Video na picha: Waafrika weusi tii walioishi India miaka elfu 60

Video na picha: Waafrika weusi tii walioishi India miaka elfu 60

African union kazi yake ni nini, kwa nini wasiwaprotect hawa jamaa?
Swali zuri mkuu,.lakini kaa ukijua "adui" mkubwa wa andamanese ni Indian government,wanajifanya wanalinda haki za makabila asilia lakini wanaruhusu uhamiaji wa maelfu ya watu kutoka bara hindi ambao wanaenda na maradhi ya kila aina,ukweli ni kwamba serikali ya India inataka "kuwafuta" wajarawa katika visiwa vyao,sasa serikali zetu AU,UN ni watu wa sayari nyingine kabisa.
 
Je ni binadamu kama sisi?
Na je wanajua nn kuhusu Mungu?

Na kama hawajui chochote
Tukisema kwamba haya mafundisho ya dini waliyaleta kwetu wazungu ili watutawale mtabisha?

Kama Mafundisho hayo yako corect kwa nini wasikutwe na wao wanayo mafundisho yanayofanana na ya vitabu vyetu vya dini, kwa kuzingatia kuwa aliyesimamia upatikanaji wa vitabu vyetu vya dini ndiye huyo aliyetuumba pamoja na hao "weusi pori"

Ni binadamu kama sisi na sababu wao hawajachanganya sana damu (kuzaliana wao kwa wao) na kutobadilisha mazingira kwa miaka mingi vinasaba zao zina taarifa muhimu kuhusu maendeleo ya mwanadamu na pengine hata immunity ya magonjwa. Blood samples zao zilichukuliwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Labda hawana dini ila wanaamini katika supernatural powers. Huhitaji dini ili kuamini katika some divine power au labda hawaamini kabisa katika hayo mambo who knows!!
 
Hapana mkuu wa hawahii hawanavinasaba yeyote na waafrika. Hawa wapo chini ya group of People called POLYNESIANS ambao ni Tongan, Tahitians (French Polynesian), Samoans, Maoris (wale wa Newzealand) Na Hawaiian. Pia watu wa Madagascar ni Polynesian wasichana wao warembo sana.

Kuna wakati nilitaka kulera Uzi kuhusu hawa watu nikawa preoccupied.

inasemekana chimbuko lao ni taiwan dna inaonyesha
Umenitajia the Maori wa new Zealand, wana akili sana, na kwa tattoo ni kiboko
 
Imeniuma sana japo nimecheka kwa huzuni. Mwenye namba ya mkulu wao amwambie awaambie watu wake warudi home tujenge nchi kwa pamoja.
Sura zao kama za wabongo kabisa, au sioni vizuri?
 
wanaua MTU yeyote anayeingia kisiwani kwao, hadi serikali imeamua kuwaacha
Serikali haiwezi kuwaacha ktk hali hiyo, itakuwa na mpango mbadala,
kama wanauwa watu wengine wanaoingia kisiwani humo kufikia mahala pa serikali kuona hilo huenda nao wako
Anekana adui wa binadamu wengine;
sasa kama serikali inaweza kuwachukuli hivyyo maana yake ina lake jambo nyuma ya pazia,
isipokuwa haiwezi kuitangazia Dunia
 
Sio katika mantiki kama hii yako.Ninajua kuwa waafrika walikuwepo kabla ya Yesu hajafika duniaji.Sasa sijui unamaanisha nini?
Sasa jamani?! Yesu kama tujuavyo ilikuwa ni miaka elfu mbili tu,sisi tunaongelea elfu sitini ya wenzetu walio ondoka katika bara hili wakaenda kuyajaza mabara mengine.
 
mkuu Kuna mwanahistoria flan gwiji uingereza anadai hawa watu waliachwa nyuma kisiwani hapo na wenzao waliotangulia mbele Papua New Guinea, Australia na east and west pacific.

Wenyewe waliamua kubaki visiwani humo. Wataslam wamepima DNA zao zinashabiana kabisa na sisi wa east Africa na yale aborigine ya australia
Sina tatizo kwa hilo hata kidogo, sana sana ndo nazidi kupata hamu zaidi! Hadi Papua New Guinea... is a long terrible and dangerous trip hasa tukizingatia enzi hizo hapakuwa na vifaa bora! Sasa hapo ndipo ninapokosa jibu... ni nini hasa kiliwafanya wahatarishe maisha kwa kukata bahari wakati walikuwa na option nyingi tu?! Ni kwamba, kutoka kwenye makazi yao ya asili wakaelekea East na kuchukua mitumbwi wakati, hata kama ni kusaka makazi bora, bado wangeweza kuelekea West/North/South na kuanza kula pori kwa pori kama ilivyokuwa kwa Wazulu ambao hatimae walitua Mkoani Ruvuma! Labda kama walikuwa ni wakazi wa asili wa moja ya visiwa vidogo vya bahari ya Hindi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki! Impact ya Mzungu na Mwarabu kuvuruga bahari hadi Afrika inaonekana mpaka leo kwenye uchumi wao... kwamba, walivuruga bahari kutafuta kitu na kitu hicho kinaonekana hadi leo! Sasa hawa ndugu zetu pamoja na kuvuruga bahari bado hawaoneshi ni nini hasa walikuwa wanatafuta hadi ku-risk maisha yao kiasi hicho!
 
Da yan taifa kubwa kama India wameshindwa kuwapelekea ustaharabu hawa watu wamewaacha tu watembee uchi.Dah!Nimeumia sana,najua in dhambibya ubaguzi mwisho wa Sikh wakajikuta wanatembea tu pekeyao wakashindwa kufanya adaptation
Si ubaguzi ndugu suala hapa ni kuheshimu tamaduni za watu na c huko india tu huko amerika kusini yapo makabila yanayoishi promitive life mpaka leo na wameachwa hivyohivyo. Huku kwetu wapo wahadzabe na makabila mengine wanaishi uchi huko porini. Wala c suala la ubaguzi.
 
North ni baridi south ni baridi wenyewe walikuwa wamezoea hali ya kitropiki zaidi.
Umechukulia north/south ya dunia wakati nimezungumzia north/south ya hapo walipokuwa kabla! Kwavile wanatoka East Africa... let's assume from Mombasa; south wangeelekea Tanga na north wangekuwa wanaelekea Malindi, Lamu, n.k! Na kama walitokea Lindi, basi south wangekuwa wameelekea Mtwara na kama north wangekuwa wameelekea Kilwa. Rufiji, Dar n.k! Sasa nini kiliwafanya waache hizo safe routes ambazo hazikuwa na any whether/climate variations na badala yake waka-opt kuingia baharini?!
 
Umechukulia north/south ya dunia wakati nimezungumzia north/south ya hapo walipokuwa kabla! Kwavile wanatoka East Africa... let's assume from Mombasa; south wangeelekea Tanga na north wangekuwa wanaelekea Malindi, Lamu, n.k! Na kama walitokea Lindi, basi south wangekuwa wameelekea Mtwara na kama north wangekuwa wameelekea Kilwa. Rufiji, Dar n.k! Sasa nini kiliwafanya waache hizo safe routes ambazo hazikuwa na any whether/climate variations na badala yake waka-opt kuingia baharini?!
Hakuna ushahidi unao onyesha kuwa watu hawa walitumia bahari,inaonekana miaka elfu sitini ilikua ni kipindi cha (ice age) bahari zilikuwa hazija jaa kama hivi leo, kwa hiyo watu hawa walikuwa wanatembea kwa miguu pembezoni mwa bahari wakaingia yemen (asia) hadi bara hindi na kwengineko.
 
Umechukulia north/south ya dunia wakati nimezungumzia north/south ya hapo
image.jpg
Inafikirika kuwa ilikuwa hivi.
 
Pana historia nyingi humu duniani watu wanababia babia tu ila kuna vitu vingi hatuvijui sasa wale tunaowaona wameendelea wanatuingiza chaka wapendavyo kumbe nao hawajui mengine wanabuni buni tu. Shukran mleta uzi nimepata elimu bila kulipia ada stahiki.
Mimi nafikiri wakati biashara ya utumwa inaendelea ulimwenguni ktk maisha yao huko ugenini wapo waliokuwa wakitoroka na kukimbilia wasipo pajua kujificha so hamna mtu aliyeweza kujua hao watu walipo it's all about nature.....I love our mother nature.
 
Story yao nyingine nzuri ni kwamba kwa wapenzi wanapenda sana kukumbatiana. inasemekana wanaweza kukumbatiana kwa siku nzima mtu na mpenzi wake.
Mkuu ni kweli?naomba kama una details zaidi niweze kuwasoma
 
Back
Top Bottom