Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza

Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza

Hivi Makonda ni nani hasa?
Ni Makonda ni mhamasishaji wa vijana wahuni, ni kijana asiyejua anaenda wapi, ni kijana ambaye uwezo wake wa kufikiri umezidi kupungua siku hadi siku, ni kijana aliyejivika uwakilishi wa vijana wakati hakuna siku alipopigiwa kura kufanya hivyo. Kwa ujumla ni kijana wa kufikirika tu.
 
Inawezekana vipi Tanzania ya 2014 watu washindwe kurekodi hata kwa simu tukio zima la kupigwa kwa warioba?

Dunia ya leo ya Twitter, youtube etc inamaana hata mtandao wa JF nao wameshindwa kupandisha hiyo video au ndio walikuwa hawana facilities za kurekodi kwa simu?
 
Hawa wachumia tumbo idadi yao ni ndogo sana kuliko sisi wanamapinduzi ya kweli. Kwa Warioba ni ushindi mkubwa na kwa Magamba aibuu. Mdahalo ulikuwa wa kutoa hoja na si vurugu ili wananchi wazipime waamue na si kulazimisha mambo ambayo hayafai
 
umesahau na hii pic ya makonda kumpiga warioba

Hata hii picha haioneshi kama makonda ana mpiga warioba au ana mmwagia maji kama ulivyo ripoti jana! Tafuta picha ya makonda akimumwagia maji Warioba uweke hapa
 
makonda amejibu uzushi unaosambazwa mitandao tangu jana kuwa kampiga mzee wariyoba

mimi nilienda kama mtanzania mwingine yeyote wa kawaida ila vijana waliponyoosha mabango walitokea watu waliyotaka jumdhuru mlemavu wa macho nilitokaza kumsaidia baada ya hapo nilimsaidia pia mzee wariyoba zipo picha mtaziona

ukumbi wa ubungo plaza ni ukumbi wa kisasa sana una camera pande zote hilitukio liangaliwe vizuri mtaona kama nimefanya hilo tukio hilo

chanzo ni radio free Afrika

Kwani angekubali? huyo ni mpumbavu ambae hajitambui kama ni mpumbavu, keshafanya mambo mengi ya kipumbavu na kawaida yake ni kukanusha, kwenye bunge la katiba aliiba simu na akakanusha, kwa upumbavu wake alidhani asingejulikana kama kafanya hayo kwa kuwa kulikuwa na kundi la watu, shame on her mother, sijui mzazi wake anaficha wapi sura yake. Ujinga usikutie upofu hata mara moja aibu hii ni kwa familia yake yote na wote waliomchagua kuwa muwakilihi wao.
 
Warioba hajapigwa. Huo ulikuwa ni uzushi wa vijana walioandaliwa kufanya fujo ili ionekane kuwa CCM ndo wamefanya fujo
 
vijana hawa wametia aibu sana Tanzania, eti ndio vijana wasomi? msomi unatumika kwa maslahi ya mtu mwinge tena ya kipumbavu namana hii? usomi maana yake ni pamoja na kustaarabika sasa hawa vijana wasomi mbona wanashindwa ustaarabu na wale ambao hwajaenda shule? Kuheshimu wazee haihitaji kwenda shule.
 
Watanzania tunapaswa kujifunza demokrasia ya kweli na kuvumiliana kwa maoni kinzani. Kilichotokea ubungo plaza ni ukosefu wa subira, utovu wa nidhamu, lakini kubwa ni kutoielewa vyema demokrasia. Walioingia na mabango walipaswa kuvumiliwa na kuacha waonyeshe mabango (mawazo) yao. Kisha kutolewa kwa amani. Hata hivyo nao walipaswa kupima hali. Wangetoa hayo mabango nje ya ukumbi au wakati wa mapumziko. Ikiwa walipanga kufanya fujo, hiyo ni shauri ingine. Ninashangaa vyombo vya ulinzi vilikuwa wapi kudhibiti haya!

Tatizo kuu ninaloliona ni kuwa pamoja na kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi kwa zaidi ya miaka ishirini hatujawaandaa watu wetu kwa mabadiliko. Kuna watu wanaofikiri hakupaswi kuwa na mabadiliko ya kutawala na pale wananchi wanaposema na kutenda tofauti na mawazo yao wanalazimisha ya kwao. Tuwaandae wananchi jamani kuokoa taifa letu. Tumeyaona yaWaburkinabe tusifikiri sisi ni tofauti.
 
Halafu leo saa nne Makonda ameitisha mkutano na waandishi wa habari, huyu dogo awe makini sana, asidhani kuwa watu wote wana nia njema au tunampenda.

Kama alikuwa hakubaliani na waliokuwa makamishna sasa alienda kufanya nini?

pia warioba na wenzake ni wananchi kama wengine, sasa nashangaa watu wanasema kuwa eti apumzike!! ili iweje?

kama hatuna uvumilivu wa demokrasia ya nn tuliiruhusu?
 
vijana hawa wametia aibu sana Tanzania, eti ndio vijana wasomi? msomi unatumika kwa maslahi ya mtu mwinge tena ya kipumbavu namana hii? usomi maana yake ni pamoja na kustaarabika sasa hawa vijana wasomi mbona wanashindwa ustaarabu na wale ambao hwajaenda shule? Kuheshimu wazee haihitaji kwenda shule.

UDSM imeharibiwa sana na wajinga wa ccm. Haina thamani tena.
 
Hivi kweli makonda alialikwa alienda kufanya nini wakati alijua kabisa Warioba atapinga katiba iliyopendekezwa? Ni bora angekaa nyumbani kwake akatazama kwenye tv pale alienda kuhakikisha alichokopanga kinafanikiwa.
 
Tangulizi akili na siyo ushabiki. Ukiangalia hiyo picha inaonekana kuna mtu anajitahidi kuzuia mikono ya Makonda isimfikie Warioba. Makonda alimfuata Warioba kwaajili ya nini? Mikono ya Makonda ilikuwa inaelekezwa kwa Warioba ili afanye nini? Na nayemzuia Makonda kwa nini alikuwa akimzuia kama Makonda alionekana kuwa na nia njema?

Huyu makonda inaonekana ni rubbish. Ni takataka hii haistahili hata kuwepo katika jamii achilia mbali kuwa viongozi. Hao walimchagua labda wanafanana naye.

Hata hii picha haioneshi kama makonda ana mpiga warioba au ana mmwagia maji kama ulivyo ripoti jana! Tafuta picha ya makonda akimumwagia maji Warioba uweke hapa
 
Makonda na wenzake walikwenda kufanya nini kwenye mdahalo wa Waryoba hata kama ulikuwa ni wawazi?mbona Waryoba walishamkataa kwa kudai kuwa rasimu iliyopelekwa bungeni ni ya Waryoba na siyo ya wananchi.Kama Makonda na wafuasi wake pamoja na chama chake cha CCM wanaamini kuwa rasimu iliyotengenezwa bungeni ndiyo inayotokana na maoni ya wananchi kwa nini wahangaike kwenda kwenye mdahalo wa mtu waliyemkataa badala ya kusubiri maamuzi ya wananchi yatakayofanyika kwa njia ya kura?.
 
hata mimi sijathibitisha uzushi huu popote
makonda amejibu uzushi unaosambazwa mitandao tangu jana kuwa kampiga mzee wariyoba

mimi nilienda kama mtanzania mwingine yeyote wa kawaida ila vijana waliponyoosha mabango walitokea watu waliyotaka jumdhuru mlemavu wa macho nilitokaza kumsaidia baada ya hapo nilimsaidia pia mzee wariyoba zipo picha mtaziona

ukumbi wa ubungo plaza ni ukumbi wa kisasa sana una camera pande zote hilitukio liangaliwe vizuri mtaona kama nimefanya hilo tukio hilo

chanzo ni radio free Afrika
 
Kuna kitu kinapikwa, tunafichwa na hakiko wazi.
Team ya uchafuzi ya chadema iko kazini.
Kama kweli MAKONDA kafanya haya, basi hukumu ya mungu dhidi yake haiepukiki. Ila kama ndio ileile style ya chadema ya kuwachafua vijana wana mapinduzi,,, basi MAKONDA atatoka katika hili kama shujaa.
Nawakumbusha tuuu.
YU WAPI YULE ADUI MKUU WA CHADEMA MWINGULU NCHEMBA)
YU WAPI YULE ADUI WA KUDUMU WA CHAMA(ZZK)
YU WAPI ADUI MWINGINE WA CHADEMA ((JAKAYA MRISHO KIKWETE)
nionavyo mimi, yule aliye adui mbele ya chadema ni TUNU ya taifa letu. Tusubiri, hata makonda itathibitisha hili.
maaaaweeeeeeeee!
hapa lazima uteuliwe kuwa mkuu wa wilaya, hutaambulia buku 7 tu
 
makonda amejibu uzushi unaosambazwa mitandao tangu jana kuwa kampiga mzee wariyoba

mimi nilienda kama mtanzania mwingine yeyote wa kawaida ila vijana waliponyoosha mabango walitokea watu waliyotaka jumdhuru mlemavu wa macho nilitokaza kumsaidia baada ya hapo nilimsaidia pia mzee wariyoba zipo picha mtaziona

ukumbi wa ubungo plaza ni ukumbi wa kisasa sana una camera pande zote hilitukio liangaliwe vizuri mtaona kama nimefanya hilo tukio hilo

chanzo ni radio free Afrika

Kuratibu jambo sio lazima ulitekeleze wewe mwenyewe, unaweza kuweka mambo sawa halafu wewe ukajinafiki kutaka kusaidia. Chezea Binadamu wewe !!!
 
Back
Top Bottom