Video: Msiba Urusi, imepoteza kamanda mwingine kule Ukraine

Mkuu propaganda ziko on both sides,ukiangalia RT ndiyo utaelewa,nachokubaliana na wewe ni kuwa Putin kazidiwa zaidi kwakuwa media zake zilitegemea zaidi Digital satellite Television za hao hao makuburu kuwafikia watu wengi zaidi Duniani,mfano kwa Africa,kitendo cha kuondolewa RT kwenye DSTV ni pigo kubwa kwa Russia upande wa propaganda zake kuwafikia wengi upande wa Africa huku akina CNN,Sky News,ljazeera na wengine wakijitawala kadri wapendavyo.
 
Hii ni ndoto Mkuu,kwamba hiyo "special operation" kama pro Russia mnavyoiita ndiyo ije kuleta new World Order πŸ˜€
 
Kitu ambacho wengi hawajui ni kuwa Putin na Russia yake wamejiandaa kwa karubu miaka 20 kupambana na Marekani na nchi za magharibi...Kila angle wamejipanga iwe kwa sanctions na hata silaha....sehemu kubwa ya Askari wa Russia walioko Ukraine ni conscripts...kwa Tanzania tunawaita national service au JKT...amefanya hivyo makusudi...jeshi lake kwa maana ya professional soldiers anaisubiri NATO Kama wataleta za kuleta...ukweli ni kuwa kwenye Vita vya nyuklia hakutakuwa na mshindi ...wote watakufa tukiwemo sisi humu wa JF na ushabiki...Russia and USA Kila mmoja Ana silaha za nyuklia zinazoweza kuiangamiza dunia hi ten times...wote tutakuwa ashes..NATO wanajua hivyo na Russia inajua...but Russia inasema it has nothing cha kupoteza...Wa magharibi wana hofu kubwa na hali hii..
 
Tulipe gharama ila hairuhusiwi Hitler mwingine dunia hii, never again.
It will never ever happen,Dunia ya sasa hakuna mtu ataruhusu hiyo kutokea,ndiyo maana wamemkalia kooni Putin,kama ulivyosema huko juu,hakutegemea kabisa outcome ya hii 'special operation πŸ˜‰" iwe hivi,alidhani vile alijivinjari Crimea na hakuna aliyehangaika nae ingekuwa hivyo hivyo na kwa Ukraine,kinachomkuta kwa sasa ni total blow pale Kremlin.
 
Huyo ni muoga sana,huoni hata kwa vikao anakaa mita 30 mbali na wasaidizi wake wa karibu kabisa,itakuwa leo umwambie aende vitani mwenyewe.Mwamba ni Zelensikky yupo kikazi zaidi mambo ya suti ameshatupa kule πŸ˜€
 
Hakuna cha Superpower tena kama tulivyokuwa tunaaminishwa na propaganda za kikomunist,kwa tunachokishuhudia kwa sasa huko Ukraine ni Chui wa makaratasi.
Chui vip wakati NATO ina nchi zaidi ya 25 lakini wanaogopa kufunga anga, wanasema wanaogopa mapigano ya moja kwa moja na Urusi, halafu wewe huku mbagala unasema hakuna super power ahahahha, Libya walifunga anga mapema tu lakin kwa Urusi wanajua nini kitatokea wakithubutu
 
Na pia Zelensikky ni mwanaume kweli kweli,mwanaume unapaswa kulinda mji wako kwa gharama yoyote ile,siyo kisa jirani anakuzidi kila kitu anakuja kwako akuletee madharau na wewe umkalie kimya.
Gharama sio kulia lia kila siku mpaka sasa amesha hutubia mabunge 10 lakini wapi, jana anasema dunia watu waandamane kupinga Urusi huku ni kuchanganyikiwa, kila linalo mjia anaropoka akiona nchi inakuwa magofu
 
Tunajua mlivyokuwa frustrated na hii vita mkiongozwa na Babu yenu Putin.Rashidi Matumla mpaka sasa yuko ulingoni round ya saba akipambana na Mike Tyson
Tunapambana na Ukraine, NATO na US , si unaona vikao aviishi kila siku ni Ukraine, cha ajabu wanamlazimisha mpaka China huu ni uoga mkubwa sana
 
Mbona bado mnambwela mbwela mpaka sasa. Superpower amegeuka kuwa chui wa makaratasi.
Leo NATO walikuwa na kikao, nakwambia mpaka vita ikiisha yule comedian atakuwa kahutubia mpaka bunge la Burundi na wale NATO watakuwa wamekaa vikao 1000, wewe unafikiri Urusi ni Libya au Iraq tutaelewana tu
 
Shehena za silaha kutoka West zinakuja kila siku, kwahiyo nazo lazima zipigwe, operation inaendelea ila yule comedy apunguze kulia lia
 
Huyo ni muoga sana,huoni hata kwa vikao anakaa mita 30 mbali na wasaidizi wake wa karibu kabisa,itakuwa leo umwambie aende vitani mwenyewe.Mwamba ni Zelensikky yupo kikazi zaidi mambo ya suti ameshatupa kule πŸ˜€
Juzi alikuwa anahutubia watu zaidi ya elfu 50, kwenye uwanja moscow wakiadhimisha miaka kadhaa ya kuichukua Crimea sasa unasema kajificha wapi tena? alikuwa hadharani kwenye halaiki ya watu, Putin sio mtu wa kuyumbishwa
 
Sasas wewe uliyeko Manzese kwa mfuga mbwa ndiyo unasema NATO wanamuogopa,yes ni Chui wa makaratasi tena yule wa kuchorwa na mtoto wa Lower Kindergaten ClassπŸ™‚
 
Gharama sio kulia lia kila siku mpaka sasa amesha hutubia mabunge 10 lakini wapi, jana anasema dunia watu waandamane kupinga Urusi huku ni kuchanganyikiwa, kila linalo mjia anaropoka akiona nchi inakuwa magofu
Tunajua jinsi mlivyo panic Pro Russia,hamkutegemea operation ya masaa 72 igeuke kuwa hivi ilivyo.Usije na blaha blah zenu za kuniuliza US alitumia siku ngapi Irak hapa maana ndiyo kichaka chenu mkikumbushwa "special operation ya masaa 72"πŸ˜€
 
Tunapambana na Ukraine, NATO na US , si unaona vikao aviishi kila siku ni Ukraine, cha ajabu wanamlazimisha mpaka China huu ni uoga mkubwa sana
Teh teh teh,'Special operation ya masaa 72" πŸ™‚
 
Leo NATO walikuwa na kikao, nakwambia mpaka vita ikiisha yule comedian atakuwa kahutubia mpaka bunge la Burundi na wale NATO watakuwa wamekaa vikao 1000, wewe unafikiri Urusi ni Libya au Iraq tutaelewana tu
Wakati Putin anatumia maguvu bila akili,wenzie wanampiga kisayansi,wanabonyeza tu kitufe cha sanctions,mtu analia kama paka aliyebanwa mlangoni.Kina Biden wanamaliza vikao wanapop champagne na maisha kwenye mataifa yao yanaendelea kama kawaida huku Mwamba Zelensikky akipatiwa kila kitu anachokitaka.Hebu nikuulize,vile vikwazo Russia alivyowawekea kina Biden vina madhara gani kwao? πŸ™‚
 
Juzi alikuwa anahutubia watu zaidi ya elfu 50, kwenye uwanja moscow wakiadhimisha miaka kadhaa ya kuichukua Crimea sasa unasema kajificha wapi tena? alikuwa hadharani kwenye halaiki ya watu, Putin sio mtu wa kuyumbishwa
Sasa hao si wamesombwa kutoka Crimea,sherehe za Crimea ahutubie Moscow,alishindwa nini kwend huko huko Crimea kuwahutubia kama sio uoga wake na ndiyo maana nasisitiza ni Chui wa kuchorwa kwenye makaratasi tuπŸ™‚
 
Sanctions wanapigwa warusia wanaumia nchi za ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…