kambitza
JF-Expert Member
- Jul 24, 2013
- 2,045
- 1,320
Sina tatizo na midahalo lakini ninatatizo na yaliyojificha nyuma yake. Mzee Warioba kwa nafasi yake alitakiwa kukaa mbali nayo na sisi pia tulipaswa kuipuuza na kuwapuuza wanaoiandaa. Hii midahalo ina watu nyuma wenye malengo tofauti na tunavyoaminishwa, hao watu wanatumia nguvu kubwa ya pesa ili kutugawa. Wana watu wamewapandikiza kwenye Magazeti, Vyama vya siasa vyote ikiwemo na Ccm, Serikali, NGO na Nk. Haimaanishi kuwa katika hizo sehemu hakuna ambao wamebaki na uzalendo kwa nchi yao, wapo japokuwa wamezidiwa na uzuzu wetu sisi wananchi kushindwa kuukataa ujinga huu.