##bring back Ben alive.