Video: Msiba Urusi, imepoteza kamanda mwingine kule Ukraine

Video: Msiba Urusi, imepoteza kamanda mwingine kule Ukraine

Huwezi kumlinganisha Putin na Hitler...Hata Western leaders pamoja na kumchukia Putin hawajadiriki kumlinganisha na Hitler...Baadhi wameishia kumtaja kwa kuropoka kuwa ni war criminal...Tangu aseme hivyo Biden Hata. kumtaja Putin kwa jina anashindwa...anaishia kusema tu 'he'...na yule mwanamke wa Uingereza ambaye ni waziri wa nje naye aliropoka Jambo kuhusu Russia na kumfanya Putin aviambie vikosi vyake vya nuclear vikae tayari kwa Vita...Tangu wakati huo yule mwanamke hajazungumza Tena kuhusu Russia...

Kwa sasa hivi huyo Hitler wa Urusi anaogopwa maana tayari keshatupia mikwara kwamba hakawii kubonyeza manyuklia, ujue vita vya nyuklia hata asilimia 5% vitakua na atahri kubwa sana, ndio maana bado anatafutiwa angle pamoja na kwamba anaendelea na mauaji ya kimbari.
 
Makamanda wa Urusi wanakufa, lakini anae ongoza kwa kulia lia na kuomba msaada ni Rais wa Ukraine, sasa kama mnaua makamanda na mna uhakika wa kushinda mnalia lia nini dunia ipinge vita? kuna vitu vinachekesha sana
Analia aonewe huruma na jumuia ya kimataifa lakini mapambano lazima yaendelee
 
Mpaka sasa Rais wa Ukraine ameshahutubia mabunge 10, jana alikuwa anawalilia Japan, alipotoka akaanza kulilia dunia kuwa leo tuandamane dunia nzima, sasa unashangaa mbona kila siku analia lia yeye tu kama mambo yake ni mazuri?
Mambo yake sio mazuri maana anapigika kweli.
Ila anajitahidi na yeye kujibu mashambulizi yanayopeleka kilio kikubwa kwa adui.
Kitu ambacho wataalamu wabobezi wa mambo ya kivita hawakujua.
Watu walidhani the so called military operation ingeisha ndani ya masaa 72
 
Mambo yake sio mazuri maana anapigika kweli.
Ila anajitahidi na yeye kujibu mashambulizi yanayopeleka kilio kikubwa kwa adui.
Kitu ambacho wataalamu wabobezi wa mambo ya kivita hawakujua.
Watu walidhani the so called military operation ingeisha ndani ya masaa 72
Ngoja waje wale wasiotaka kusikia hiyo sentensi ya mwisho,watakutolea mapovu mpaka basi
 
Mpaka sasa Rais wa Ukraine ameshahutubia mabunge 10, jana alikuwa anawalilia Japan, alipotoka akaanza kulilia dunia kuwa leo tuandamane dunia nzima, sasa unashangaa mbona kila siku analia lia yeye tu kama mambo yake ni mazuri?
Tunajua mlivyokuwa frustrated na hii vita mkiongozwa na Babu yenu Putin.Rashidi Matumla mpaka sasa yuko ulingoni round ya saba akipambana na Mike Tyson
 
Unadhani Putin halii?analia kilio Cha samaki machozi yanaenda na maji!angalia kila wiki makamanda wake wanakufa,ndege zinaangushwa,vifaru vinaharibiwa,nchi umeishiwa nahitaji muhimu,vikwazo kila Kona! kaishia kuwaweka vizuizini maafisa wake wakubwa kwa hasira na uchungu,kuniambia Putin halii sio kweli sema Yule jamaa ana kiburi na pride hataki kuonyesha udhaifu ilihali moyoni ana msiba mzito....
Na kurecover kutoka kwa hii mess aliyoitafuta kwa kilanga chake itamchukua muda mrefu sana.
 
Na hiyo ndio tabia ya mwanaume , sio mwanaume kila siku unalia lia mitandaoni tu kama mtoto mdogo, Putin is a real man anafanya mambo yake anapojikwaa anatafuta solution
Na pia Zelensikky ni mwanaume kweli kweli,mwanaume unapaswa kulinda mji wako kwa gharama yoyote ile,siyo kisa jirani anakuzidi kila kitu anakuja kwako akuletee madharau na wewe umkalie kimya.
 
... kazi nzuri wananchi na jeshi la Ukraine japo ni ofisa wa rank ya chini - captain. Waueni popote waonekanapo kwenye viunga vya mitaa; mwageni damu zao kwa ujazo mwingi; pangeni maiti zao safu safu ni thawabu kuilinda nchi yenu dhidi ya mafashisti!

Unajua system ya vyeo vya navy?. Wakisema captain wa Navy black see maana yake ni kanali brother.Kwa kifupi ni kwamba navy ina system yake ya vyeo ambapo luteni wa navy landforce ni captain
 
Russia ni super power huyu ni balance ya dunia , kwahiyo super power mwengine hawezi kusogea jirani , lazima alie mkaribisha achakae
Hakuna cha Superpower tena kama tulivyokuwa tunaaminishwa na propaganda za kikomunist,kwa tunachokishuhudia kwa sasa huko Ukraine ni Chui wa makaratasi.
 
Yaani inaelekea putin anatafuta mlango wa kutokea vita kashindwa hakutegemea. Tatizo atawaambia nini warusi maana majeneza yameanza kuja.
Na mengine miili kibao ya wanajeshi wake imehifadhiwa kwenye macontainer ya freezer kule Ukraine.Nilikuwa naangalia CNN muda si mrefu.
 
My View in this kuanzia NATO, USA na RUSSIA wote ni walewale to ma-bully in different degrees (and has the world we need balance of power) Kwahio mwisho wa siku inabidi sisi tusio na hizo Nuclear na Weapons of Mass Destruction tuwabane wote walionazo wasiteketeze na hakuna mtu kwenda on that road anymore...., United Nations yenye One Country One Vote ipate Meno ili tuki-vote na kuona fulani amekengeuka twende tukampige na kumcharaza kwa mishale, Majambia au hata Risasi (na sio Biological Weapons) wala hatatutisha kutumia arsenal yake kwamba tukimuwajibisha.
Huwezi kuwa na UN yenye One Country one vote,wakati michango tu ya kuiendesha hiyo UN almost karibu ya nusu ya budget yake inachangiwa na Nchi 4 peke yake (mfano 2019-21 ni US 21%,China 12%,Japan 8.56% na Germany 6%) na wengine wamekaa nyuma wakifurahia wao kutoa michango kiduchu,kama tunahitaji tuwe na nguvu sawa huko UN,tuanze kwanza kwa kuwajibika kwenye swala la kuiendesha UN
 
Back
Top Bottom